Monday, August 12, 2013

TAARIFA YA KINAFIKI YA JESHI LA POLISI NCHINI TANGANYIKA KUHUSU SHEIKH MPONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Jamhuri ya Tanganyika.
Wizara ya Mambo ya Ndani.
Jeshi la Polisi Tanganyika.
Dar es Salaam
Agosti 10, 2013
1. Mnamo tarehe 10, Agosti, 2013, majira ya saa 8 mchana, maeneo ya shule ya msingi ya kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro kulifanyika kongamano la Baraza la Eid lililoandaliwa na Umoja wa wahadhiri mkoani Morogoro,
Dakika chache kabla ya kongamano hilo kumalizika alifika Shekhe Ponda issa Ponda alizungumza kwa muda mfupi.
2. Kongamano hilo ambalo lilifungwa majira ya saa 12:05 jioni,
Ambapo watu walianza kutawanyika, baadhi yao wakiwa wamezingira gari dogo alilokuwa amepanda Shekhe Ponda baada ya kutoka katika eneo hilo, askari wa Jeshi la Polisi walilizuia gari hilo kwa mbele kwa nia ya kutaka kumkamata Shekhe Ponda ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi sehemu mbalimbali hapa nchini yenye mlengo wa kusababisha uvunjifu wa amani.
3. Baada ya askari kutaka kumkamata, wafuasi wake walizuia ukamataji huo kwa kuwarushia mawe askari wa Jeshi la Polisi, kufuatia na purukushani hizo askari walipiga risasi hewani kama onyo la kuwatawanya.
4. Katika vurugu hizo, wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha mtuhumiwa, hivi sasa imethibitishwa kuwa Shekhe Ponda yupo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akitibiwa majeraha katika bega la mkono wa kulia linalodaiwa alilipata katika purukushani hizo.
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, akiwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Sheikh mponga akiwa muhimbili na jiraha la Risasi aliyo Pingwa na Polisi Morogoro nchini Tanganyika Pilisi wanadai ni jiraha la purukushani duuuuuuuuuuh!!
5. Kufuatia tukio hilo timu inayoshirikisha wajumbe toka jukwaa la haki jinai ikiongozwa na CP Issaya Mngulu imeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
SSP Advera Senso
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanganyika.

No comments:

Post a Comment