Thursday, August 8, 2013

TUSIMTAFUTE MCHAWI WA TINDI KALI BALI NI HAWA HAWA VIONGOZI

  1. Hapa kuna mkono wa hao hao viongozi kujaribu kuanzisha zaidi fitina sasa na kama mtu wa sanaa wakujitolea wa volantia kwa nini asihojiwe serekali ya Tanganyika kushirikiana na serekali ya Zanzibar ni wahalifu na wavunjifu wa haki za binaadamu wa kubwa tena sana na wao ndio mafia.
    Sababu kuna kesi chungu mzimaza ambazo zimetokea katika kipindi kifupi haya ambayo ya kihalifu na kuto kuheshimu haki za watu imeanza kwa sheikh faridi kutekwa nyara polisi wakasema watachunguza mwisho wamemshika yeye na kumuweka jela walio mteka wako nje aliyetekwa yuko jela umesikia wapi duniani..?
    Ikaja kwa sheikh suraga tukambia tena polisi inafuatilia na itahakikisha anawakamata walio fanya mambo haya ya kumwangia tindi kali sheikh wapi hakuna lolote mpaka kimya kimya kama hakuna moja lililo tokea.
    Ikaja kwa murshi yalio fuatia nyote munayajuwa hakuna zaidi kubambikiwa kesi watu wasio na makosa alimuradi serekali hizi mbili za Tanganyika na Zanzibar ni mamafia watupu kisha kudanganya watu kuwa polisi wanafuatilia kisha jiiiii hakuna lolote.
    Sheha wa tomondokamwangiwa tindi kali mpaka leo walio mwangia hawajashikwa hivi kweli matokeo yote haya polisi hawaja mshika hata mtu moja na wakimshika basi ni kesi ya kubambikiwa hivi hawa polisi haswa wanafanya nini..? ndio tunasema hawa wanao fanya haya mambo sio majambazi wa wizi wala watu wa siasa bali na hao hao serekali na watu wao polisi na ndio wanao fanya haya ndio maana hawawakamati.
    Na sasa imekuja kwa raiya wawili wa uwingereza pia inasikitisha kuona kuwa rai wa uengereza anathaminiwa zaidi ya wazanzibari maana yalio tokea yote watu kimya viongozi kimya leo wamemwangia watoto wa kigereza viongozi wanabweka kama majibwa koko
    Kwa upande wa nchi ya  Tanganyika
    Imekuja kwa kibanda mbona mpaka leo hatujasikia mtu yoyote kukamatwa..?
    Ikaja kwa ulimboka kimyaaa mpaka leo nani kashikwa au kupelekwa mahakamani..?
    Imekuja kwa mabomu ya arusha na kupiga watu risasi polisi wanasema hawajapiga risasi wakati mpaka mtoto kamasema kweli kuwa amepingwa risasi na polisi nani kafikishwa mahakamani..? sasa nini uchunguzi wa matukio haya na hatma ya uchunguzi...? kila kesi kapuni.
    Mimi kwa maoni yangu binafsi serekali ya uwengereza iwakamate na kuwatia nguvuni baadhi ya viongozi wa nchi ya Tanganyika na viongozi wa nchi ya Zanzibar kwa makosa ya uhalifu.
    Akamatwe (1)Balozi Seif Ali Iddi, (2) Muhammed  Abood (3) mwinyi haji makame na Vuai Ali Vuai wahojiwe kijeshi jeshi na mateso juu watasema tu ni nani anaye toa mri ya kufanywa mambo kama haya hapa nchini kwetu Zanzibar.
    Tanganyika akamatwe (1) Nchimbi (2) Pinda (3)  Samuel Sitta (4) Nape akamatwe pia na wao wahijiwe kijeshi jeshi na mateso kama wanavyo watesa watu watasema tu ni nani anayefanya na kumrishi haya mambo mabaya.

1 comment:

  1. kuna wakati nawaza anayepost kwenye hii blog ana elimu kiasi gani.. na akili yake iko sawa kweli?

    ReplyDelete