Sunday, December 1, 2013

TIMU YA SOKA YA VIETNAM NA CHINA KOMBE LA MAUWAJI YA WAZANZIBARI



TIMU za soka za Vietnam na China, zimetumiwa mialiko na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya ‘Kombe la Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi’) yatakayofanyika nchini Zanzibar, mwezi huu.
Timu hizo zimealikwa, ili kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi), yanayofikia kilele chake Januari 12, mwaka ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari wiki iliyopita, kutoka Ofisi ya Balozi Mdogo wa Nchi ya Tanganyika hapa nchini Zanzibar, ilieleza kuwa mwaliko huo umetolewa na Balozi Mdogo wa nchi ya Tanganyika, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Sherehe za Kitaifa, Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa nchi nyengine kama Balozi wa nchi ya Vietnam na Jamhuri ya Watu wa China kwa nyakati tofauti.
Balozi Seif alisema Serikali tayari imeshaandika barua kwa nchi hizo na hatua hiyo, imefikiwa kutokana na msimamo wa nchi hizo kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tangu mwaka 1964 baada ya kuwauwa Wazanzibari.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Serikali imejiandaa kuzihudumia timu hizo kwa kutoa huduma za malazi, chakula na usafiri wa ndani wakati zitakapokuwa nchini, huku nchi hizo zikitakiwa kugharamia usafiri wa kwenda Zanzibar na kurudi nchini kwao.
Kwa upande wao mabalozi hao, Nguyen Thanh Nam wa Vietnam na Lu youqing wa China, wakizungumza na Balozi Seif, wameahidi kulishughulikia ipasavyo suala hilo la mualiko, ili kuona kwamba lengo lililokusudiwa la mwaliko huo, linafanikiwa vyema.
Mashindano ya Kombe la Mauwaji ya Wazanzibari (Mapinduzi) mara hii yatakuwa na makundi matatu, mawili yatakuwa yakicheza uwanja wa Amaan, Unguja na kundi moja litacheza uwanja wa Gombani, Pemba ili wazidi kuwakumbusha maumivu ya kuliwa jemaa zao.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza kuwa mbali na timu hizo mbili kutoka China na Vietnam, mashindano hayo yatashirikisha timu ngapi na kutoka wapi.

No comments:

Post a Comment