Monday, February 3, 2014

NCHINI ZANZIBAR RAI WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI WAFARANSA WAMEULIWA NA KUFUKIWA KATIKA KISIMA CHA MAJI


JE PASPOTI ZITARUDISHWA ILI WAJULIKANE WANAOINGIA NCHINI MWETU ZANZIBAR AU NDIO MUUNGANO FEKI UDUMU WANYATURU WANAINGIA WATAKAVYO WAKIUWA WATAKAVYO NA KUIBA WATAKAVYO ATI NCHI HII INA MAMLAKA KAMILI TOKA 1964 YAGUJUUU SEMANI KWELI KUWA NCHI HII IMEFANYWA JAAA LA KILA MACHAFU TOKA MWAKA 1964 HUO NDIO UKWELI WA MAMBO.
Nchini Zanzibar ni Aibu na masikitiko makubwa ya kuliwa wafaransa wawili.  Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji (KZU) na Polisi wa MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA wamefanikiwa kuvunja zege lililokuwa limejengwa kufunika kisima walichotupwa raia wawili wa Ufaransa, baada ya kuuawa na kupata sehemu za miili yao ikiwamo fuvu la kichwa.
Ikielezwa kwamba waliotekeleza unyama huo walilenga kupora nyumba na kiasi kikubwa cha fedha walichokuwa nacho Wazungu hao.
Akizungumza na Mwandishi wetu wa siri jana, Mkurugenzi na Makosa ya Jinai nchini Zanzibar (DCI) Yussuf Illembo, alisema kuwa hadi jana mchana, mifupa miwili ya mapaja, fuvu la kichwa na miwili ya mbavu imepatikana kutoka ndani ya kisima hicho.
Alisema kwamba Kikosi Kazi cha Uokoaji kinaendelea kufanya kazi eneo hilo la Matemwe lililopo Shehia ya Kaskazini, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Kazi bado ni ngumu, tunaendelea kuzamia ndani ya kisima na itakapokamilika tutatoa taarifa. Tuacheni kwanza tufanye kazi hii nzito na ngumu kwa wakati huu,” aliomba DCI Illembo.
Zoezi hilo lilifanyika huku likishuhudiwa na ofisa mmoja wa Ubalozi wa Ufaransa nchini na kuelezwa kuwa marehemu hao walinunua eneo la ardhi na nyumba kwa Sh150 milioni kwa kutumia jina moja la mzawa wa nchi ya Zanzibar, kutokana na sheria kutoruhusu wageni kumiliki ardhi nchini humo Zanzibar.
Watu hao, Francios Chererobert Daniel, aliyekuwa mtumishi mstaafu wa ngazi za juu wa Serikali ya Ufaransa na mkewe Brigette Mary, walipotea tangu Desemba 27 mwaka jana.
Baadaye taarifa za kupotea kwa watu hao zilifikishwa Polisi ndipo msako wa kuwatafuta ulipoanza na baadaye kugundulika kuwa, kuna watu wameuawa na miili yao kutupwa katika kisima cha maji kilichopo ndani ya ua wa nyumba hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya waokoaji na mashuhuda wa tukio hilo, walimuambia  Muandishi wetu kwamba sehemu hizo za mwili zinazosadikiwa kuwa za Wafaransa hao, zimefukuliwa baada ya kazi kubwa ya kuvunja zege kwa kutumia mashine maalumu inayofanywa na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wakazi wa eneo hilo zege ambalo inasadikiwa lilimwangiwa juu ya maiti hizo baada ya kuuliwa.
“Tumefanikiwa kutoa sehemu ya miili, imehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,” alisema mmoja wa mashuhuda ambaye alitaka jina lake lisiandikwe. Alisema kuwa kazi ya kuvunja zege hilo ilikuwa ngumu, walilazimika kuwachukua vijana wengine raia wa kawaida ili kuifanikisha.
Akielezea mazingira waliyokutana nayo chini ya kisima walichotupwa Wafaransa hao baada ya kuuliwa, alisema kuwa baada ya zege kuvunjwa walikuta nguo nyingi zimejazwa chini yake na juu yake kujengwa zege hilo kabla ya kumwagwa saruji isiyochanganywa na kitu ili kufunika kisima kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Hata hivyo, vyanzo vya habari vinaeleza kuwa zoezi hilo lililazimika kusitishwa kutokana na sehemu ya chini ya kisima kupita mkondo wa maji ya bahari, hivyo kulazimika kutafuta mashine ya kuvuta maji nchi imefisidika mpaka hai hata mashine ya kuvutia maji inasikitisha sana alisema mashuhuda moja.
“Kazi hiyo ikiweza kufanyika ndipo tutakapoweza kwenda katika kina kirefu zaidi cha kisima hicho ili kukusanya mifupa. Tukipata idadi ya mifupa na mafuvu yote, tutaweza kujua waliouawa ni wangapi,” kilieleza chanzo kimoja kingine.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa siri ya mauaji hayo ni baadhi ya watu wasio julikana kama ni Wazanzibari au ni Mijitu yakutoka nchi nyengine iliyo jaa humu nchini mwetu Zanzibar kwa faidi ya MUNGANO FEKI na MAPINDUZI DAIMA kutaka kupora nyumba, waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao pamoja na fedha zinazodaiwa walikuwa nazo raia hao wa kigeni wakitaka kununua eneo la kujenga hoteli kwenye ufukwe wa Urowa.
Inelezwa kuwa kabla ya kuingia nchini Zanzibar, Wafaransa hao walifikia Nairobi nchini Kenya ambako walitaka kujenga Hoteli lakini inadaiwa kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo aliwashauri kuja nchini Zanzibar kuishi na kuwekeza maana Zanzibar hakuna cha sheria pesa yako tu basi mambo poa.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya Jeshi la Polisi la MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA zinaeleza kuwa mazingira ya tukio hilo yanaonyesha kuwa kabla ya watu hao kuuwawa, mbwa wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Allan, alipewa chakula chenye sumu na kufa na kwamba sehemu ya mabaki ya chakula hicho yaliliwa na mbwa wa jirani ambaye pia alikufa huu kweli ni uchunguzi hata mtoto wa darasa lapili anaweza kujuwa uchunguzi huu.
Aidha, mifuko mitupu ya saruji inayosadikiwa kutumika katika ujenzi wa zege la kisima hicho, imeokotwa nyuma ya ukuta wa nyumba hiyo waliyokuwa wakiishi Wafaransa hao. 
MZEE ABEID AMANI KARUME OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
JULIUS NYERERE BABA WA WATANGANYIKA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

AFRO FISADI INAENDELEA KUIFISI ZANZIBAR,WAZANZIBARI NA WAGENI OYEEEEEEEEEEEEEEE.
MAPINDUZI DAIMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

MUUNGANO FEKI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
MUKIONA TUNAWAUWA SANA HAMENI  OYEEEEEEEEEEEEEE.
NCHI HII INA MAMLAKA KAMILI TOKA MWAKA 1964 OYEEEEEEEE.

No comments:

Post a Comment