Wednesday, November 13, 2013

SHEIN KAMA WEWE SIO MNAFIKI NI NINI...???


SHEIN WEWE KAMA SIO MNAFIKI NI NINI....????

Shein alisema kila mwananchi ana haki kikatiba(UAMSHO SIO WANANCHI WAO HAWANA HAKI YA KIKATIBA..?) kufanya jambo analolitaka ukiwamo uhuru wa  kutoa maoni:(MBONA UAMSHO WALIVYO TOWA MAONI YAO UMEWESWEKA JELA IKIWA NI UHURU KUTOWA MAONI..? )
“Kama Makamu wa Kwanza wa Rais anayo maoni yake kuhusu  muundo wa Muungano ni maoni yake au ya chama chake (UAMSHO PIA YALIKUWA MAONI YAO MBONA UME WASWEKA JELA..?)…Lakini siyo msimamo wa  serikali…Isitoshe msemaji wa serikali ni mimi labda atoe msimamo wa serikali  kwa maelekezo yangu,”.SHEIN WEWE SIO MSEMAJI WA SEREKALI WEWE NI MSIMAJI WA DODOMA ASIYEJUWA NI NANI KATIKA ZANZIBAR HII UMELALA BADO HII NI 2013.

Shein amemtetea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Maalim Seif Sharif Hamad kwamba hajakiuka utaratibu wa kuendesha serikali ya  umoja wa kitaifa kwa kutoa kauli za kutaka kuwepo mfumo wa Muungano wa serikali tatu na Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili.
Akizungumza Ikulu mjini Zanzibar jana, Shein  aliwaambia wandishi wa habari kwamba Maalim Seif hajawahi kutoa kauli ambazo zinahusu msimamo wa serikali  kwa mambo mbalimbali na kwamba kama ametoa kauli ni maoni yake binafsi  ama ya chama chake.
Shein alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali kwamba  inakuwaje Maalim Seif anatoa kauli tofauti na msimamo wa serikali hususan mfumo  wa Muungano kwa kusema kwamba uwe wa mkataba.
Shein alisema kila mwananchi ana haki kikatiba kufanya jambo analolitaka ukiwamo uhuru wa  kutoa maoni:
“Kama Makamu wa Kwanza wa Rais anayo maoni yake kuhusu  muundo wa Muungano ni maoni yake au ya chama chake…Lakini siyo msimamo wa  serikali…Isitoshe msemaji wa serikali ni mimi labda atoe msimamo wa serikali  kwa maelekezo yangu,”.
Aliongeza:  “Waziri yeyote wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawezi kuisemea serikali juu ya Katiba…Mimi sijamsikia Maalim Seif anazungumza hivyo kwa niaba ya serikali,” alisema  Shein.
Hata hivyo,  Shein alisema mawaziri wote wanaounda serikali hiyo wanafanya kazi kwa  ushirikiano mkubwa na kwamba hawajawahi kuvutana:
“Tunajadili maslahi ya  watu wetu…ukija katika vikao vya Baraza la Mawaziri huwezi kujua nani anatoka  chama gani…La msingi ni kuvumiiana na kila mmoja kufuata Katiba,” alisema  Shein.
Pia Shein alisema amefanikiwa kuiongoza serikaliya umoja wa kitaifa kwa  mafanikio, ingawa alisema kuna wanachama wa CCM ambao wakati inaundwa walimuuliza  kama ataweza kuiongoza.
Alipoulizwa kuhusu kutofautiana kwa kauli kati  Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi kuhusu mchakato wa Katiba mpya baada ya Waziri Bakari kusema kuwa nchi ya Zanzibar haikushirikishwa na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Balozi Iddi kusema kuwa ilishirikishwa,  Shein hakuwa  tayari kujibu hilo na alisema: “Suala hilo limemalizika,”.
Shein  aliwashukuru Maalim Seif na Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika Balozi Iddi kwa jitihada na kazi zao kubwa  walizofanya katika kipindi cha miaka mitatu kwa kumsaidia kuiongoza nchi ya Zanzibar: “Umahiri wao na uadilifu wao umesaidia sana katika kuwatumikia wananchi,” alisema Shein.

SHEIKH FARID,SHEIKH AZZAN,SHEIKH MUSSELEM,SHEIKH MUSSA NA WENZAO WACHIWE BASI MAANA WAO PIA NI WANANCHI NA WANAHAKI KIKATIBA WACHIWE BASI. WACHIWEEE WAPUMUWEEE

No comments:

Post a Comment