Sunday, August 4, 2013

TUSISAHAU KUMUOMBEA DUWA DADA YETU KIPENZI CHETU DAA SALMA SAID KATIKA MFUNGO HUU WA RAMADHAN NA BAADA YA RAMADHAN PIA

Assalaam Alaykum Muandishi wa Blog hii Dada Salma Said anahitaji Dua zenu kwa wingi ili ayashinde magumu anayopitia katika maradhi yake na matibabu yake.
Assalaam Alaykum
Muandishi wa Blog ya ZANZIBAR YETU haki ya kuwa mzanzibari Dada Salma Said anahitaji Dua zetu kwa wingi ili ayashinde magumu anayopitia katika maradhi yake na matibabu yake.
INSHAA ALLAH
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema, “Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufurie sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu.” (59:10)
Katika hadithi yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “Maombi ya Muislamu kwa nduguye ni yenye kujibiwa, katika kichwa chake kuna malaika aliyewakilishwa kila atakapo muombea ndugu yake kheri anasema malaika yule: Amin, nawe upate kama hivyo (ulivyo muombea ndugu yako).” (Imepokewa na Imam Muslim)

No comments:

Post a Comment