Saturday, August 3, 2013

NCHINI TANGANYIKA BAKWATA NI MTETEZI WA WAISLAMU AU MLINDA SEREKALI YA MADHALIM..???


BARAZA KUU LA WAISLAMU NCHINI TANGANYIKA BAKWATA,Limetangaza mpango wake wakusambaza mashushushu Misikitini akitangaza mpango huo,Mufti wa Baraza hilo Sheikh Issa Shaaban Simba mesema kuwa mashushushu hao watakuwa wakitowa tarafa zao polisi. Mufti Simba amesema kuwa hatuwa hiyo inakuja kufuatia hali inayoendelaambapo amedai kuwa misikiti imegeuzwa kuwa majukwa ya siasa na hivyo kuhatarisha amani ya nchi.

Akasema baadhi ya wana siasa wamekuwa wakiwahamasishi Waislamu kuasi Bakwata kiasi cha kufikia kudai kuwa Baraza hilo lifutwe.Waislamu wanachuzwa na wana siasa Baraza la Waislamu nchini Tanganyika lifutwe misikiti si kwa jili ya siasa bali ni sehemu ya kuwaelekeza watu kutenda mema, alinukuliwa Mufti Simba Akisema,

Akaongeza kutokana na hali hiyo BAKWATA inakusudia kuanzisha kamati za Ulinzi na Usaalama Misikitini ili kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani.Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya magazeti,Sheikh Mkuu, Mufti Simba wa Bakwata amesema kuwa mpango huo umependekezwa na Mkuu wa Majeshi ya Polisi nchini Tanganyika  (IGP) Said Mwema Akisisitiza kuwa makachero hao wa Bakwata wakisha baini viashiria vya uvunjifu wa amani watatoa taarifa polisi.

Katika kufanikisha mpango huo wa ushushushu Misikiti,Maimamu na Masheikh wa Bakwata watashirikiana kwa karibu na makamanda na kwamba BAKWATA Makao Makuu itasambaza taarifa kwa maimamu wa misikiti nchini namna ya kutekeleza na kufanya mawasiliano na maofisa wa polisi, Msikiti wowote utakao kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani,taarifa itatolewa polisi (mara moja) ili kulinda amani ya nchi, Mufti Simba amesema na kunukuliwa nagazeti moja wiki iliyo pita.

Sheikh huyo Mkuu anaetambulika na serekali ya Tanganyika na sio kama wanavyomchukulia waumini wa dini ya kislamu kuwa sio kiongozi wao na wala hawaitambuwi BAKWATA kuwa na pahali paa waislamu ambapo wanaweza kueleza matatizo yao na yakatatuliwa.waumini wa dini ya kislamu wanaona kama BAKWATA ni pahala paa watu kutafuta kula yao,na pia ni pahala pamoja wapo panapo ikwamisha dini ya kislamu kupiga hatuwa mbele.

Swali ni kuwa ikiwa BAKWATA ni kwajili ya waislamu kweli mbona mpaka leo hawasema kuhusu waislamu waliouliwa MUEMBE CHAI kuwa ilikuwa sio haki kwa hiyo walio wauwa waislamu wale lazima wafikishwa mahakamani na wahukumiwe ili haki itendeke BAKWATA KIMYA. mbona watoto wa kislamu wanavuliwa hijabu mashuleni na BAKWATA KIMYA. mbona wanafunzi kibao wakislamu wanafelishwa maskuli na vyuo vikuu BAKWATA KIMYA Sheikh Mponda alishikwa na kutupwa jila BAKWATA KIMYA Quraan zinakojolewa na kuchwana BAKWATA KIMYA N.K. je hili BAKWATA NI MTETEZI WA WAISLAMU..?? AU NI JINAMIZI LIKUJUWALO HALIKULI LIKAKWISHA NDIO HIVYO LINAWALA WAISLAMU WALA HALIWAMALIZA..?

No comments:

Post a Comment