Sunday, December 1, 2013

MARAISI WA NCHI ZOTE ZA EAC WASAINI MKATABA WA KUANZA MCHAKATO WA KUWA NA SARAFU MOJA SHEIN WEWE UKO WAPI..???


MIKWARA YA KAGAME,MUSEVENI NA UHURU IMEWAINGIA WATANGANYIKA WENYEWE WAMESAINI SARAFU MOJA SASA WATANGANYIKA MUTABURUZWA KAMA MULIVYO IBURUZA NCHI YETU YA ZANZIBAR MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI AKHERA NI HISABU TU KAKA BLAZAA

Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wamesaini mkataba wa kuanza mchakato wa kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanchama wa jumuiya hiyo Kenya,Tanganyika,Uganda,Rwanda na Burundi... nchi yetu ya Zanzibar inaburuzwa ndani ya tumbo la chatu TANGANYIKA.
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Sherehe za kutia saini mkataba huo zilifanyika jana jumamosi jijini Kampala nchini Uganda ambako viongozi wa Mataifa matano wanachama walikutana JE KISHEIN WEWE SAWAJIDAI NI RAISI MBONA HUKWENDA KAMPALA...??
Marais wa Mataifa ya EAC, Yoweri Mseveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jakaya Kikwete wa Tanganyika, Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkuruzinza wa Burundi walihudhuria kikao cha 15 cha umoja huo ambacho kilichofikia maamuzi hayo jana jumamosi.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa EAC Richard Sezibera alisema hatua hiyo inathibitishauanzishwaji wa matumizi ya sarafu moja mara mchakato wa maandalizi utakapokamilika na hii ni hatua mojawapo ya kuhakikisha nchi za EAC zinafikia azimio la kuwa na shirikisho la kisiasa ambalo ni hatua ya juu kabisa.
Umoja wa sarafu ni miongoni mwa malengo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC, mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imeanza kutekelezwa.
Katika kikao hicho cha Kampala Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alichukua uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Aidha viongozi hao walikubaliana watakuwa wanashauriana mara kwa mara kuhusu maswala muhimu yanayohusu jumuiya nzima ya EAC. Zanzibar bado tume lala fofofoooooooooo

No comments:

Post a Comment