Saturday, February 15, 2014

NCHI YA ZANZIBAR NI YAWAZANZIBARI SIO YA SERA ZA NYERERE WANAOTAKA SERA ZA NYERERE NENDANI TANGANYIKA SIO HAPA ZANZIBAR


“MUUNGANO huu unatubana mno…..na Muungano ni kama koti tu, likikubana unalivua”. Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa nchi ya Zanzibar ambaye aliwekwa baada ya kufanywa mapinduzi ya haramu ya kuwauwa Wazanzibari. na mwasisi wa Muungano feki ambao mpaka leo unaiangamiza nchi yetu ya Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume aliyoyatamka mwaka 1968, miaka minne kabla ya kifo chake akionyesha kukerwa na kuthiwa na mzigo mzito kwa nchi yake na rai wake wa Zanzibar na Muungano feki huo  wa Tanganyika na Zanzibar.
Kauli hii haikumfurahisha Baba wa Taifa la Tanganyika hata kidogo. [Tanganyika ambayo imeva koti linalo itwa Tanzania], Nyerere, aliyetaka Muungano wake feki ulindwe kwa nguvu zote kijeshi,polisi,mgambo,wanasisa kwa kila hali na mali Muungano ulindwe, tofauti na Karume alipoonekana kuchoshwa na kuelemewa na mzigo mzito wa Muungano feki kutokana na kile alichokiita “kupelekwa puta kwa Muungano feki unaokiuka makubaliano waliyo kubaliana ndio Wazanzibari tukaita ni Muungano feki maana ungalikuwa sio feki basi mtu akikiuka angelishtakiwa lakini hapa hakuna hilo nchi ya Tanganyika anakiuka ikikiuka tena na tena makubaliano na hakuna hatuwa yoyote inayo chukuliwa”.
Tangu mwanzo,Mze Karume alielewa kwamba, alilazimika kuingia Muungano kwa shinikizo na ghiliba. Aliwahi hata kutishia kutohudhuria sherehe za kubadilishana “Hati za Muungano feki” na kutangazwa rasmi kwa Muungano feki huo, mjini Dar es Salaam Aprili 26, 1964.
Na kwa sababu hizo hizo, aliendesha nchi ya Zanzibar atakavyo na kuwa Raisi pika katika Marasi wote walio kuja baada yake kuongoza nchi ya Zanzibar bila ya kuiogopa nchi ya Tanganyika kwa sasa tunaita WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA, Bila ya kujali kuwa nchi ya Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano feki ya Tanganyika  (Tanzania), wakati huo huo Nyerere aliendelea zaidi na zaidi  kuimeza nchi ya Zanzibar kwa kuongeza mambo ya Muungano feki kwa imla, kutoka 11 ya mwanzo walio kubaliana hadi 16 chini kwa chini bila ya Viongozi wa nchi ya Zanzibar kujuwa wala rai mpaka kufikia wakati wa kifo cha Mzee Karume ambaye ndia aliyekuwa Raisi wa nchi ya Zanzibar kwa wakati huo.
Uhasama kati ya Maraisi wa wawili wa nchi ya Zanzibar Mzee Karume na yule wa nchi ya Tanganyika Nyerere ulifikia hali ya kutisha na hatari katika nchi hizi mbili huku wanachi wakisubiri nini kitatokea kwa bahati mbaya kilicho tokea kilikuwa kifo cha Raisi wa nchi ya Zanzibar kupigwa risasi Mzee Karume mpaka anakufa aliku kiasi cha wawili hao bado hawaongei kabisa ana kwa ana kwa zaidi ya mwaka mmoja mwananchi kumbuka nchi mbili hizo ziko katika muungano lakini Viongozi wake hawaongei. Mawasiliano yao yalikuwa kupitia wapambe wao, Bhoke Munanka kwa upande wa Nyerere, na Aboud Jumbe kwa upande wa Mzee Karume. Kisa.....? Mfarakano juu ya Muungano huu feki nukuwa tayari Mzee karume alijuwa kuwa nchi ya Zanzibar inamezwa na nchi ya Tanganyika na mpaka leo hii 2014 tuko pale pale kero za Muungano feki hazishi!!!! Maana sasa Wazanzibari wote washajuwa kuwa nchi yao imemezwa na nch ya Tanganyika isipokuwa tu hao Wahafidhina wawili watatu ndio wao bado Muungano Mzuri kwa kuwa matumbo yao yako poa.
