Monday, September 9, 2013

NDAAAA!! WARWANDA WALIO OLEWA NA WATANGANYIKA WATABAKI TANGANYIKA NA KUPEWA URAI-WATANGANYIKA KUMBE NI WAZUNGU HAHAHA


Nchini Tanganyika Bukoba. Serikali ya Tanganyika imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanganyika wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
“Hatupendi kuachanisha familia zilizoishi kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo, wanatakiwa kwenda uhamiaji kuhalalishwa na baadaye ikigundulika hana tatizo anaweza kupewa uraia wa nchi ya Tanganyika,”
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria, mhusika atapewa kibali alichokiita ‘Independence Pass’ kitakachomwezesha kuendelea kuishi  nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa lazima zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka kwa hiari ni 11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na 53,000, hivyo idadi kubwa bado wanaishi nchini Tanganyika.
Akizungumzia zoezi la kurudisha wahamiaji haramu lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari wamewakamata  1,851.
Pia, Sirro alisema ng’ombe 1,765, sare za Jeshi la Wananchi Tanganyika (JWT) na bunduki saba vimekamatwa  na kwamba, wahamiaji  wanaokamatwa wanarudishwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia haki za binadamu hapa nchini kwetu Tanganyika.

No comments:

Post a Comment