Saturday, November 23, 2013

SOTE WAZANZIBARI TUNAITAKIA TIMU YA NCHI YETU YA ZANZIBAR HEROES KILA LA KHERI


TIMU YA TAIFA YA NCHI YA ZANZIBAR HEROES WAKISHANGILIA BAO WALILO FUNGA

Nchi ya Tanganyika na Nchi ya  Zanzibar zimetangaza vikosi vya timu za Taifa zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji mwaka huu.
Michuano ya Kombe la Chalenji inayoshirikisha mataifa ya nchi za Afrika Mashariki na Kati imepangwa kufanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12.
Timu hizo ambayo ya nchi ya Tanganyika ikiwa chini ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Timu ya nchi ya Zanzibar ikiwa chini ya Kocha wake, Salum Bausi ziko kambini zikijinoa kwa mashindano hayo.
 Zanzibar Heroes ya nchi ya Zanzibar na Kilimanjaro Stars ya Tanganyika  zimepangwa katika makundi tofauti katika michuano hiyo ambayo timu hizo zina uzoefu mkubwa.
Ikiwa  Zanzibar Heroes ni muanzilishi wa michuano hiyo ni matumaini yetu Wazanzibari  Zanzibar Heroes itatuwakilisha vyema na kurudi na kombe nyumbani nchini Zanzibar.
Litakuwa jambo la furaha iwapo kwa mara ya kwanza zote zitafanikiwa kucheza mchezo wa fainali kwani zitawahakikishia Watanganyika na kwa Zanzibar pia kisha katika mchezo wa fainali tuwapige bao Watanganyika na kombe litakuja nchini Zanzibar itakuwa furaha ya aina yake.
Zote mbili zina historia ya kutwaa kombe hilo kwa hiyo hakuna kitu cha ajabu kwa safari hii kurudia na kuiwezesha Zanzibar kuwa na heshima katika ukanda huu au Tanganyika kuwa na heshima katika ukanda huu.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mashindano hayo kuanza Kenya ni wakati mwuafaka kwa Shirikisho la Soka la Tanganyika (TFF) na Chama cha Soka cha nchi ya Zanzibar (ZFA) kuhakikisha kwamba wanaziandaa vizuri timu hizo.
Vilevile ni muhimu kwa wadau mbalimbali wa mpira wa miguu nchini kuzisaidia timu hizo ili zisiwe na matatizo yoyote wakati zinakabiliwa na mechi ngumu za mashindano hayo.
Makocha Poulsen na Bausi nao wana kazi ya ziada ya kuhakikisha kwamba wanazinoa timu hizo na kuzipa makali ya kuweza kuhimili kishindo cha mashindano hayo makubwa kwa Afrika Mashariki na Kati.
Lakini, kazi kubwa zaidi iko mikononi mwa wachezaji wa timu hizo mbili ambao ndiyo wenye jukumu kubwa uwanjani la kuhakikisha kwamba nchi ya Zanzibar  inang’ara kwenye mashindano hayo na  Tanganyika inang’ara kwenye mashindano hayo pia.
Jambo la kwanza na la muhimu sana ni kwa wachezaji wote kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika kipindi hiki cha maandalizi na katika kipindi cha mashindano hayo. Nidhamu na kusikiliza na kufuata maelekezo ya makocha wao ndizo silaha kubwa zitakazowasaidia wachezaji hao na kuziwezesha timu zao kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Chalenji.
Wachezaji wanapaswa pia kuonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujituma kwa nguvu zao zote katika michezo yote watakayopambana katika mashindano hayo yanayofanyika Kenya.
Iwapo wachezaji watakuwa makini na kucheza kwa bidii kubwa huku wakiweka mbele mapenzi ya nchi zao bila shaka yoyote watarudi nchini Zanzibar wakiwa na furaha kubwa kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Ni vyema wachezaji wa timu zote mbili wakajiweka katika mazingira ya ushindani wakijua kwamba wanakwenda Kenya kupambana na timu zenye uwezo kwa hiyo wajiandae vizuri.
Wakati tunazitakia kila la kheri Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes itakuiwa furaha kubwa kwa Zanzibari au Watanganyika iwapo moja ya timu hizo italileta Kombe la Chalenji katika ardhi moja ya nchi hizi mbili ima nchini Zanzibar au nchini Tanganyika.

No comments:

Post a Comment