Kuna wakati Nyerere [mwaka 1968], alikuwa karibu kusalimu amri ili Mungano feki huu uvunjike mpaka ikafikia. Kuandika katika gazeti la “The London Observer” la Aprili 20, 1968, alisema kwa kulalama na kulalamika: “Kama umma wa Wazanzibari, bila ya kurubuniwa kwa hoja za nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona Muungano si wa manufaa kwa uhai wao [na kuamua kujitoa], sitawapiga mabomu kuwalazimisha waendelee na Muungano”. Ok kwanza tujiulize kwa nini alalame na ana bunge la nchi la Tanganyika halimtoshi tu kuwa Raisi wa nchi la Tanganyika...? pili Nyerere hakutupiga mabomu lakini waliofuta yeye na mpaka sasa wanatupiga mabomu kila siku kwa nini na sisi tunataka nchi yetu ya Zanzibar hatutaki nchi yao....??
Yote haya yalitokana na kutekeleza Muungano feki wenye muundo tata na feki wa kutaka kuimeza nchi ya Zanzibar. Wakati Karume aliamini aliingia Muungano wenye Shirikisho lenye Serikali ya mkataba ndio maana anakasema Muungano huu miaka kumi tu kisha tuwangaliye kama unafa tutaendelea haufai basi tuvunje ni mkataba sio serekali Mbili wala Tatu kama zinavyo pikwa sasa na nchi ya Tanganyika na Wazanzibari hivi sasa asilimia 60 wanataka Muungano wa mkataba –, Nyerere kwa upande wake, alitaka Muungano feki wenye Serikali mbili – Serikali ya Muungano feki [ambayo pia ndiyo Tanganyika imeva koti la Muungano] na Serikali ya Zanzibar, lengo likiwa kuelekea Serikali moja kwa sababu ya kutaka kuimeza nchi ya Zanzibar na kuipoteza kabisa katika ramani ya Dunia kuwa hakuna nchi iliyo au ambayo iko inayoitwa Zanzibar.
Na hiyo ndiyo sababu ya kuongezwa kwa mambo ya Muungano feki kinyemela kinyemela kila kukicha, kinyume na matakwa ya Mkataba wa Muungano wa Aprili 22, 1964. Niwazi kuwa nchi ya Tanganyika imevuja sheria na mikataba ya Muungano na kufanya wanavyo taka wao.
Siku moja kabla ya Mzee Karume kupingwa risasi na kuuwawa Aprili 7, 1972, aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Salim Rashid, alikwenda kumuaga kwamba alikuwa anajiuzulu kazi serikalini maana alishaona mbali kuwa nchi ya Zanzibar iko siku itakuwa sio nchi tena ni kijiji tu cha pwani ya nchi ya Tanganyika. Mzee Karume alimsihi asifanye hivyo na kumhakikishia kwamba [yeye Mzee Karume] alikuwa anakusudia kuvunja vunja Muungano feki huo siku chache baadaye. Hata hivyo [Mzee Karume] hakubahatika kuifikia siku hiyo kuweza kutekeleza alilokusudia kuvunja vunja Muungano feki wa nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika, kwa sababu alipigwa risasi na kuuwawa kabla hajauvunja na kuwa ndio kifo chakee.
Wachambuzi wa mambo ya siasa za Muungano feki wanaamini kwamba, kama Mzee Karume angeishi mwaka mmoja zaidi ya 1972, Muungano feki huu ungevunjika haraka sana tena sana na kusingelikuwa tena na koti linalo itwaa Tanzania duniani, kwa adha na kwa hali ya kutisha na Wazanzibari kujengewa hofu ya kuto kuhoji Muungano feki au nawa yatawakuta kama yaliyo mkuta Mzee karume. Lakini pamoja na hayo, kupingwa risasa Mzee Karume na kuuwawa na kuwa ndio kifo chake hakikuzika mzimu wa kero za Muungano feki tangu hapo hadi leo, mambo yameendelea vile vile na sasa ndio yamezida haswa maana sasa sio Mzee karume hapendi Muungano feki bali ni nchi ya Zanzibar kwa ujumla  isipokuwa hao Wahafidhina wanao shiba matumbo yao kupitia Muungano feki nasema tena isipokuwa hao Wahafidhina wanao shiba matumbo yao kupitia Muungano feki ndio bado wanaukumbatia na kubusu Muungano feki.
