Friday, August 30, 2013

KAMA KUNA MWANAJESHI WA ZANZIBAR CONGO BASI JITAYERISHENI TENA KUZIKA MWANAKWEREKWE M23 HAWACHEZI KICKBOXING WAO WANAUWA TU


Mashirika. Mpiganaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanganyika, JWT Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na kundi la M23 la nchini congo kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.

Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanganyika wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa.

Askari wa Tanganyika na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi atii ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.

Meja Mshindo alikuwemo katika kikosi cha vifaru na alikuwa kwenye Kambi ya 83KJ iliyoko Kiluvya Dar es Salaam.

Kuuawa kwa manajeshi huyo kumekuja ikiwa ni siku 47 tangu kuuawa kwa wanajeshi wanne wa nchi ya Tanganyika na wa wili wa nchi ya Zanzibar  waliokuwa atii wakilinda amani kwenye Mji wa Darfur Sudan na Kikundi cha Janjaweed.
Msemaji wa JWT, Meja Erick Komba alikiri kutokea kifo hicho na kusema: “Jana (juzi) Agosti 28, Wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi.

“Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.”

Habari zaidi kutoka Congo zinaeleza kuwa mwili wa marehemu Meja Mshindo ulisafirishwa jana kupelekwa Entebbe, Uganda ambako ungefanyiwa matayarisho ya mwisho na tayari kwa kuletwa nchini Tanganyika.

Katika hatua nyingine, wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa, mmoja akiwa Mtanganyika na mwingine raia wa Afrika Kusini walijeruhiwa kwa bomu eneo la Munigi huko huko Congo.

Bomu hilo lilirushwa na kundi la M23 kuelekezwa kwa askari wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakikagua maeneo mbalimbali karibu na Mji wa Goma.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amelaani mashambulizi na mauaji hayo ya mwanajeshi  huyo wa Tanganyika na kusema: “Ninatoa pole kwa Tanganyika (Watanzania) Zanzibari na familia ya mpiganaji huyu na ninalaani kwa nguvu zote mauaji haya na majeruhi kwa walinzi wa amani.”

Msemaji wa UN, alisema Majeshi ya UN kwa kushirikiana na yale ya Serikali, yalianzisha mapigano makali dhidi ya kundi la M23 kwenye eneo la Kibati Kaskazini mwa Goma, kwenye Mji wa Kivu ya Kaskazini.  Majeshi ya UN na Fardc yalitumia helikopta, vifaru na askari wa miguu kutekeleza mashambulizi hayo yaliyojibiwa na kundi hilo la M23. Kwa mujibu wa msemaji huyo, mapigano bado yanaendelea je hii ndio kueka amani au wamekwenda kuzidisha vita...???

No comments:

Post a Comment