Friday, September 27, 2013

NLD KUWAPELEKA ICC THE HAGUE MKAPA NA KARUME JE WALIO WAUWA WAZANZIBARI 1964 MAPINDUZI NAO WATAFIKISHWA ICC..???


CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kimesema kina dhamira ya kuwafikisha kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) The Hague, Uholanzi marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Amani Karume.Ili liwe funzo kwa maraisi wengine wote wanao tawala ktk nchi ya Zanzibar na Tanganyika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho mjini magharibi nchini  Zanzibar, marais hao wanadaiwa wakiwa madarakani, kutumia nguvu kubwa za kijeshi na kusababisha vifo vya watoto 60 kisiwani Pemba, mwaka 2001.
Naibu Katibu Mkuu wa NLD nchini Zanzibar, Khamis Haji Mussa alimuambia muandishi wetu wa siri  kwamba utawala wa viongozi hao ulifanya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kutumia helikopta na askari wa ardhini kuwamimiminia risasi wananchi wasio na hatia waliofanya maandamano Januari 26 na 27, 2001 kisiwani Pemba nchini Zanzibar.
Alisema Mkapa, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Karume akiwa Rais wa nchi ya  Zanzibar, walisababisha mauaji ya halaiki. Anashangaa kwanini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria: alihoji
“Waliokufa ni watu akirudia tena waliokufa ni watu mbwana weee…Taasisi za kutetea haki za binadamu zinapaswa kuingilia kati na kuwafikisha mahakamani viongozi hawa na washirika wao,” alisema na kuongeza:
“Lakini pia Karume akiwa madarakani…alitumia vibaya madaraka yake kwa kuhodhi ardhi kubwa ya wananchi akitegemea kulindwa na Katiba mbovu isemayo Rais hatoshtakiwa akiwa madarakani na hata baada ya kuondoka madarakani,” alisema Mussa.
Alishangaa ni kwa nini Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata na Makamu wake, William Ruto walifikishwa ICC kwa madai ya kusababisha mauaji ya watu mwaka 2008 wakati Mkapa na Karume wakifumbiwa macho...???
Alipokumbushwa kwamba wakati wa mauaji hayo yakitokea Mkapa alikuwa nje ya nchi na aliyemwachia madaraka alikuwa ni Makamu wa Rais, hayati Dk Omar Ali Juma. Alijibu kwa mkato: “Kila kitu kitajulikana mahakamani,”.
Alisema miaka mingi baadaye, Karume aliamua kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na kumrubuni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) isiyo na tija kwa Zanzibar na Wazanzibari wanyewe:
“Alimrubuni kwa ghilba Maalim Seif ili tu kukwepa mashtaka…Karume akiwa madarakani alijiwekea chini yake Wizara ya Fedha kwa miaka 10 na kumuahidi Maalim kuwa angemsaidia kupata urais wa Zanzibar,” alisema na kuendelea:
“Miezi sita kabla ya kukutana Ikulu mwaka Novemba 2009…Maalim katika mkutano wa hadhara pale Kibandamaiti alisema. (Mussa anamnukuu Maalim Seif):
‘Karume na familia yake wanafanya ufisadi wa kupora mali…ardhi na fukwe za bahari huku watoto wake wakipata zabuni kinyume na utaratibu’:
“Leo inashangaza eti anasema Karume ni shujaa na Profesa wa siasa!,” alisema na kudai: “Hadi leo nnayo kanda ya video ya mkutano huo,” alisema Mussa.
Alidai pia kuwa Karume aliyatumia madaraka yake na kuipinda kama si kuivunja Katiba ya nchi yetu ya  Zanzibar ya mwaka 1984 na ile ya CCM kwa kuleta SUK kumlinda, dhidi ya mauaji yaliyotokea Pemba nchini Zanzibar.
Muandishi wetu  alipotaka kujua kama ana ushahidi wa madai hayo, alisema Mussa: “Nimejiandaa vya kutosha kuihakikishia ICC kuhusu hayo yote pamoja na ndugu na jamaa wa waliopoteza familia zao na sasa wanadai fidia,”.
Maandamano ya wafuasi wa CUF kupinga ushindi wa CCM nchini  Zanzibar, Januari 26 na 27 yalikumbana na rungu la dola na kusababisha mtafaruku mkubwa hadi watu kadhaa kwenda ukimbizini, Shimoni Mombasa  nchini Kenya.
Ingawa NLD inawasakama Mkapa na Karume, wadadisi wa masuala ya siasa walidai kuwa walioitisha maandamano yale, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu, Maalim Seif nao wanapaswa kuwajibika pia huko huko ICC:
“Lipumba na Seif wala hawakwenda kuyaongoza maandamano…Seif alikwenda ughaibuni eti kuwaomba wahisani waache kuisaidia nchi ya  Zanzibar wakati Lipumba alijificha Buguruni (Makao Makuu ya CUF) wakati wafuasi wao wakipambana na nguvu za dola na kupingwa na kutwangwa risasi,” alisema mwanachama mmoja wa CUF akitaka na viongozi hao pia wapelekwe  ICC ‘The Hague’.
Hata hivyo, mwanasheria mmoja mkongwe aliyewahi kuwa mwanachama mwandamizi wa CUF aliliambia Muandishi wetu kuwa hakuna uwezekano wowote wa Mkapa na Karume kupelekwa ICC The Hague:
“Ni uzushi tu na kutaka kufahamika kwa NLD…Huyo kiongozi angepaswa kwanza kufahamu Mkataba wa Roma (Rome Statute) uliounda ICC unasemaje?,” alihoji mwanasheria huyo.
Alisema Mkataba wa Roma, ulianza kisheria Aprili 11, 2002 pale idadi ya nchi wanachama ilipofika 60 na ICC ikaanza utekelezaji rasmi Julai 1, mwaka huo huo:
Anafafanua: “Kwa mujibu wa Mkataba…ICC ina uwezo wa kuchunguza na kupeleka mahakamani matukio ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yaliyofanywa baada ya Julai 1, 2002.
“Maandamano na mauaji ya Pemba yalifanyika mwaka 2001 kwa hiyo ICC haina mamlaka ya kusikiliza wala kupokea malalamiko kama hayo,” alisema Mwanasheria huyo.....Muandishi wetu alipo muliza kwani hakuna viongozi wa nchi nyengine walio fanya mauwaji kabla ya mwaka huo na wamefikishwa mahakamni kama kosovo,bosnia na wengine alibaki ah ah ah mmmmm na kutoweka.

No comments:

Post a Comment