Tuesday, July 23, 2013

RAISI KIKWETE ASEMA TANGU UHURU NI SERA YA NCHI YETU KUTETEA WANYONGE DHIDI YA UKOLONI,UBAGUZI,UONEVU,DHULMA-HAYA YOTE ULIOSEMA NCHI YA TANGANYIKA INAIFANYIA NCHI YETU YA ZANZIBAR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Dar es Salaam.nchini Tanganyika Rais Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa Tanganyika waliouliwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya U.N na Afrika (Unamid) ambao waliouliwa.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).
“Raisi wa Tanganyika alisema lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya vijana wetu ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini watu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezesha wafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao..???
“Moja kwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na watu wote walioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani.(swali tunamuliza kikwete mbona huwatetei Wazanzibar au wao sio wanyonge..? Zanzibar hatuoni muungano tunaona ukoloni au wewe huwoni...? mumetubaguwa Wazanzibari mpaka tumechoka sasa tunataka nchi yetu au unakata kuwa hamutubaguwi..? munatuoneya katika kila kitu cha muungano nyinyi munatuoneya au hamutuonei..? mumetudhulumu mpaka nchi yetu ya Zanzibar imekuwa kama kijiji tu cha Tanganyika tulipeni basi pesa zetu tulizo towa katika benk kuu tulipeni wanajeshi wetu walio uliwa uganda mpaka leo hamujawalipa tulipeni pesa zote mulizo omba nchi za nje kwa mgongo wa Tanzania kisha mukazitia katika mfuko wa Tanganyika n.k. hiyo sio thulma..? sasa nyinyi wenyewe thulma kisha ati munakwenda nchi nyingeni kusitisha thulma sivichekesho. U.N ifanyie marekebisho sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu za kujihami ili kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza.”
Hivi karibuni, Msemaji wa Unamid, Chris Cycmanik alimwambia mwandishi wetu wa siri: “Majeshi ya U.N mjini Darfur yanaweza kufanya kazi chini ya Kifungu cha VII ambao inaruhusu kutumia nguvu lakini kwa hali iliyopo hawafanyi hivyo,” alisema.
Rais Kikwete alisema eneo hilo ni hatarishi kwa sababu hadi sasa watu 41 kutoka katika nchi mbalimbali wameuawa wakati wakilinda amani huku wengine 55 wakijeruhiwa tangu mpango wa kulinda amani ulipoanza mwaka 2007.
“Tumeshawasilisha U.N maombi kutaka Kifungu namba Sita cha kulinda amani kibadilishwe na kitumike Kifungu namba Saba ambacho kinawataka wanajeshi kujihami pindi wanapovamiwa na maadui,” alisema.
Alisema tayari amewasiliana na Rais al-Bashir akimtaka kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na tukio hilo huku akiwataka wanajeshi kutokata tamaa kwa tukio hilo na kulichukua kama changamoto katika kujilinda na kuwabaini maadui.
Aliwapa pole wafiwa na kusema Serikali na wananchi wote wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu na kuwataka kuwa na subira. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema kitendo cha waasi kuwaua wanajeshi saba wa Tanganyika ni mkakati wa vikundi vya waasi kuhakikisha kuwa jitihada za kuleta amani zinagonga mwamba.
Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanganyika (JWT), Jenerali Davis Mwamunyange alisema askari hao pamoja na wengine walikuwa wakisindikiza msafara wa walinzi wa amani uliokuwa ukitoka katika kambi yao karibu na Mji wa Nyala.
Alisema walipofika kilometa 25, katika eneo la Khor Abeche walivamiwa kwa kushtukizwa na kikundi cha watu wachache na kwa sababu hawakuwa na silaha za kujihami, walishindwa kujitetea na kusababisha vifo hivyo.  Simanzi, vilio vyatawala
Rais Kikwete aliwasili katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa saa 11.10 asubuhi na kupokewa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Jenerali Mwamunyange.
Muda mfupi baadaye, malori saba kila moja likiwa na mwili wa wanajeshi hao yaliwasili katika viwanja vya wizara hiyo.
Wakati miili hiyo ikiteremshwa kwa ajili ya kuaga, wafiwa ambao awali, walikuwa wametulia kwenye viti walianza kulia.
Rais na mkewe, Salma walianza kutoa heshima zao na kisha kuwapa mkono wa pole wafiwa.
Askari wawili wa JWT walizirai wakati utoaji huo wa heshima za mwisho ukiendelea na walibebwa na wenzao kwenda kupatiwa huduma ya kwanza.
Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza katika viwanja hivyo kiasi cha wengine kukosa nafasi ya kuingia ndani hivyo kulazimika kukaa nje hadi miili hiyo ilipoondoshwa tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa maziko.

No comments:

Post a Comment