Monday, August 19, 2013

WAMEMUWA MZEE KARUME,WAKAMFUNGA MAALIM SEIF SASA WAMFUKUZA MANSOOR YUSSUF HIMID


MANSOUR, MWANA MKATABA ASIYE YUMBA,WAZANZIBARI BADO TU HAMJAJUWA KAMA CCM SIO CHAMA CHA WAZANZIBARI BALI NI CHAMA CHA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KUITAWALA NCHI YETU YA ZANZIBAR CHAMA CHETU NI ASP NA WAMEKIUWA.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Zanzibar, kimemeguka baada ya Kamati Maalumu kumvua uanachama Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansoor Yussuf Himid, akidaiwa kukiuka atii maadili ya chama hicho. Uamuzi huo umekuja baada ya Mansoor kudaiwa kupingana na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inayoamini katika muundo wa Serikali mbili.
Chanzo cha kuaminika kutoka katika kamati hiyo, kiliiambia  jana kuwa uamuzi wa kumvua uanachama Mansoor uliwasilishwa katika kikao kilichofanyika CCM Kisiwandui chini ya Makamu Mwenyekiti wake ambaye pia ni Ali Mohamed Shein.
Kwa mara ya kwanza, tuhuma za Mansoor zilifikishwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM nchini Zanzibar, kilichoketi Agosti 16, 2013 katika Ofisi za CCM Kisiwandui ambapo wajumbe wa kamati hiyo kwa kauli moja walitoka na azimio la kumfuta uanachama mwakilishi huyo. 
Shein ndiye aliyeongoza kikao cha Kamati ya Maadili, huku wajumbe wakiwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mohamed Hija, Mbaruk Rashid Omari na balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika, Balozi Seif Ali Idd.
Chanzo hicho kutoka ndani ya CCM nchini Zanzibar, kilisema tuhuma za Mansoor zilizowasilishwa zilikuwa tatu, huku ya kwanza ikiwa ni kushindwa kusimamia malengo, madhumuni na masharti ya chama.
Aidha, Mansoor anadaiwa kutokusimamia wajibu wa mwanachama kwa kukiuka maadili ya kiongozi wa CCM, kwa kukiuka Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa suala la kufukuzwa uanachama kwa mwakilishi huyo lilizua mjadala mzito katika kikao cha jana, lakini baadaye wajumbe walikubaliana kwa kauli moja kufukuzwa kwake.
Mansoor amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio katika safu ya mbele kutetea muundo wa Muungano utakaoipa nchi ya Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa suala la mwakilishi huyo kutakiwa kuwasilisha utetezi dhidi ya tuhuma zake, lilianzia katika kikao cha CCM Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo alisema kama kufungwa afungwe lakini atasimamia Muungano wa mkataba pamoja na mamlaka kamili.
“Katika kikao cha mkoa alitoa utetezi wake na kusema kama kufungwa afungwe, kama kunyongwa anyongwe na kama kufukuzwa afukuzwe, lakini anataka Serikali ya mkataba.
“Wakati anatoa utetezi wake, Mansoor, alikuwa anatumia nakala moja ya gazeti la wiki la Julai 26, mwaka huu na kumtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, kuwa naye anavunja Katiba ya CCM,” kilisema chanzo hicho.
Kutokana na misimamo yake, Mansoor, anaaminika zaidi kwa Wazanzibari hususani wale wanaoamini katika Muungano wa mkataba pamoja na madaraka kamili ya dola ya nchi ya Zanzibar.
Muandishi wetu wa siri alipomtafuta Msemaji wa CCM upande wa nchi ya  Zanzibar, Waride Bakari Jabu, atoe ufafanuzi wa suala hilo, alisema yupo katika kikao.
“Kwa sasa siwezi kusema jambo lolote mwanangu, nafikiri unasikia sauti za wajumbe wakizungumza, nipo katika kikao na siwezi kusema jambo lolote kwa sasa,” alijibu kwa kifupi Waride.
Mwanasiasa huyo ni mtoto wa Mkuu wa Kwanza wa Jeshi la nchi ya Zanzibar baada ya Mapinduzi, Brigedia Jenerali Yussuf Himid.
Amekuwa akisimamia maridhiano ya Wazanzibari na Umoja wa Kitaifa akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano aliyoshiriki kikamilifu kuyaanzisha mwaka 2009.
Pia ni miongoni mwa Wazanzibari walio mstari wa mbele kutetea muundo wa Muungano, utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Mwenyekiti Hassan Nassor Moyo (CCM), Eddie Riyami (CCM), Abubakar Khamis Bakari (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF) na Salim Bimani (CUF).

No comments:

Post a Comment