“Tunang’ang’ana kujadili Muungano feki kijuujuu bila kugusa Mkataba wa Muungano feki. Kwa nini hatujadili Mkataba wa Muungano feki .....? Hii ndiyo hati pekee inayohalalisha Muungano huu feki na ni msingi na chimbuko kuu la Katiba. Kwa nini tumefanya kujadili Mkataba wa Muungano feki kuwa dhambi....? mnaficha nini au mnaogopa nini.....?
Migogoro, mikanganyiko na mitafaruku yote juu ya Muungano feki inatokana na kukataa kujadili Mkataba huo ambao ndio “Cheti cha kuzaliwa cha Muungano feki”. Ni maneno ya Rais wa awamu ya pili Zanzibar, Aboud Jumbe akihoji Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu [NEC] ya CCM iliyomwita kumhoji na hatimaye kumvua nyadhifa zote za uongozi kwa kuhoji muundo wa Muungano huu feki, Giningi Dodoma, Januari 24 – 30, 1964: Soma Mhtasari wa Kikao hicho, ukurasa 116 – 117].
Mzee Jumbe, kama Mzee Karume, alikuwa ameanza kubaini jinsi utekelezaji wa Muungano feki ulivyopelekwa puta bila kuzingatia Mkataba wa Muungano feki kwa mtizamo wa Muundo wa Serikali mbili kuelekea Serikali moja na kuimeza nchi ya Zanzibar na kuipoteza kabisa katika ramani ya dunia, na kuzua hofu miongoni mwa Wazanzibari kwamba “nchi” yao ilikuwa inamezwa taratibu na Tanganyika au WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA.
Na hiki ndicho kilichomsukuma Mzee Jumbe kutumia haki yake ya kikatiba kutaka kuhoji kwenye Mahakama Maalumu ya Katiba kupata ufafanuzi juu ya Muundo sahihi, ridhaa inayopatikana kwa kila Tanganyika (Mtanzania ni koti tu) chini ya ibara ya 125, 126 na 128 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano feki ikiwa ndio katiba aliyokuwa ya nchi ya Tanganyika na kuwa ndio katiba ya Muungano feki ya 1977.
“Awali ya yote, niweke wazi kuwa, chini ya Mkataba wa Muungano, uhusiano wa kisiasa uliokusudiwa ni wa Shirikisho. Mkataba wa Muungano haukufuta Tanganyika wala Katiba na Sheria za Tanganyika”, alisema Jumbe kwa kutoa changamoto kwa NEC ya CCM ((Wauwaji wa nchi ya Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla)) iliyomwita kumhoji.
Akaendelea, “Ule ukweli kwamba Tanganyika ilikabidhi mambo yake kwenye Muungano, haimaanishi kwamba Tanganyika ilikufa. Huu ulikuwa mpango wa muda tu kusubiri Katiba ya Muungano”,
Kwa hili, bila shaka,Mzee Jumbe alikuwa ananukuu ibara ya 5 ya Mkataba wa Muungano feki na kifungu cha 8 (1) cha Sheria ya Muungano feki, Namba 22 ya 1964, vinavyotamka kuwa; “Kuanzia siku ya Muungano feki na kuendelea, Sheria za nchi ya Tanganyika na Sheria za nchi ya Zanzibar zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi hizo kwa mambo yote yasiyo ya Muungano feki”,”.
