Sunday, August 11, 2013

SHEIKH MPONDA APINGWA RISASI NA POLISI MOROGORO NCHINI TANGANYIKA


Muda si mrefu moja wa wandishi wetu wa siri aliyekuwepo nchini Tanganyika amzungumza na shuhuda mmoja aliyekuwepo Morogoro. Ni kweli kuwa Sheikh PONDA amejeruhiwa vibaya kwa KUPINGWA RISASI NA POLISI. Huu ni mwendelezo wa matukio ya kuwawinda Viongozi wa dini, Viongozi wa vyama vya siasa, waandishi wa habari na wanaharakati ambao serikali mfu inaamini ni “watu hatari” au ni maduwi wa serekali ya Tanganika na serekali ya Zanzibar.
Hivi karibuni, taarifa za ndani za serikali ya Tanganyika na hata serekali ya Zanzibar zimekuwa zikimuonesha Sheikh Ponda kama “mtu hatari kwa usalama wa taifa”, huu ni upuuzi na ujinga mkuu ambao utatupeleka pabaya kama ni hatari kwa taifa basi ni hii serekali ya Tanganyika na Zanzibar ambazo hazitaki kubadilika na kusikiliza rai wanataka nini na badala yake kila anae tetea haki basi wanamuwa au wanamfunga jela bila hata kosa.
Ikiwa kuna mtu ni hatari sana kwa taifa, na serikali ya Tanganyika na Zanzibar ina ushahidi, kwa nini isimfungulie mashtaka mtu huyo na ipeleke ushahidi huo mahakamani ili mahakama ipime na kuamua au laaa!!!!
Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar inayotumia “approach” (mbinu) ya kushambulia, kujeruhi,kuwafunga jela kwa nia ya kuwaua watu wenye msimamo tofauti na serikali hizo, hii inakuwa “serikali hatari, ya kijinga, dhaifu na iliyoshindwa kuongoza”, serikali za namna hii “is more dangerous to the peace of the nation than the dangerous persons themselves” (serikali za namna hii ni serikali hatari mno kwa amani ya taifa kuliko watu inaowadhania kuwa hatari”.
Sisi sote kuanzia Tanganyika hadi nchini Zanzibar tunacho jua, Sheikh Ponda ni mwanaharakati wa kiislamu anayebeba matumaini, hoja na visheni ya waislamu walio wengi. Kwa upande mwingine serikali ya CCM inamuona Sheikh PONDA kama mtu hatari kwa sababu hoja na visheni zake zikifanikiwa zitawatoa waislamu chini ya BAKWATA ambayo inatumiwa na serikali ya Tanganyika na Zanzibar inayo ongozwa na CCM kama nyenzo ya kuwadhibiti waislamu katika masuala yao ya msingi na hata baadhi ya haki zao muhimu za kiimani,kilemu,kimaish,kiutamaduni.
Serikali yoyote ya kipuuzi na iliyokufa “a failed state” haifikiri namna ya kutafakari hoja zinazokinzana na serikali na kuzitafutia ufumbuzi mezani. Hufikiri kutumia nguvu,ubabe,matusi na kuwatisha watoa hoja husika na hata kuwaua pale nafasi inapopatikana,kama walivyo pata na kumpiga risasi Sheikh Mponga au walivyo waweka jela Masheikh wa Uamsho ilimradi udhibiti “sensorship” uendelee.
Serikali mfu kama ya CCM huwasha kiberiti yenyewe na baadaye huhaha kuzima moto ikiwalaumu watu wengine kwa matatizo yaliyoanzishwa na serikali yenyewe ya majuwa, wavivu wa kufikiri.
Ikiwa Viongozi,Wandishi wa habari na hata Rai wa kawaida tutachekelea unyama huu na kuacha fulani atambuliwe kama “mtu hatari sana” ATI kwa sababu tu yeye ni dini fulani, ni kweli mhusika atashughulikiwa ipasavyo, atateswa tutachekelea, ataumizwa tutasheherekea na atauawa tutapiga nderemo na vifijo.
Serikali mfu iliyo kufa isyo fikiria rai wake zaidi ya matumbo yao na wake zao na watoto wao haitaishia hapo, ikimaliza kumshughulikia yeye kwa dini yake itahamia kwako, itakuita “mtu hatari sana” kwa sababu ya chama chako, kwa sababu ya uanaharakati wako, kwa sababu ya uandishi wako na kwa sababu ya msimamo na mtizamo wako ambao unapingana na serikali mfu. Nani atabaki salama..???
Nyerere baba wa Tiafa la nchi ya Tanganyika  aliwahi kusema, “ukinywa damu ya mtu, utaendelea kunywa tu”. Nami nasema, tukichekelea na kukubali propaganda za CCM kuwa Sheikh Ponda ni mtu hatari sana, akishamalizwa watahamia kwetu (kwangu na kwako), mimi na wewe tutapewa “uhatari” na tutasakwa kwa mtutu wa bunduki tuuwawe haraka ili taifa libaki kuwa kimyaaa na wao wanaoza juu ya madaraka ambayo hayawanufaishi rai walio jaa umasikini.
