Monday, October 21, 2013

NCHI YA TANGANYIKA YAEKWA UBAO KATIKA EAC NCHI YA ZANZIBAR TUMEKUWA MABUBU


Nadhani wenzangu nyote mnafuatilia mwenendo wa Tanganyika na mahusiano yake na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa kwa kitambo sasa Tanganyika inaenguliwa au inapingwa changa katika vikao muhimu sana vya maamuzi ya EAC. Nchi kama Uganda, Rwanda na Kenya ndio zinashika usukani wa kuiengua Tanganyika katika mazungumzo  wenyewe maarufu wanajiita ‘coalition of the willing’. Burundi imekaa kando kidogo, ingawa imo humo humo. Tanganyika ndio ‘out’ kabisa.
Wakati kikao hichi muhimu kinapofanyika, Tanganyika na Rais wa Tanganyika wao walikwenda Iringa kuanzimisha mbio za Mwenge wa uhuru, sasa upumbavu kama huo unaingizwa kwenye mambo muhimu ya nchi na ‘national interests’ hizo anazosema Kikwete. Iwe mbio za mwenge ni muhimu kuliko EAC na masuala yake yote ya nchi..??
Juzi kimefanyika kikao chengine muhimu zaidi kinachojadili ‘political federation’ ya EAC. Hii haikuwa tena ‘Federation of the willing’ imeitwa ‘coalition of federation’ maana na Burundi pia ameingia tele na kupewa maamuzi na kufanya action plan towards, EAC political federation. Tanganyika na Zanzibar hazimo na Tanganyika imetolewa kabisa hapo.
Tanganyika imejitoa na kutolewa kutokana na ubabe wake; kama walivyo zowea kuwaoniya Wazanzibari walifikiri Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi watakuwa kama Zanzibar kumbe wamekosea.jambo la  zaidi ni switilfahamu baina ya Kikwete Raisi wa nchi ya Tanganyika na Kagame Raisi wa nchi ya Rwanda, hapo sasa imetufanya sote tufuate ‘bwana anavyotaka’ au ni seme MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA (national interests hizo!).
Lakini sasa swali la kujiuliza, je kama NCHI YA Zanzibar tuna ‘Zanzibar interest’ ndani ya Jumuiya hii, lakini ‘mabwana hawataki’ au niseme tena MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ndio na sisi tukose moja kwa moja. Kwa mfano, sisi nchi ya Zanzibar kama kisiwa tuna ‘interest’ za kibiashara tokea asili sisi na nchi hizo, kuanzia mifumo ya kodi, ufanyaji biashara n.k — sisi nchi ya Zanzibar kwa ninavyojua mimi ndio hasa waasisi na vinara wakuu wa EAC, na tulikuwa mbele katika east african common currency/board.
Leo just kwa sababu Bernard Member hataki, na Kikwete hawataki WAKOLONI HAWA WEUSI WA TANGANYIKA kutokana na ugomvi wao binafsi na Kagame — basi wameona bora litote na tugawane mbao, na nchi ya  Zanzibar ni nani (they are just nothing). Huu ndio msimamo wa nchi ya Tanganyika MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA, na hizi ndio faida za Muungano feki kwa Wazanzibari kunganishwa kwa lazima na hili JIKOLONI  huu tulionao; kuwa kama jambo hawalitaki Tanganyika MKOLONI MWEUSI, basi sooote iwe hatufaidiki nalo hata kwetu nchini Zanzibar ni faida na lina tija kwetu.
Kwa ufupi, naomba mfuatilie vikao hivi vya EAC na maamuzi yake.
Pia naliomba Baraza la Wawakilishi (BLW) linalokaa sasa hivi, wafikiri ‘strategic’ walizungumze hili na kama serikali, SMZ hiyo ya Mapinduzi Daima walitolee maamuzi, na wananchi tujue: Nini msimamo, mustakabali wa nchi ya Zanzibar ndani ya jumuiya hii ya EAC.
Jamani hili ni suala muhimu sana. Mtu kama Uhuru Kenyatta, au Odinga wanajua sisi kuwa ndio EAC na wanapenda kuwa na sisi kwa hilo, lakini tumezidiwa, tumefunikwa na MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA — na ukweli hasa wanatutetea wao yanapozungumzwa mambo muhimu yanayohusu Zanzibar, kama bahari kuu wakati — MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA  inatuamisha au wanataka kula ‘keki’ yote. Mifano ipo tena mingi tu, mkiitaka sana nitawisilisha (pengine si lazima). Ina maana sisi tunatolewa tonge mdomoni hivi hivi...?? mpaka lini Wazanzibari tutaburuzwa na JIKOLONI HILI TANGANYIKA....???
Kimsingi wao Tanganyika walipofanyiwa survey, imeonekana kuwa 85%ya Watanganyika hawako tayari kujiunga na EAC; lakini ni wao Watanganyika, sio sisi Wazanzibari -sisi hata hiyo survey haikufanyika hapa nchini kwetu Zanzibar.
Hili linaniuma sana maana kwa nia moja au nyengine nimehusika katika ushiriki wa kuifufua EAC miaka ya 1998; na tukaweka msimamo wetu wa SMZ humo.Leo Bernard Membe anatuletea mambo ya ‘yasiyokuwa na maana’ — mambo ya kipuuzi; misaada ya Oman anaizuia na kuweka kauzibe, misaada ya climate change anaizuia na kututilia guu, misaada mengine na mengine anaizuia huu ni uthibitisho tosha kuwa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA kapagawa kwa kujuwa kuwa duuuuh nchi ya Zanzibar ITAENDELEA MAHASIDI WAKUBWA, wao ndio nani, ufalme huu mpaka lini...?? CCM Zanzibar wamekaa tu kama viwete midomo kimya si walelivyo spika anajengewa nyumba ya 1.2 BILLIONI labda na wengine washambiwa zamu yako itakuja basi imepumba, wanatokwa na madenda — hawawezi kufikiri hata chembe, hao CUF nao kadhalika– wanapiga kelele kelele tu; not strategic. Hawazungumzii ‘national issues, au issues of interests’ wanasukuma sukuma tu mawazo kama kuendesha rikwama hapa darajani.
Wazanzibari tuamke jamani — hivi tutakaa hivi mpaka lini — hatuwezi kudai hata chembe ya haki zetu za msingi...???

No comments:

Post a Comment