Sunday, July 21, 2013

WANAJESHI WA JWT NCHI TANGANYIKA WALITHANI DARFUR NI KAMA MTWARA NA ZANZIBAR WATAPIGA WANAVYOTAKA NA KUUWA WANAVYOTAKA


HAWA NI VIONGOZI WA CUF NCHINI TANGANYIKA WAKIONYESHA ALAMA ZA VIPIGO WALIVYO PEWA NA JESHI LA LA NCHI YAO JWT HUKO NCHINI KWAO TANGANYIKA
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Mtwara nchini Tanganyika wakiwaonyesha waandishi wa habari majeraha yanayodaiwa waliyapata baada ya kupigwa na wanajeshi wa JWT.
Viongozi watano wa Chama cha Wananchi (CUF), wamesimulia mateso na vipigo walivyovipata wakati wakiwa mikononi mwa Jeshi la Wananchi (JWT) mkoani Mtwara nchini Tanganyika.
Viongozi hao ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi (Taifa) Shaweji Mketo, Mwenyekiti Jumuiya ya Vijana (JUVICUF) wilaya ya Mtwara Vijijini, Ismail Njalu na Mwenyekiti wa wilaya ya Mtwara Mjini, Salum Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa wilaya ya Mtwara vijijini, Ismal Jamal, Katibu wa wilaya ya Mtwara Mjini, Said Kulagwa na dereva wa gari walilokuwa wakilitumia siku ya tukio, Kashinde Kalumbwana.
Pamoja na taarifa hizo kwa wanahabari, wameeleza kusudio lao la kwenda mahakamani baada ya kuwasiliana na mwanasheria wao pamoja na asasi zinazotetea haki za binadamu.
Viongozi hao wanadai kukamatwa Juni Juni 27, mwaka huu na kupata mateso yaliyowasababishia majeraha, wakiyaonesha kwa waandishi wa habari, kwamba yalifanywa na wanajeshi wa JWT.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mketo, alidai kuwa siku ya tukio walikuwa wakitoka kufuatilia madai yaliyowafikia kuhusu kuwapo wanajeshi watatu wa JWT hapa hapa nchi waliombaka mtoto (jina kapuni).
“Taarifa tulizopata nyumbani kwa mtoto huyo ni kwamba wanajeshi hao walifika hapo na kumkuta (mtoto huyo) akiwa jikoni, wakamdanganya kuwa watampa Shilingi 3,000, wakamkamata kwa nguvu wakambaka walitumia mipira, (kondom)” alidai.
Mketo alisema katika kufuatilia zaidi tukio hilo, alibaini uchunguzi wa daktari uligundua kuharibika sehemu zake za siri za mtoto huyo vibaya sana.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, aliamua kulikabidhi suala hilo kwa viongozi wa chama eneo husika ili kuendelea kufuatilia hatma yake.
Alisema baada ya kulikabidhi, wakati wakirudi Mtwara mjini, walikutana magari mawili ya JWT yakiwa yameziba barabara.

Alisema eneo hilo kulikuwa na wanajeshi zaidi ya 50 ambao baada ya wao kusimama, walikamatwa na kuanza kupigwa.
“Nilikuwa na Shilingi 85,000 mfukoni wakati tunatembezewa kipigo, mmoja wa wanajeshi alitaka kuzichukua katika kupambana naye, mwanajeshi huyo alinihoji kwa nini nagombana na kanali wa jeshi,” alidai.
Alieleza kuwa baada ya kipigo hicho, walichukuliwa kupelekwa katika kambi ya jeshi ya Lembele, ambapo waliposhushwa, mmoja wa wanajeshi aliwataka wenzake waandae peni na panadol kwa ajili yao, lakini hawakujua ilimaanisha kitu gani.
“Tulivuliwa nguo zote na kuanza kupigwa bila kujali unapigwa wapi, tulipata majeraha na kuvuja damu nyingi, “ alidai na kuongeza:
“Cha ajabu kilichofuata, yalitengenezwa maji yenye barafu ambayo ndani yake yaliwekwa pilipili na ndimu, tukawa tunamwagiwa kwenye majeraha.”
Mketo alidai kuwa kwa upande wake, aliwahi kufanyiwa upasuaji eneo la ubavuni, hivyo kutokana na mateso hayo, aliamua kuwaweka wazi wanajeshi hao juu ya tatizo lake.
Alisema licha ya kufanya hivyo, kilichotokea ni kwamba aliitwa mwanajeshi (daktari) ambaye baada ya kudhibitisha hilo, waliamriwa wanajeshi wengine wawili wamshike mikono juu na kuambulia kipigo eneo lililofanyiwa upasuaji.
“Ilifikia hatua nikatamka maneno haya, nipigeni najua mmetumwa na Pinda, baada ya mateso makali, walimuita Mkuu wa upelelezi Mtwara na polisi ili watuhoji,” alisema.
Mketo alisema baada ya mahojiano, siku iliyofuata jioni walisomewa mashtaka yao na kupelekwa gerezani ambapo huko walikataliwa kutokana na majeraha waliyokuwa nayo.
“Jeshi la magereza liliamua kutuchukua kutupeleka hospitali ya Igula kwa matibabu na baadaye waliturudisha gerezani, hadi hapo tulipoachiwa,” alisema.

Akielezea zaidi hali ya Mtwara, Mketo alisema kuwa, sio shwari na kwamba wananchi wamekuwa wakipigwa bila hatia.
Kufuatia mateso hayo, CUF imemtaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hilo kwa sababu kazi ya polisi ni kulinda sio kutesa raia.