Nyerer akacharuka na kupagawa na MARUHANI YAKE YA UTANGANYIKA YAKA MSIMAMA Msomaji ona Nyerere alivyokuwa hasidi wa nchi ya Zanzibar ni lipi mbaya alilosema Mzee Jumbe...?, akasema Nyerere: “Sasa mkanganyiko wa mawazo umezuka sasa. Makamu [Makamu Mwenyekiti wa CCM - Jumbe] anasema kuna Serikali tatu; mimi nasema mbili. Ni suala la Mkataba wa Muungano. Na kesi imeandaliwa kwenda Mahakamani kwa Serikali ya Mapinduzi kuishitaki Serikali ya Muungano kwenye Mahakama [maalumu] ya Katiba. Ukuu wa Chama. Kwa kosa gani Serikali ya Zanzibar iishitaki Serikali ya Muungano...............???  Makamu, jiuzulu sasa hivi nasema jiuzulu sasa hivi”, Mwalimu akamuagiza Mzee Jumbe kikaoni ijiuzulu. hapa tayari Nyerere alishavunja sheria ya katiba maana yeye sio wakumvuwa Mzee Jumbe uraisi kama ni kumvuwa alikuwa amvuwe Umakamu Mwenyekiti wa CCM - Sio Uraisi wa nchi ya Zanzibar ni wananchi ndio wenye uwezo wa kumngowa Mzee Jumbe madarakani ndio tukasema huu sio Muungano huu ni mpago maalumu wa kuimeza nchi ya Zanzibar basi.
Mzee Jumbe akajiuzulu [kwa shuruti....?] nyadhifa zote za Chama na Serikali kwa dhambi ya kuhoji Muundo wa Muungano feki. Na kuanzia hapo akawekwa chini ya Ulinzi nyumbani kwake “Mji mwema” kwa miaka mingi tusio ijuwaa sisi.
Nyerere alikuwa muumini wa Serikali mbili kuelekea moja na kuimeza nchi ya Zanzibar kabisa.
Kama tutakavyoona baadaye, tangu mwanzo, Mwalimu hakuwa muumini wa Serikali tatu wa mkataba, bali wa Muungano feki wa serekali mbili kuelekea moja. Kwake Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyo, ulikuja kama nyota ya jaha au kuokota dhahabu katikati ya jiji la Dar tu.
Kwa nini nikasema hivyo ni kutokana na shinikizo la nchi za Magharibi enzi za vita baridi, zikimtumia Nyerere kama mpambe wao “aimeze” nchi ya Zanzibar ndani ya tumbo kubwa la nchi ya Tanganyika baada ya Shirikisho la Afrika Mashariki kushindwa ili isiangukie mikononi mwa Wakomunisti kama ilivyo kisiwa cha Cuba kufuatia Mapinduzi ya Mauwaji ya Wazanzibari na kumilikiwa na nchi ya Tanganyika Mauwaji hayo yalitokea Januari 12, 1964.ili Wakomunisti wa Kizanzibari wasifanikiwe na kugauza nchi ya Zanzibar kuwa Cuba ya pili. 
Mwanzoni, Nyerere alijidai kuwa mpinzani mkubwa wa Muungano na kujidai kama hataki kuwe na Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, pale wazo hilo lilipowasilishwa kwake na Balozi wa Marekani, Februari 1964; na tena Machi 7, 1964 na Naibu Waziri wa Nchi wa Marekani [Mambo ya Afrika], Jimmy Trimble. Lakini baadaye taratibu, alianza kuona hatari mbele yake kwa Zanzibar ya Kikomunisti [hakupenda Ukomunisti mwanzoni] kuwa mlangoni mwa Tanganyika, huku nchi za Magharibi nazo zikimshinikiza achukue hatua juu ya jambo hilo.
Alianza kutambua udhaifu wa Serikali yake ya Tanganyika na wa nchi zingine za Kiafrika dhidi ya hatari kutoka nje. Si hivyo tu, tangu mwaka 1960 kabla ya uhuru, alihofia sana sana nchi ya Zanzibar Nyerere kuwa karibu na nchi yake ya Tanganyika akatamka wazi wazi akisema: “Kama ningekuwa na uwezo wa kukisukuma au kukingowa kisiwa kile [Zanzibar] hadi katikati ya bahari ya Hindi, ningefanya hivyo. Sitanii akasema kwa sitanii ningelikingowa. Nina hofu [kwamba], huko mbele kitakuja kutuumiza kichwa sana sana Watanganyika”. 
