Friday, January 3, 2014

MOJA KATIKA MASULTANI WEUSI WA TANGANYIKA SITTA NA DOTO ZAKE ZA ALINACHA ZA KUENDELEA KUIFANYA NCHI YA ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA


*Sitta Asema: ‘CCM Iiache Kuwa Kichwa Ngumu Kumpinga Jaji Warioba’
WAKATI Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewasilisha Rasimu ya pili ya Katiba kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta amesema Tanganyika (Tanzania) haiwezi kuongozwa na marais watatu.
Sitta alisema anakubaliana na mawazo ya tume ya Warioba ya kuwa na serikali tatu, lakini hakubali Raisi wa nchi ya Zanzibar na Raisi wa nchi ya Tanganyika nao waitwe maraisi, kama yule wa Muungano.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana nchini Tanganyika, Sitta alisema ili serikali tatu zifanye kazi kwa kuheshimiana, kuwekeana mipaka, Raisi wa Tanganyika na Raisi wa Zanzibar, wapewe majina na hadhi nyingine, ili Tanganyika (Tanzania) iwe na rais mmoja tu wa Muungano.
“Niliposikia maoni na ufafanuzi wa kina jinsi serikali tatu zitakavyokuwa, nimekubaliana na mawazo ya tume kwamba tuwe na serikali tatu. Lakini kwa maoni yangu tuwe na Amiri Jeshi Mkuu mmoja tu ambaye ni Rais wa Muungano, maana hatuwezi kuwa na marais watatu kwenye nchi mmoja,” alisisitiza Sitta.
Waziri huyo mwandamizi wa Serikali ya nchi ya Tanganyika, alitoa mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) kwamba rasimu yake imependekeza kuwa na rais mmoja tu na si marais sita, wanaounda shirikisho hilo.
Pia, alipendekeza jina la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika (Tanzania) libadilishwe na badala yake, liitwe Shirikisho la nchi za Tanganyika (Tanzania.)
Akizungumzia msimamo wa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), kupinga serikali tatu na kutaka muundo wa serikali mbili uendelee, Sitta alisema: “CCM isibaki kuwa kichwa ngumu kupinga serikali tatu,”.
Alisema CCM inakosea kung’ang’ania serikali mbili wakati Katiba ya nchi ya Zanzibar ndiyo iliamua serikali mbili, hivyo serikali ya tatu kwa sasa, haiepukiki.
Akitoa mfano, alisema Katiba ya nchi ya Zanzibar inataka miswaada yote inayopitishwa na Bunge la Jamhuri iridhiwe kwanza na Baraza la Wawakilishi, jambo ambalo alisema si sahihi.
Alisema Katiba ya nchi ya  Zanzibar, imefanya mambo mengi kuihalalisha nchi ya  Zanzibar kuwa nchi kamili na imefanya mambo hayo bila ridhaa ya Tanganyika (Tanzania Bara.)
Alisema ili kubaki na serikali mbili, lazima nchi ya Zanzibar ikubali kuifumua Katiba yake inayotoa mamlaka kamili kwa Raisi wa nchi ya Zanzibar, jambo ambalo alisema ‘Wazanzibari hawawezi kulikubali  ng’oooo:
“Mimi nilipomsikiliza Jaji Warioba safari hii, jinsi alivyojenga hoja ya serikali tatu, nimeona kuna hoja za msingi sana zipo kwa sababu kuna mambo makubwa na ya msingi yameshafanyika,” alisema na kuongeza:
“Huwezi kupitisha Katiba inayosema miswada inayopitishwa bungeni Dodoma nchini Tanganyika isifanye kazi nchini Zanzibar hadi Baraza la Wawakilishi likae na kuridhia, ukishafika hapo, basi serikali tatu haziepukiki,” alisisitiza Sitta.
Sitta alisema tume ya Warioba, imefanya kazi kubwa na nzuri kwani rasimu ya pili imekwenda mbali kuangalia vitu kama zawadi za viongozi, jambo ambalo zamani viongozi waliona ni haki yao kupata zawadi za aina hiyo bila kujali kwamba hiyo ni rushwa.
Kwa mujibu wa Sitta – Kuna mambo ya msingi ya kuendelea kujadili nje na ndani ya CCM, nayo ni namna ya kuiendesha Serikali ya Tanganyika (Muungano), kwani kwa maoni ya tume, serikali hiyo itakuwa ikichangiwa zaidi na Tanganyika, jambo ambalo linaweza kuibua manung’uniko ya upande mmoja wa Tanganyika kuwa kwa nini Tanganyika inachangia zaidi katika serekali ya shirikisho kuliko serekali ya Zanzibar.
Aliwataka Wana CCM na wadau wote wa nchi ya Tanganyika kuifanyia kazi kauli ya Rais wao Kikwete wa nchi ya Tanganyika aliyokaririwa mara kuwa vyama visipojali masilahi ya taifa katika mchakato wa Katiba, – Katiba mpya itakwama na Watanganyika watalazimika kuendelea kutumia katiba ya sasa ambayo ndio katiba ya Tanganyika toka wakati wa baba yao Nyerere yeye kafa na wao wameshindwa kuandika katiba mpya, Wazanzibari Mzee karume kafa lakini Wazanzibari wameandika katiba yao bila ya wasi wasi lakini Watanganyika wanaruka wakitoja hawajuwi walifanyalo maana Nyerere ndio mwenye akili zao na ashakufa.

No comments:

Post a Comment