Sunday, July 14, 2013

WANAJESHI SABA WA NCHI YA TANGANYIKA WAULIWA DARFUR NCHINI SUDAN

Dar es Salaam. Wanajeshi saba wa nchi ya Tanganyika, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wameuliwa.
Taarifa zilizolitufikia jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa nchi ya Tanganyika, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini Tanganyika.
Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa nchi ya Tanganyika wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja ikiwacha wale waliyouliwa nchini Liberia wanajeshi wa Tanganyika 11walio uliwa.
Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanganyika huko huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo ila mara hii wamewauwa saba.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanganyika (JWT) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanganyika huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa nchi ya Tanganyika kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao ati lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.
Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogelea.
Nchi ya Tanganyika ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.
Wanajeshi hao wa nchi ya Tanganyika wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur.
Aprili mwaka huu nchi ya Tanganyika ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.


Majeshi ya nchi ya Tanganyika yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanganyika inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanganyika imepeleka wanajeshi 850.“Tanganyika imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi sasa,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya wa nchi yetu ya Tanganyika yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuliwa wanajeshi wa Tanganyika 11.
“Majeshi ya nchi yetu ya Tanganyika daima hayaendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema.swali kama mumeombwa na nchi hiyo mbona wanakuuweni..??

1 comment:

  1. Hiyo Tanganyika katika ramani ni nchi gani niko ughaibuni naomba wadau mnifahamishe

    ReplyDelete