Juhudi zote za Nyerere kuona Shirikisho la Afrika Mashariki [EAF] likiundwa, zilikuwa ni kuhakikisha Zanzibar inamezwa ndani ya Shirikisho hilo ili isionekane, na pale Shirikisho hilo liliposhindwa au kugonga mwamba, akaona njia pekee sasa ya kuondokana na hofu yake [na sasa kwa kupewa nguvu pia na Marekani na Uingereza ambazo nazo zilikuwa na hofu ya Ukomunisti kuenea Afrika Mashariki kupitia nchi ya Zanzibar] ni kuiunganisha nchi ya Zanzibar na Tanganyika katika Muungano feki.
Kuhusu Muundo wa Serikali mbili alioendeleza huku akiwa na plani ya kuwa na serekali moja mwishoni, tofauti na Serikali tatu za Mkataba wa Muungano au Muungano wa mkataba walio kubaliana na Mzee Karume,aliendelea na mfomo wake wa serekali mbili na huku analenga Serikali moja kwa kuongeza taratibu [kinyemela] mambo ya Muungano feki ili hatimaye nchi ya Zanzibar ijikute imenyang’anywa mambo yote kuwa chini ya Serikali ya Muungano feki koti la Tanganyika ambayo ndiyo Tanganyika pia. Ugomvi wa Mzee Karume na baadaye Jumbe juu ya Muungano feki umejikita hapo. Na hivi karibuni,  Shein,na fikra zake za kijuwa amewakemea wote wanaodhani Zanzibar siyo nchi yenye mamlaka kamili waache uzandiki huo je mzandiki ni nani hapa Wazanzibari au yeye Shein asiye soma historia ya nchi ya Zanzibar.....? ikiwa Mzee karume alijuwa kuwa nchi ya Zanzibar imemezwa na anataka irudi na Mzee jumbe pia anajuwa ndio hivyo hivyo kuwa nchi hii imemezwa lazima irudi yeye kibushuti huyu asiye juwa anasimama na kusema nchi hii ina mamla kamili kivipi kuwa na mahakama feki ya kuwafunga masheikh ili wasikombowe nchi ya Zanzibar ndio wewe Shein unaona nchi ina mamlaka kamili.....?
Nyerere aliti amri ya mabwana zake
Marekani na Uingereza wilimfanya Nyerere akubali Muungano feki wa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar kukidhi matakwa ya Mataifa yao. wangine wanasema Nyerere alifanyiwa Vitisho ili akubali kuivamia nchi ya Zanzibar na kuanzisha Muungano feki je ni vipi hivyo vitisho......??  Kwanza, alikuwa bado na kumbukumbu yenye hofu jinsi alivyonusurika kupinduliwa na Jeshi lake mwenyewe ndni ya nchi yake ya Tanganyika wanajeshi wake walichoshwa naye wakataka kumpinduwa kwa hiyo alikuwa bado ana hofu ile, Januari 20, 1964; na jinsi alivyookolewa na Jeshi la Waingereza ambao ndio pia walioshinikiza anzishe Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar kwa hiyo alikuwa anawafurahisha mabwana zake walio mueka madarakani.
Na hata kama angekataa kuungana, Uingereza na Marekani, chini ya mpango wa kivita ulioitwa “Zanzibar Action Plan” [ZAP], zilikuwa tayari kuivamia Zanzibar kijeshi, kama Karume angekataa Muungano feki kama walivyo ivamia wakati wa Mapinduzi ya Wauwaji wa Wazanzibari na kuuwauwa Wazanzibari.
Uhakika ni kwamba, majeshi ya Uingereza, chini ya Kamanda wa Jeshi la Anga – “Royal Air Force” [RAF], Brigedia Jenerali I. S. Stockwell, na Kamanda wa Jeshi la Ardhini nchini Kenya, Brigedia Jenerali I. H. Freeland, yalipewa Amri [Joint Operation Instruction] Namba 2/64 kuvamia, huku yakitarajia upinzani na kipigo kutoka Jeshi la nchi ya Zanzibar [Zanzibar Liberation Army – ZLA LEO HII LIKO WAPI WAMELIUWA] chini ya Uongozi makini wa Kanali Ali Mahfoudh, na pengine kwa msaada kadhaa wa silaha kali kutoka China na Urusi.