Serikali mfu ya CCM iache mbinu hizi ambazo tulishazijua. Serikali mfu ikatatue tatizo la msingi la MZOZO WA MIONGO KADHAA KATI YAKE NA WAISLAMU. CCM iwaache waislamu watafute uongozi wao huru kabisa, wanaouamini. Kufikiri ATI maoni ya waislamu yataendelea kusimamiwa, kuratibiwa na kuongozwa na JINI BAKWATA ni kupoteza muda na kujidanganya. Mbona hawa wakristu wana taasisi zao muhimu na imara za kidini na wanaziamini..??? Kwa nini serikali mfu ya CCM inaendelea kuwashika waislamu na kuwadhibiti kwa kuitumia taasisi ambayo waislamu hawaiamini..???
Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, pamekuwa na marais wawili ambao ni waumini wa dini ya kiislamu, Mzee Mwinyi na sasa Kikwete, hawa ni waislamu kabisa, ina maana hawajui malalamiko ya waislamu ya miaka nenda rudi..??? Zanzibar maraisi wote toka Mzee Karume Mpaka huyu wa sasa hivi pia wao hawajuwa waislamu na Wazanzibari wanataka nini miaka nenda miaka rudi..??? Kama Kikwete na wenzie walichoshwa na mauaji yaliyokuwa yanaendelea nchini Zanzibar na wakaamua kuwaacha Wazanzibari waamue hatima yao na Leo imeundwa S.U.K. japo kuwa bado hawajawapa haswa wanacho kitaka Wazanzibari ambacho sote tunakijuwa ni kuwa na nchi yao yenye mamlaka kamili.Basi Kina Kikwete haohao wanashindwaje kusema matatizo ya waislamu sasa basi na wakawaachia waislamu huru waamue hatima yao, wawe na vyombo wanavyoviamini visimamie maslahi yao. Mwinyi na sasa Kikwete siyo waislamu nyiaa..??? CCM ina maslahi gani na BAKWATA....???
Mtizamo wangu pia ni kwamba, waislamu wanaweza kuwa wanamalizana wao kwa wao bila kujua.
Pale Marekani kulikuwa na tatizo la msingi kwa wamarekani wengi wa kipato cha chini, huduma za afya zilikuwa kuzungumkuti. Sehemu kubwa ya waathirika wa jambo hili walikuwa wamarekani weusi. Marais wote wazungu waliopita hawakuwahi kufikiri kulitatua, alipopata nafasi Obama akalibainisha Suala la afya kwa wamarekani wa kipato cha chini kama tatizo la msingi linalohitaji utatuzi wa haraka.
Obama akatengeneza muswada wa bima ya afya, akapambana hadi ukawa sheria, Leo wamarekani wa kipato cha chini ambao wengi ni weusi wanafaidika na mpango huo. Obama alipigwa vijembe kuwa analeta muswada wa kuwapendelea watu weusi lakini aliwapuuza wapinzani wake, alijua anafanya jambo ambalo litaondoa mgawanyiko na ukosefu wa haki muhimu ambalo lingeisumbua Marekani ya baadaye.
Hapa kwetu tuna marais wanaonea haya dini zao na wanashindwa kutatua matatizo ya msingi ya kundi ambalo wameliishi na kuonja adha ya kero zao. Kuwaacha waislamu wajichagulie vyombo huru vya kujiongoza ni kuongeza na kupanua wigo wa demokrasia na uhuru muhimu kwa watanganyika wote, hili halitakuwa na faida kwa waislamu peke yao, lina faida kwa nchi nzima. Ni bora rais uitwe mdini kwa kuondoa udhibiti wa chama chako kwa taasisi ya kidini na kuiacha huru kuliko kuacha mifarakano na malalamiko ya kundi linalodhaniwa linaonewa kwa miongo kadhaa yaendelee.
Mimi nadhani waislamu wana matatizo ya msingi kati yao, panahitajika viongozi imara wanaoliona hilo. Ikiwa yataachwa au kushughulikiwa kwa mtindo huu wa kuvizia na kupiga RISASI wale wanaotetea maslahi halisi ya waislamu, hayatakwisha.
Ikiwa atauawa Ponda mmoja eti kwa sababu anadhaniwa kuwa “mtu hatari”, in the next morning watazaliwa Ponda wengine hatari zaidi wapatao 1000. Uhuru wa Dokta hauzimwi kwa RISASI.
Sote bila kujali itikadi zetu za kidini, kisiasa na kimtizamo, TULAANI KWA NGUVU UNYAMA ALIOFANYIWA SHEIKH PONDA.

No comments:

Post a Comment