Friday, July 19, 2013

NCHI YA TANGANYIKA IMEPATA UHURU WAKE 1961 MPAKA LEO 2013 MUMESHINDWA KUJENGA HOSPITALI MPYA KWA RAI WENU



HICHI NI CHUMBA CHA WANAWAKE WANAO SUBIRI KUZA NCHINI TANGANYIKA NCHI HII IMEPATA UHURU TOKA MWAKA 1961 MPAKA LEO 2013 MUMESHINDWA KUJENGA HOSPITALI MPYA KWA RAI WENU WACHA HOSPITALI HATA VITANDA TU MUMESHINDWA KISHA MUNA SEMA NCHI YETU YA ZANZIBAR IKIJITEGE TUTATESEKA NA KUWA KATIKA TABU SAWA DIVYO TUNAVYOTAKA NA NYINYI TANGANYIKA KUWENI NEW YORK TUKISHAKUWA NA KILA MTU NA NCHI YAKE

Hadithi ya kuhuzunisha nchini Tanganyika Mwanahamisi Majube amelala katika kitanda cha hospitali moja ya umma nchini Tanganyika (jina kapuni) ikiwa ni  saa chache  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kujifungua.

Analia na kuugulia kwa uchungu, akilalamikia maumivu makali ya tumbo.

Kwa sababu hiyo, anamwita daktari akimweleza kuwa anahisi kuna kitu tumboni mwake na kinamuumiza mno,  lakini daktari anamjibu kuwa maumivu hayo yatatulia na niyakawaida tu.

“Nisaidieni nitakufa miye jamani Nisaidieni nitakufa miye kabla ya kumwona mtoto wangu, naumwa daktari, nakufa jamani,” daktari, nakufa jamani'' anasema Mwanahamisi.

 Anapoendelea kuita, wakunga ndani ya wodi hiyo wanaibuka na kumjibu: “Acha kudeka, ulifikiri kuzaa ni kama kucheza kamari. Nyamaza, unawapigia kelele wenzako.”

Anaendelea kuita kwa zaidi ya saa lakini bila msaada wowote na baada ya kulia kwa muda mrefu, anatupa miguu huku na kule…ananyamaza, kisha anatulia. Kumbe… Mwanahamisi amekata roho!!! amekufa.

 Mwanahamisi ni miongoni mwa wanawake  wengi nchini Tanganyika ambao hukumbana na vifo vya kuepukika wakati wa kujifungua au muda mfupi baadaye.
Vifo hivyo, vingi vinasababishwa na uzembe wa madaktari, huduma dhaifu, ukosefu wa vifaa na sababu nyingine zinazozuilika wakati wa kujifungua na nchi yao ya Tanganyika kuto kushighulikia rai wake bali iko busy kuwa vipi wataimeza nchi ya Zanzibar vipi tutawalaghai Wazanzibari vipi tutawaibia na kuwafanya masikini Wanzibari vipi wataendeleza ukoloni wao weusi wa Kitanganyika zaidi ya nchi ya Zanzibar na kuwawacha wananchi wao wakifa katika mahospitali.

 Pamoja na uchungu wa kujifungua anaoupata mwanamke, ukosefu wa vifaa tiba, maumivu mengine huyapata toka kwa baadhi ya  wahudumu wa afya.

 Hali hiyo imesababisha baadhi ya wanawake, hasa wale wanaojiweza kukimbilia katika hospitali binafsi ambapo wanapata huduma bora zaidi.

Hata hivyo, ni wanawake wachache nchini Tanganyika wenye uwezo huo wengi wao ni wake wa viongozi na matajiri walala hoi na zaidi ya asilimia 80 wanategemea hospitali za Serikali ambazo  baadhi, ndizo zenye changamoto ya kuwafanya wanawake wengi kupoteza maisha nchini Tanganyika.

1 comment:

  1. wewe ulie chapa hii habari ni mpumbvuuuu mno pili ujielewi yawezekana hata shule ujaenda hamna mwenye akili timamu anaweza kufanya ulicho kifanya.

    ReplyDelete