Friday, May 24, 2013

POLISI NA JESHI LAWAUWA WATU WA MTWARA NCHINI TANGANYIKA KISA GESI DUUUUUUUUH!!!


Mtwara. Wakati mtu mwingine akiripotiwa kufa, hali bado ni tete katika Mji wa Mtwara kutokana na mabomu ya machozi na risasi za moto kuendelea kurindima kwenye mitaa kadhaa wakati polisi wakipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam badala ya kujimbwa na kufanya kila kitu mtwara ili vijana wafaidike na kazi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi alithibitisha kupokea mwili wa mjamzito ukiwa na tundu tumboni, linaloaminika kuwa linatokana na risasi ambazo mpaka sasa bado zinaendele kupingwa ovyo ovyo na polisi wasiojuwa kazi yao ya kulinda rai wao na badala yake ni kuwatwanga kwa risasi.

“Ni kweli kwa leo tumepokea maiti moja ya mwanamke ambaye ni mjamzito wa miezi saba akiwa amepigwa risasi tumboni,” alisema Dk Kodi. Inadaiwa kwamba mjamzito huyo ambaye jina lake halikufahamika, ameuawa akiwa nyumbani kwake. Kifo hicho ni cha pili baada ya Karim Shaibu miaka (22), mkazi wa Chikongola kuuawa juzi.

Aidha, kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa mtu mwingine ambaye jinsia yake haikujulikana aliuawa kwa bomu la machozi na mwili wake kutawanyika barabarani askari wanaendelea kuuwa tu mtwara.

Kuhusu majeruhi, Dk Kodi alisema wamefikia watu 18... “Majeruhi wa mwisho tuliyempokea ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chuno. Alikuwa amevunjwa miguu yote kwa  kupingwa  risasi.”
Umati waomba hifadhi hospitalini mjini mtwara

Umati wa watu wengi wao wakiwa kinamama na watoto wachanga na waja wazito umemiminika kwenye Hospitali ya Ligula kukimbia msako na kipigo wanacho pewa na askari wa jeshi la POLISI,FFU,na JWT wanao pita nyumba hadi nyumba unaofanywa na polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanganyika (JWT).

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamelalamikia kitendo cha polisi na jeshi la jwt kuingia katika makazi yao na nyumba zao,na kuwapiga na kuwapora mali zao.

“Magomeni A hatuna amani, askari wanaingia nyumbani kwetu, wanatupiga na kutunyang’anya simu, yaani huku Magomeni hatuna amani kabisa, tumepotezana na watoto na hatujui hata waume zetu wako wapi,” alisema mwananmke moja kwa njia ya simu akimueleza muandishi wetu wa siri aliyopo mtwara.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa alikanusha kabisa hayo waliyokuwa wakisema wanamtwara na kusema hali ni shwari na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Hadi sasa huduma za kijamii zimesimama, hakuna maduka yaliyofunguliwa, hakuna usafiri wa daladala wala pikipiki, mji upo kimya huku sauti za milio ya mabomu na bunduki ikitawala, wanajeshi waliovalia sare wametapakaa sehemu mbalimbali za mji wakiwa katika magari na pikipiki.
Nchimbi atua Mtwara, jeshi lamwaga vifaa

Dk Nchimbi aliwasili jana jioni kwa helikopta na kukutana na viongozi wa Mkoa wa Mtwara walioongozwa na Mkuu wa Mkoa, Kanali Joseph Simbakalia kujadili suala hilo.

Pia ndege kubwa ya jeshi nayo ilitua huko na wanajeshi walikuwa wakipakua vitu mbalimbali vilivyoaminika kuwa vifaa yani silaha kali.

Jeshi hilo limeombwa kuongeza kukabiliana na vurugu hizo ambazo zimesambaa sehemu mbalimbali za Mtwara.

No comments:

Post a Comment