Pili, Mwalimu bado alikuwa akikumbuka kwa hofu, kuuawa kwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kongo, Mwanamapinduzi Patrice Emery Lumumba, na Rais Sylivanus Olympio wa Togo, waliouawa kikatili chini ya kile kilichoitwa “mchezo mchafu wa nchi za Magharibi dhidi ya Viongozi wanamapinduzi barani Afrika”.
Kwa hili, Nyerere aliona DAAAAH lazima achukue hatua haraka badala ya kusukumwa na kujiweka rehani kwa ugomvi wa mataifa makubwa ya Magharibi na Mashariki. Na hii ilikuwa Baraka pia kwake kumaliza “hofu” yake juu ya KUUIMALIZA NCHI YA ZANZIBAR HURU NA KUIGEUZA KUWA KOLONI LAKE.
Muungano feki huo, ambao ulibuniwa baada ya kuvunjika kwa mpango wa EAF mjini Nairobi, Aprili 10, 1964, ulikuwa njia pekee ya kumzuia aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa Zanzibar wa wakati huo na Mkomunisti, Abdulrahman Mohamed Babu na mawakala wenzake wa Wachina [Chicoms] na Warusi, asidhibiti na kuhodhi madaraka ya Serikali ya Mapinduzi ya Wauwaji wa Wazanzibari SMZ.
Kuna dhana isiyo kweli kwamba Machi 1964, Nyerere na Mzee Karume walikutana Ikulu Dar es Salaam ambapo Nyerere alipendekeza kwa Mzee Karume juu ya Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar, na eti kwamba Karume alikubali mara moja akisema: “Atii  waandishi wa magazeti; waambie kwamba sisi tuko tayari sasa hivi”.
Dhana hii imepotoshwa. Maneno ya Mwalimu yalikuwa hivi: “Tazama, nimewaeleza wazi wazi Waziri Mkuu [Jomo] Kenyatta na Waziri Mkuu [Milton] Obote kwamba, wao wakiwa tayari kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki, sisi [Tanganyika] tuko tayari. Na sasa nakwambia na wewe [Karume, kama nilivyowaambia Kenyatta na Obote], kwamba Zanzibar mtakapokuwa tayari kuunda Shirikisho [hilo], sisi [Tanganyika] tuko tayari”.
Ukweli ni kwamba, alichomwambia Mzee Karume ni juu ya uundaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki na si Muungano feki wa Tanganyika na Zanzibar. Ingekuwaje hivyo wakati muda huo Nyerere alikuwa akifukuzia Shirikisho la Afrika Mashariki kuliko kitu kingine chochote, hadi juhudi hizo ziliposhindwa Aprili 10, 1964 na ndipo alipo amuwa kuwa maadamu nchi ya Zanzibar haikumezwa katika Shirikisho la Afrika Mashariki basi sasa kilicho baki ni Tanganyika kuimeza nchi ya  Zanzibar katika Muungano feki wa nchi ya Zanzibar na Tanganyika WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA.
Nani anasema Nyerere alitaka Serikali tatu au mkataba..?
Tumesema, Nyerere tangu kale hakuwa muumini wa Muungano FEKI  wenye Serikali tatu wala mkataba alichotaka ni Muungano wa serekali mbili kuielekea moja ila kwa lengo maalumu. Kwenye Mkutano wa nchi huru za Afrika mjini Cairo, Julai 1964, alionyesha wazi wazi kutopendelea Muundo huo aliposema, “Muundo wa Serikali moja [Unitary System of government] haufai kwa Afrika kwa sasa; Muundo bora ni ule wa Shirikisho la Nchi”.tukumbuke hapa ilikuwa ni kuhusu nchi nyingi za afrika kwa hiyo lazima atasema hivi kwa kuwa anajuwa yeye pia hataweza kuchanguliwa kuwa raisi wa bara la afrika kwa wakati huo.
Akitetea hoja hiyo baadaye, aliandika makala ndefu kwenye Gazeti la “Africa Forum” [Vol.1 No. 1] mwaka 1965 akisema: “Mfumo bora ni ule wa Shirikisho lenye Serikali Kuu ya Muungano na Serikali za nchi zinazoungana, kila moja ikiwa na Mamlaka juu ya Mambo yasiyo ya Muungano”. Msimamo wake huo ameurudia pia katika Kitabu chake: “Uhuru na Umoja” [Freedom and Unity] ukurasa 300 – 304.
Na hivyo ndivyo alivyoamini Mzee Karume. Akitoa taarifa kwa Serikali yake kwa simu ya maandishi [telegraph], aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Zanzibar kabla na baadaye kidogo kufuatia Muungano, jasusi la CIA, Frank Carlucci, Aprili 23, 1964 alisema, “Karume ametia sahihi [Aprili 22, 1964] Hati [Mkataba] ya Muungano Mzee Karume akiamini kwamba ameingia Mkataba wa kuunda Shirikisho lenye Serikali tatu”.
Na siku za karibuni kabla ya kifo chake, baada ya kuchoshwa na kero za Muungano zisizoisha, Nyerere alitambua utata wa Muundo wa Serikali mbili alisema muundo huo yafaa ujadiliwe kuondoa utata hata kama yeye alikwishatoa msimamo wake wa Serikali mbili. sasa ikiwa Nyerere mwenyewe aliyeleta Mundo wa serekali mbili anasema inafaa ujadiliwe je hawa visonoko wa CCM Wauwaji wa Wazanzibari wa ni nani wakusema usijadiliwee....?
Ukweli Nyerere alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, kama isingekuwa kwa “mambo fulani fulani” juu yake, asingemvua Jumbe madaraka kwa kuhoji Muundo wa Muungano.
Je, hawa wanaojifaragua, hivi sasa, kwamba kujadili Muundo wa Muungano feki nje ya Serikali mbili na ndani ya serekali mbili kuelekea moja atii itakuwa ni  kumsaliti Nyerere., wanatoa wapi ujasiri huo kuuhadaa umma....? Kama ni kumsaliti Nyerere, tusemeje juu ya hao hao waliohujumu Azimio la Arusha na Ujamaa; waliobinafsisha mali za umma bila kujali ili kuwapa ulaji mawakala wa ubepari.....? Je, si wasaliti, hao hao wanaokigeuza Chama cha Nyerere [CCM] kichaka na kimbilio la mafisadi wasiotaka kujivua gamba.......?
Sio siri tena duniani kwamba Wazanzibari wengi hawapendelei Muungano feki wa Serikali mbili kualekea moja, mbali na wanaotaka uvunjwe. Lakini Wahafidhina wa siasa za makundi, kwa unafiki mkubwa, wanajifanya kutoliona hili.
Ni hao hao waliopinga mchakato wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Zanzibar, wakiwamo Wajumbe wa NEC ya CCM, mpaka Raisi wa wakati huo, Amani Abeid Karume akatishia kuwaumbua.
Uhafidhina huo na unafiki wao wa kutaka kuona migogoro na kero za Muungano feki zikiendelea ndio unaofanya waishi kwa gharama ya amani na umoja wa Kitaifa wa nchi yetu ya Zanzibar.
Sasa, ifike mahali waambiwe wazi wazi, waache demokrasia na mawazo ya wananchi juu ya Muundo wa Muungano wautakao yatawale badala ya ubinafsi wao. Na tunaposhinikiza mambo dhidi ya matakwa ya wengi tunatafuta nini, na nini hatima ya yote haya.....? Wazanzibari asilimia 60% wanataka Muungano wa Mkataba wapewe ili tujenge nchi yetu ya Zanzibar kwa upole na masikilizano sio mutupe kasumba za Nyerere hivi na Nyerere vile Nyerere ni Watanganyika sio Zanzibar kama unataka kufuata ya Nyerere Tanganyika iko nendeni hamjafukuzwa ati nendeni mkaendeleze sera za Nyerere huko Tanganyika.

No comments:

Post a Comment