Wednesday, August 28, 2013

NCHI YA TANGANYIKA ILIFIKIRI RWANDA NA KENYA NI KAMA NCHI YA ZANZIBAR HEWALA BWANA TANGANYIKA KILA ITAKACHO SEMA.


WABUNGE WA NCHI YA RWANDA WASUSIA KIKAO CHA BUNGE LA EALA

RAIS Paul Kagame wa nchi ya Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya nchi ya Tanganyika kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete.  wa nchi ya TANGANYIKA Mwandishi wetu wa siri aliyekuwepo mjini Arusha alidokezwa.Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha nchini TANGANYIKA kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa nchi ya Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa nchi ya Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge shambashi sio wahafidhina wetu wa KIZANZIBARI KILA KITU HEWALA BWANA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA.

Mwenendo wa hayo yaliyojitokeza jana katika Bunge la Afrika Mashariki hadi kikao kuvunjika, msingi wake ni mgogoro unaowagusa wakuu hao wawili wa dola.
Habari zilizotufikia toka katika vyanzo vyake mbalimbali vilivyo ndani na nje ya mipaka ya Tanganyika, lakini pia katika vikao vya Bunge hilo la Afrika Mashariki vinavyoendelea jijini Arusha nchini TANGANYIKA zinaeleza kuwa, Rais Kagame hata kama ataalikwa kuja nchini leo, hatakuja.
MTANGANYIKA mwandishi wetu wa siri alidokezwa kuwa jambo hilo tayari limethibitishwa na Wabunge wa nchi ya Rwanda wanaohudhuria vikao vya (EALA).

Taarifa toka ndani ya Bunge hilo zilizotufikia sisi Jumatano zinaeleza kuwa, tayari mzimu wa msuguwano huo uliojitokeza baina ya wakuu hao wawili wa dola, umeanza kuwavuruga wabunge hao baada ya jana kikao cha Bunge hilo kuvunjika, kutokana na kuibuliwa kwa hoja ya kutaka vikao vya Bunge hilo kufanyika kwa utaratibu wa kuzunguka kila nchi.
Zinaeleza zaidi kuwa; Ni katika hoja hiyo wabunge wa Kenya na Rwanda walionekana kuungana na kuwa kitu kimoja na hivyo kususia kikao hicho cha jana, jambo ambalo lilimlazimisha Spika wa Bunge hilo, Magreth Zziwa kuvunja kikao.

No comments:

Post a Comment