WAMEKWENDA DARFUR SUDAN KWA MIGUU YAO WANARUDI KWENYE MASANDUKU WANAJESHI WA NCHI YA TANGANYIKA
Dar es Salaam.nchini Tanganyika Makamu wa Raisi wa nchi hiyo ya Tanganyika, Dk Mohamed Gharib Bilal jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji kupokea miili saba ya wanajeshi wa Tanganyika wa nchi hiyo waliouliwa Darfur, Sudan, Julai 13, mwaka huu.

Miili ya wanajeshi hao saba iliyowasili jana ni Sajeni Shaibu Sheha Othman, Koplo Osward Paulo Chaula, Koplo Mohamed Juma Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Peter Werema na Private Fortunatus Msofe.

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), kusini mwa Darfur imeelezwa kuwa wanajeshi hao waliouliwa na kikundi cha waasi, huku wengine 19 wakijeruhiwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yametekwa na kundi hilo.
 
Hali ilivyokuwa

Baada ya miili hiyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi saa 10:40 jioni na ndege ya Antlantis iliyotolewa na Umoja wa Mataifa(UN), mamia ya watu waliokuwapo uwanjani hapo walionekana kuingiwa na huzuni baada ya kuona miili ya marafiki, ndugu na jamaa zao ikishushwa kwenye ndege hiyo.

Baada ya ndege hiyo kuwasili, viongozi wakuu wa Serikali pamoja na wambolezaji wengine waliisogelea ndege hiyo kwa ajili ya kupokea miili ya wanajeshi hao.

Miili hiyo ilishushwa na kuingizwa kwenye magari saba ya jeshi, na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi la Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Wanajeshi hao wanatarajiwa kuagwa kesho Jumatatu katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi Upanga, baadaye miili hiyo itasafirishwa kwenda kuzikwa katika maeneo yaliyotengwa na familia zao.

Waombolezaji

Baadhi ya ndugu wa marehemu waliofika kwenye viwanja hivyo walisema kuwa walikuwa wakiwategemea sana ndugu zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema mara baada ya kupata taarifa za vifo hivyo, walishtuka na kutoamini kilichotokea huku wakieleza kuwa walikuwa wanawasiliana nao mara kwa mara wakati wakiwa Darfur.
“Tuliwasiliana na baba (Koplo Mohamed Chukilizo wa kikosi cha 41KJ, Majimaji, Nachingwea), siku chache kabla ya kifo chake, aliniambia anarudi hivi karibuni na kunitaka niendelee vizuri na masomo,” alisema Amina mtoto wa marehemu Chukilizo.

Aliongeza, “Baada ya wiki mmoja tulipewa taarifa za kifo chake, jambo hili lilitustua sana na hatukuamini kabisa.”

Amina ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Nachingwea alisema mpaka sasa hajui hatima yake katika elimu kwa sababu alikuwa akimtegemea baba yake kwa kila kitu.

Binti huyo aliyekuwa ameongozana na mama yake, hawakuwa na ndugu yeyote wa familia ya baba yake waliomsindikiza.

Chukilizo atazikwa mkoani Kigoma mara baada ya kukamilika kwa taratibu za mazishi.

Naye Msemaji wa familia wa marehemu, Sajini Shaibu Othman kutoka Makao Makuu ya Jeshi Upanga (MMJ) jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika, Mohamed Sadiki alisema kuwa marehemu ameacha mjane na watoto watatu.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, walishtuka na kutoamini kilichotokea.

“Tumeshtushwa sana na tukio hilo, hatukuamini kabisa kwa sababu tulikuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa, na ameacha mama yake mzazi, mjane na watoto watatu,”alisema Sadiki.

Aliongeza, marehemu alikuwa anaishi Kigamboni, kwamba atazikwa nchini  Zanzibar kwa maelezo kuwa ndiko familia ilikopendekeza kumzika.

Naye mke wa marehemu, Oswald Chaula kutoka kikosi 42KJ Chabruma, Songea, Maria Chaula alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walipatwa na mshangao na walikusanyika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kupanga taratibu za mazishi.

“Nilipopata taarifa za msiba huu wa mume wangu nilihisi kuchanganyikiwa. Mume wangu tegemeo langu niliomba arudi salama ili tuweze kupanga maisha yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema kwa uchungu Maria.

Hata hivyo, waombolezaji wengine walishindwa kuongeza chochote katika eneo hilo, huku wakionekana kulia wakati wote tangu walipofika kwenye eneo la uwanja huo hadi miili ya wapiganaji hao ilipowasili.
Hata hivyo, Kaimu Msemaji Mkuu wa JWT, Meja Joseph Masanja alisema kuwa, miili ya wapiganaji hao imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi kwa ajili ya kusubiri utaratibu wa kuagwa ifikapo Jumatatu ili iweze kusafirishwa vijijini kwao.

“Ratiba iliyopo ni kupokea miili ya marehemu na kwenda kuihifadhi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, na ifikapo Jumatatu majira ya saa 2:30 asubuhi itapelekwa kwenye viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi kwa ajili ya kuaga,”alisema Meja Masanja.

Dk Bilal aliongozana na mke wa Rais, Salma Kikwete,Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika kutoka nchini Zanzibar Balozi Seif Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa nchi ya Tanganyika, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanganyika (IGP)Said Mwema.


No comments:

Post a Comment