Wednesday, July 24, 2013

MAKAMO WA KWANZA WA RAISI NCHINI ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMADA KATIKA ZIARA YAKE YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI YA KUTEMBELEA WAGONJWA NA WAFIWA.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa 

Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya 

kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali  na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjuilia hali na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi 

wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea 

wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja nchini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi 

wakati  wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa 

wa  Kusini Unguja nchini Zanzibar
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari 

iliyoandaliwa na Makamo wa Kwanza wa Rais nchini 

Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake 

Mbweni nchini  Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji mzee Ali Juma Makame wa Mkwajuni, baada ya kumjuilia hali ikiwa ni ziara ya kiongozi huyo ya kutembelea wagonjwa na wafiwa
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad akimfariji mzee Ali Juma Makame wa 

Mkwajuni,  baada ya kumjulia hali ikiwa ni ziara ya Makamo 

wa Raisi wa nchi ya Zanzibar ya  kutembelea wagonjwa na 

wafiwa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali mzee Faraji Mziwanda wa Chaani, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif 

Hamad, akimjuilia hali mzee Faraji Mziwanda wa Chaani, 

ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa 

katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Haji Makame Sangire wa Kigunda, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.  Picha zote na Salmin Said, OMKR.
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif 

Sharif  Hamad, akimjulia hali Haji Makame Sangire wa 

Kigunda, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea wagonjwa na 

wafiwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja nchini Zanzibar.

Masheikh mbali mbali walio jumuika katika nyumba ya Makamo wa Raisi Maalim Seif Shariff Hamad nchini Zanzibar katika futari aliyo wandalia Masheikh hao.
 
Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif 

Hamad akiitikia dua wakati akimjuilia hali Bi. Maryam Omar wa 

Kilimahewa Msikiti ngamia, wakati wa ziara 

yake kwa wagonjwa Mkoa wa Mjini Magharibi nchini Zanzibar.

Makamo wa Kwanza wa Rais nchini Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza waislamu kushirikiana na kusaidiana ili kudumisha umoja miongoni mwao.
Amesema umoja na mshikamano ndio nguzo ya kuzidisha mapenzi miongoni mwa waislamu, na kutaka utamaduni huo uendelezwe kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa shukrani kwa masheikh na wananchi waliojumuika nae katika futari aliyoiandaa kwa ajili ya viongozi hao wa dini, nyumbani kwake mbweni.

Amewashukuru masheikh kwa kujitokeza kwa wingi katika futari hiyo, na kwamba kitendo hicho kinaashiria mapenzi waliyonayo viongozi wa dini kwa viongozi wao wa kitaifa.
Wakati huo huo Maalim Seif amehitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa na wafiwa kwa upande wa Unguja nchini Zanzibar, baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika ziara hiyo ametembelea maeneo mbali mbali ya Wilaya za Mjini na Magharibi na kuonana na wagonjwa na wafiwa katika mitaa tofauti ikiwemo Mbweni, Tomondo, Magogoni na Mji Mkongwe.

Akiongozana na viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdulhabib Ferej na Naibu Waziri wa Elimu Zahra Ali Hamad, Maalim Seif alianza ziara mapema asubuhi katika mitaa wa Mbweni matrekta, Kiembe samaki na Mwanakwerekwe, kabla ya kusitisha ziara hiyo na kujumuika katika mazishi ya wanajeshi wawili wa Zanzibar waliouliwa Darfur nchini Sudan.

Alihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea Jimbo la Mji Mkongwe alipokwenda kuwajuilia hali na kuwafariji mzee Salim Mzee wa Darajani na mzee Ali Yussuf wa Mkunazini.
Ziara kama hiyo inatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Pemba nchini Zanzibar hivi karibuni, ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment