Saturday, September 14, 2013

SHEIN AMTEMBELEA PADRI ALIYE MWANGIWA TINDI KALI MNAZI MMOJA HOSPITAL SHEIN AZZAN JE UTAMTEMBELEA...???

Padri Joseph Magamba amemwagiwa acid maeneo ya Sunshine Internet Cafe hapo Mlandege, mjini Zanzibar.
Padri Joseph Magamba baada ya kumemwagiwa tindikali maeneo ya Sunshine Internet Cafe  Mlandege, nchini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika
Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni nchini Zanzibar, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao nchini Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kumwagiwa Tindikali jana na watu wasiojulikawa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja nchini Zanzibar, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kupatiwa matibabu. ambayo pia ndio hospitali hii hii ambayo amalazwa Sheikh Azzan na Shein hakuja kumtembelea na bado yuko humu hospitali M/Mungu anatuonyesha vipi huyu Shein na unafiki wake Wazanzibari funguweni macho kikulocho....

Mmoja wa Ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba na,Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein, akimueleza Shein hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni Unguja nchini Zanzibar je huyu Shein ashawahi kuwafariji wake na watoto na dungu na jamaa wa Masheikh walio fungwa jela wa UAMSHO au wake na watoto na jamaa wa Sheikh Nassor Bachu alifariki....???

Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa na wafuasi wa Padri Joseph Monesmo Magamba,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana jana jioni nchini Zanzibar.

Vijana wa Umoja wa Kitaifa (VUK) kupitia Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo ndugu Salum Abdallah Salum, wametoa tamko lao kama linavyosomeka hapa chini.
Kwa mara nyengine tena tukio la kinyama na la aibu limetokea kwa matumizi ya tindi kali dhidi ya binaadamu ambapo leo hii Kiongozi wa Kidini akiwa ni Padri Joseph Magamba, alieshambuliwa akiwa maeneo ya Mlandege, Nchini Zanzibar.
Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar (VUK) lina laani tukio hilo kwa nguvu zote na hakuna sababu yoyote ile ya kutumia tindi kali kama silaha dhidi ya binaadamu.
VUK inasikitishwa na matendo kama haya ambayo yanazidi kujenga uadui baina ya Wazanzibari ambapo huu ni wakati wa Wazanzibari kuwa pamoja zaidi na wazuie vishawishi vyovyote vya kuwagawa.
Kama ambavyo inalaani matumizi kwa binadaamu yoyote pia inalaani matumizi ya tindi kali dhidi ya viongozi wa kidini na inasimama kuwa hakuna sababu yoyote ile ya kufanya hivyo ama kwa njia ya kisasi, mgogoro kwa sababu njia za amani hazijafungwa na kwa hakika zimezoeleka kutumika na Wazanzibari.
VUK inawataka wananchi kushikamana, lakini hasa vijana wasikubali kuingizwa katika matukio kama hayo lakini pia wasishabikie na zaidi wasiwafiche waovu kama hawa kwa kuwatolea ripoti kwa mamlaka za ulinzi na usalama.
VUK inawataka wananchi kujua matukio kama haya sio tu ya hatari, lakini pia wanachafua jina na amani ya nchi na kwa hivyo wakati huu ndio muwafaka kwa kila mwananchi kuwa macho na kuwa mlinzi wa watu ambao wanataka kuiharibia sifa na jina jina la nchi yetu ya Zanzibar.
VUK inalitaka Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa itoe majibu ya matukio kama haya ambayo sasa yanachafua akhlaki na utengamano wa Wazanzibari, na majibu hayo tunayataka leo kabla ya kesho maana kuanzia kesi ya Sheikh Fadhil Soraga, Sheha wa Tomondo na pia vijana wawili wa Kiingereza ambao ni Katie Gee (18) na Kirstie Trup (18).
VUK inavitaka vyombo hivyo virudishe imani ya Wazanzibari ambao wamezoea jamii inayoishi kwa kupendana na kusaidiana na ambapo sasa inafisidika kwa kuchukina na unyama.
Pia VUK inatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutumia kila aina ya uwezo iliyonayo, na kwa umma kuona uwezo huo unatumika, kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Vilevile SMZ ihakikishe inadhibiti upatikanaji na usambazaji wa tindi kali, ambayo hivi sasa inaonekana kupatikana kwake ni rahisi na matumizi yake ni hatari kwa umma.
Kila mtu ajue na aone kuwa anaweza kuwa hatarini kushambuliwa kwa silaha hii na hivyo wajibu wa kuchukia na kuchukua hatua ni wa kila mtu lakini hasa vijana ambao wao huwapo mitaani saa zote.
VUK ina mpa pole Padri Joseph Magamba na inamuombea Mungu ampe afueni ya haraka na tunaungana na jamaa na waumini wake katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment