Thursday, August 1, 2013

NGAO YA VIONGOZI WANAFIQ NCHINI ZANZIBAR NI TANGANYIKA NA KUHUBIRI KWAO KWA AMANI NA UTULIVU


HAKUNA HATA KIONGOZI MOJA KATIKA NCHI YETU YA ZANZIBAR ATAKAE MFIKIA GADDAFI KWA KILA KITU NA YEYE ALINGOLEWA ITAKUWA NYINYI VISONOKO
                                                                                                                                                                                                       
Viongozi wa nchi ya Zanzibar na Tanganyika wanalazimisha amani ambayo haipo kwa Tanganyika yenyewe wala Zanzibari yenyewe ila ipo kwa wananchi ambao tayari kupigwa, kuuwawa ,kuteswa ,kunajisiwa,kuthulumiwa, kuibiwa mali zao, lakini bado wanasema na mioyo yao na kuweka amani.

 Serikali zote mbili ya Tanganyika na Zanzibar ndio waanzilishi wa fujo na ni wavunja amani na mshikamano miongoni mwa wananchi nadiriki kusema ni Viongozi wa nchi hizi mbili Tanganyika na Zanzibar na wake zao na watoto wao na wahafidhina wao wa maskani vita zaidi ya wananchi wavunja jasho, waonewao, wanywanywasaji, wanyimwa haki zao wathulumiwa.
Mifano mingi tu ipo kwamba serikali kupitia watumishi wake ikiwa polisi ,jeshi, vyombo vya usalama ndio waanzilishi na wavunjifu wa amani katika nchi hizi mbili ya Zanzibar na Tanganyika.
Mfano mmoja ni ule wa kauli ya waziri mkuu bungeni  nchini Tanganyika,kauli yake ukiiangalia kwa kina ni kauli ya uvunjifu wa amani.


 Ukiwaamrisha polisi kupiga na kuua na wao watapigwa na kuuwawa na pengine goma hilo hilo unalolitilia chapua likakufika na wewe pia kwani unafikiri unaweza kujilinda usipatikane na maafa kama yanayowafika wenzio ,angalia Gaddafi, na  Indira gandi aliuwawa na nani kama sio hao hao wanaomlinda au hao hao unaotaka wapingwe watapingwa iko siku na wao watakuwa juu wewe utakuwa chini na wewe hapo utasemaje..??

 Amaa kwa uchochezi unaotolewa na viongozi wa mathalim wa nchi ya Zanzibar kwa Wazanzibari kisha kugeukiwa na kupigwa na vyombo vya dola na wengine kuuwawa unadhani anaetakikana kwa kulipiziwa kisasa atakosekana...??? kama ndio dhana za viongozi kuwauwa na kuwatesa wananchi kupitia vyombo vya dola kishawakachekelea na kuhubiri amani na utulivu kama kwamba wao sio walioanzisha mauaji na kipigo.

 Amani na utulivu amani na utulivu siku moja itaondoka na naapa kwa jina la aliniumba kama mkiendelea kuwanyanyasa wananchi iko siku watajilipiza na Mola wetu atawapa nguvu kwani anajua mnayoyaficha ndani ya moyo yenu.
Zanzibar ndio itakayokuwa nchi ya kwanza kuondoka hiyo amani ya uongo na utulivu wa kinafiki walipa kodi wanachotoa kuchangia kwa nguvu bila ya ridhaa zao zikiingia ndani ya mifuko ya wachache ambao dhahir shahir wanajulikana wanayoimaliza nchi ya Zanzibari yao kwa hubiri za uongo za amani na utulivu,


Mzanzibari ananyimwa haki yake ya msingi na kupewa asie na haki hiyo.
Dhulma hii itatupeleka pabaya na tayari imeshatufikisha ukingoni huku kila mmoja wetu anajua hayo,dhulma imedumu muda mrefu sasa na bado wanachimbuka wengine wapya kuukandamiza umoja wa Wazanzibari kwa jili tu ya tumbo lao na wake zao na watoto wao.
Ni kwa nini basi hamuhubiri amani  ya ukweli na uadilifu katika uongozi wenu..???
hawawezi kuhubiri hivyo na hawatahubiri hivyo mpaka roho mbichi ikiwatoka kwa papatizi za kuwadhulumu wananchi walio wengi ambao wanagaragara kwa umasikini.
Amani na Utulivu itokayo mdomoni na sio moyoni itasababisha maradhi makubwa ndani ya mioyo hiyo ambayo haitapata ponyo duniani na akhera pia.


 Ngao ya viongozi wanafiq hapa nchini Zanzibar ni Tanganyika na ndio maana hawatahubiri uhuru kamili wa nchi ya Zanzibari yetu kwani wanajua fika kwamba nchi yetu ya Zanzibari ikipata uhuru wa kujiamulia mambo yake hawatakuwa na kura ya turufu hivyo wanahiyari tuwe watumwa wa Mkoloni Mweusi Tanganyika lakini nchi yetu ya Zanzibar isijitawale.

 Yagujuuuuu nchi ya Zanzibar itajitawala kwa uwezo wa Mola wetu wakitaka wahubiri uongo na unafiq wasitake lakini Zanzibar kamili ipo Inshaa allah.

No comments:

Post a Comment