Tuesday, August 20, 2013

SHEIN ANZISHA WIZARA MPYA WATU WALE BURE NA KUTUINGIZIA WARUGURU WAWILI KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ali Mohamed Shein.
Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kupangua idara zilizokuwa zikisimamiwa na wizara mbalimbali na kuunda wizara mpya nne nchini humo ili kuwa wengine kula ya bure.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee, katika mabadiliko hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kubakia na Wizara 16 kama ilivyokuwa zamani na toka mwaka 1964 mpaka leo Wizara hizo zimeleta faida gani....???
Taarifa hiyo imetaja Wizara mpya za kuwaongezea watu kula ya bure zilizoanzishwa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Shein tawala za mikoa na Idara maalum za SMZ, ambapo Waziri wake atakuwa Haji Omar Kheir, Wizara ya Nchi Ofisi ya Shein Ikulu na Utawala Bora itakayoongozwa na Dk.Mwinyihaji Makame.
Wizara nyingine ni Wizara ya Nchi Ofisi ya Shein Kazi na Utumishi wa Umma itakayoongozwa na Haroun Ali Suleiman na Wizara ya Fedha ambayo itakuwa chini ya Omar Yusuph Mzee.
Katika mabadiliko hayo idara hizo za kuwapa watu kula ya bure wala hazina faida  zilizohamishwa kutoka Wizara moja kwenda nyingine ni idara ya uwezeshaji ambayo imehamishiwa katika Wizara ya Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto ambayo itaongozwa na Waziri Zainab Omar Mohamed. Idara nyingine ni utumishi wa umma na utawala bora na kuhamishiwa katika ofisi ya Shein na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, shughuli za tume ya mipango zimehamishiwa ofisi ya Shein na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi kutoka Wizara ya Fedha na idara ya uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam zimehamishiwa ofisi ya Makamu wa pili wa Rais.
Aidha, Shein amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu wakuu katika Wizara hizo mpya na mabadiliko hayo ameyafanya kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha katiba ya nchi ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Shein amemteua (huyu ni Mtanganyika anapenyezwa umesikia wapi mzanzibari akawa na jina la kwanza la kikiristo kisha la pili la kislamu na la tatu la kiruguru..? Joseph Abdallah Meza) kuwa Katibu Mkuu Wizara ya tawala za mikoa na idara maalum za SMZ na Naibu wake Mwinyiussi A. Hassan na (CDR huyu pia Mtanganyika mwengine wanyarugusu Shein ANAWAJAZA TU KATIKA BARA LA WAWAKILISHI  Julius Nalimy Maziku). Wengine ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Shein Kazi na utumishi wa Umma na Naibu wake Yakuot Hassan Yakuot, Khamis Mussa Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Naibu Katibu Mkuu ni Juma Ameir Hafidh.
Aidha,Shein pia amemteua Asha Ali Abdulla kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, vijana, wanawake na watoto na Naibu wake ni Ali Khamis Juma na Msham Abdulla Khamis.

No comments:

Post a Comment