Thursday, August 15, 2013

NCHINI TANGANYIKA POLISI WAMCHUKUWA SHEIKH MPONDA HOSPITALI YA MUIMBILI NA KUMPELEKA GEREZA LA SEGEREA DUUUUH!!!!


HII NDIO AMANI ANAYO IMBWA SIKU ZOTE NA VIONGOZI AMANI AMANI MUNAIYONA

Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam 

nchini Tanganyika, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa 

na kesi mpya ati ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya 

Tanganyika amezungumzia kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka 

hositalini hadi jela ya Segerea.Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya 

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu Dar  es Salaam nchini Tanganyika amesema 

kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda 

aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na 

Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha 

kumhamishia katika gereza la Segerea.Wakili Jumaa amesema amesikitishwa na 

kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali 

Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, 

Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya 

ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.Jumaa akaongeza  kuwa   

ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa  Sheikh Ponda wodini na 

kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba  atalazimika kurudishwa tena 

mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo 

upelelezi  wa kesi hiyo bado haujakamilika.“Kwa kweli kitendo hicho kime 

nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria 

tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.  Kwa upande wao familia ya 

Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha 

kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama 

familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi 

za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa 

salama. “Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya 

serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui 

kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni 

tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili 

walizungumzie wao.”alisema Is-haq.
Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na 

Taasisi za Kiislamu  walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya 

kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu

No comments:

Post a Comment