Tuesday, April 9, 2013

WATUMIAO VIBAYA SIMU ZA MKONONI,MITANDAO JAMII KUKIONA.DIMOKRASI AU WAKOMONISTI..???

SERIKALI imesema((SEREKALI IPI..?)) itachukua hatua kali za kisheria kwa atakayebainika kutumia vibaya simu za mkononi, na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi((NCHI IPI))((SIMULISEMA SEREKALI HAINA DINI SASA MBONA MUNAIPA MAADILI..?))
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukomesha vitendo hivyo.
“Hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yoyote atakayetoa kashfa na kuitukana serikali, viongozi wa serikali, dini, siasa na watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi.((NcHI IPI BASI SIUTAJE JINI YA TANGANYIKA AU YA ZANZIBAR..??
Alisema hatua hizo pia zitawakumba watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji wa picha za ngono kwenye mitandao, unyanyasaji wa watoto na ukiukaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani.((MUANZE BORAFYA,NAHODHA NA VUAI BASI WANATUKANA TU JE UTAWACHUKULIA HATU AU UNAWAOGOPA..??))
“Matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama simu za mikononi, barua pepe, na mitandao ya kijamii yanafanywa na watu wachache kwa kusambaza taarifa zenye nia ya kuchafua taifa letu,((TAIFA LIPI AU TAIFA HILI HALINA JINA..??))” alisema.
Alisema pamoja na kwamba teknolojia hiyo katika miaka ya karibuni imechangia kuleta maendeleo makubwa nchini((NCHI GANI BASI..?)), baadhi ya watu wanaitumia kwa mambo yasiyofaa.
Aliendelea kusema kuwa watu wengine wamekuwa wakiitumia kwa kufanya wizi, ujambazi, ubakaji, biashara ya dawa za kulevya na ukahaba na kusambaza siri za watu binafsi bila idhini ya wahusika.((SASA KAMA KIONGOZI ANAIBA KWELI ATAKUPA IDHINI KWELI UMUANDIKE KWENYE HABARI KUWA ANAIBA SEREKALINI JASHO LA MASINI..??))
Aidha, alisema pia hatua kali zitachukuliwa kwa wakala au kampuni ya simu yoyote itakayouza SIM card kwa mtu yeyote bila ya kuwa na kitambulisho kinachotambulika kisheria.
Alisema pia ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo wakati wa usajili wa SIM card na serikali imejipanga kuzima zote ambazo hazijasajiliwa.

No comments:

Post a Comment