Friday, September 13, 2013

JK AKITIA SAINI TU JI SWADA LA KATIBA FEKI NDIO ISHA PITA JE JK NA SHEIN NI NINI NIA ZENU KULAZIMISHI HILI JISWADA..???

Rais Jakaya Kikwete Ali Shein
Wakati Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika akisubiriwa asaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 ili kuwa sheria kamili, wasomi, wanasiasa na wanaharakati wamemshauri asifanye hivyo, wakisema itapatikana Katiba Mpya isiyo na tija.

Wananchi hao kutoka nchini Tanganyika na nchini Zanzibar walisema kwa nyakati tofauti kuwa, Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika anatakiwa kutumia busara ya kushauriana na kupata maoni ya watu wa kada mbalimbali ili kujua nini kifanyike, kabla ya kuamua kusaini muswada huo.

Mjadala wa muswada huo uliopitishwa Ijumaa iliyopita na wabunge wengi wakiwa wa CCM chama cha MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA, ulizua tafrani bungeni iliyosababisha Kiongozi wa Upinzani Bungeni huko nchini Tanganyika, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) kutolewa nje na askari. Katika tafrani hiyo iliyozuka huko nchini Tanganyika, baadhi ya wabunge wa upinzani walirushiana makonde na maofisa usalama, huku wabunge wote wa upinzani, isipokuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, wakiususia.

Wapinzani walisema Serikali iliubadili kwa nguvu muswada huo kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau, pia walilalamikia kitendo cha wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge kutokwenda nchini Zanzibar kuchukua maoni ya wananchi wa nchi ya Zanzibar ambayo ndio upande huo wa muungano na nchi ya Tanganyika katika Muungano huu feki.

Wasomi
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanganyika (UDSM), Gaudence Mpangala alisema mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ulikuwa ukienda vizuri… “Lakini umebadilika vibaya, tena katika kipindi muhimu. Kupitishwa kwa muswada na kusubiri saini ya Rais kunaweza kuleta Katiba Mpya, ikawa siyo ile ambayo Watanganyika wanaitarajia.” Alishauri busara itumike kabla ya kusainiwa kuwa sheria kamili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu nchini Zanzibar, Ali Uki alisema hakuna haja ya muswada kukimbiliwa kusainiwa kwani katiba ni mali ya wananchi na kuupitisha ili uwe sheria bila kuyashirikisha makundi mengine, kutaendeleza malalamiko na kurudisha nyuma malengo ya kupatikana kwake. Uki alisema upo wasiwasi kwamba Katiba Mpya itatokana na utashi wa kisiasa badala ya matakwa ya wananchi, jambo ambalo alisema linaweza kuathiri malengo ya kuandikwa kwake.

“Utashi wa vyama umeanza kujitokeza, huku chama kimoja kikiwa na uwakilishi mkubwa kwenye Bunge hilo lililokuwepo nchini Tanganyika, chama kimoja kina uwakilishi wa asilimia 72 katika Bunge la Katiba,” alisema Uki.
Alikosoa Kifungu cha 8 na Kifungu kidogo cha 4 na 5 cha muswada huo kwamba vina kasoro kwa kuruhusu wabunge wa Bunge la Katiba kufanya uamuzi kwa wingi wa kura badala ya kutumika utaratibu wa theluthi mbili kutoka nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika.

Profesa mwingine wa UDSM, Chris Peter Maina alisema ikiwa kuna nia njema ya kupata Katiba bora, lazima suala la uwiano wa idadi ya wabunge katika Bunge la Katiba litazamwe upya.
“Rasimu ya pili ikishatolewa na kukabidhiwa kwa Bunge la Katiba, kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo itakuwa imekwisha. Sasa inakuwaje Bunge linajadili Rasimu ya Katiba huku waliyoiandaa hawapo, hiki kitu kinashangaza,” alisema Profesa Maina.

Mhadhiri Mwandamizi wa chuo hicho, Dk Frank Tilly alisema hakuna umuhimu wa kukimbiza muswada kutiwa saini wakati kuna mambo mengi ya msingi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi… “Watanganyika hawajakubaliana kwa pamoja, ili jambo liwe zuri ni lazima pande mbili au zaidi zenye masilahi na kitu husika zikubaliane, sasa hilo halijafanyika tunakimbilia wapi?” alihoji.

No comments:

Post a Comment