Monday, April 15, 2013

SEREKALI YA TANGANYIKA YATENGA SH/BILIONI 1 KWA AJILI YA KUZIKA VIONGOZI WAKATI WANANCHI HAWANA HATA CHAKULA CHAA KULA MLO MOJA


Dodoma. Serikali ya Tanganyika inayo ongozwa na Rais Jakaya Kikwete imelaumiwa kwa kutenga Sh bilioni 1 narudia tena sh bilioni 1 narudia tena sh bilioni 1 ati kwa ajili ya maziko ya viongozi huku Watanganyika wengi wakilia na umaskini mkubwa wa maisha na hata hawana chaku cha kula hata mlo moja na nyumba za kuishi wachilia mbali wanao ishi vijijini hawana hata maji safi na umeme kwao ni doto tu wanayo iyota.
Shutuma hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki bungeni kwa nyakati tofauti wabunge akiwamo wa  Viti Maalumu Lucy Owenya (Chadema) na Kangi Lugola (Mwibara-CCM) wakati wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/14.
Katika mchango wake Owenya alisema inatia aibu kuona kiasi kikubwa cha fedha kikitengwa kwa ajili ya maandalizi ya kuzika viongozi huku mambo muhimu na ambayo ni kipaumbele yakiachwa.
“Ni aibu na fedheha kubwa, hivi mmetenga kiasi hicho kwani mnajua nani atakufa na lini atakufa ndio maana mnajiandaa kumzika,” alihoji Owenya.shabashiii
Mbunge huyo alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa Serikali imeshindwa kufikiri na hasa namna ya kuwaondolea umasikini na tabu wanazopata wananchi wake lakini inawaza habari za watu wanaojiandaa kufa.
Vile vile katika mchango wake Lugola ambaye alisema asingeunga mkono hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, alihoji sababu za kutengwa kwa fedha hizo bila kujua nani atakufa lini.
Mbali na hilo, Owenya pia aliilaumu Ofisi ya Waziri kwa kushindwa kutumia mbinu mbadala za kuzuia matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi zinazotumiwa na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kwenda Dodoma kufuatilia hotuba ya Waziri Mkuu.
Alimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwatimua wakuu wa mikoa ili warudi mikoani kwao ili kuokoa fedha za walipa kodi zinazoteketea katika misafara yao mjini Dodoma pasi na sababu za msingi.

No comments:

Post a Comment