Saturday, May 3, 2014

NCHINI ZANZIBAR ZOME ZOME LASHIKA KASI WANANCHI MSIMAMO HUO HUO MPAKA KIELEWEKE

IMG_6934Kulia ni Muwakilishi wa Koani Mussa Ali Hassan tumbo njaa asiye shiba
Zomea Zomea jana imemkuta Mwakilishi wa Koani. Mussa Ali Hassan hapo katika Soko la Mboga Mboga kwa Mchina Mombasa nchi Zanzibar, kiasi cha kuhumiwa na kupanda Taxi kwa fedheha na Kuliwacha gari lake alilo kwenda nalo hapo Sokoni. Msaliti huyoo…. dalali huyoo…,, msaka tonge huyoo…… mnafiki huyooo…., huyoo …. huyooo .. wewe si ulisema UKAWA Waondoke kabla hujarudi wewe….. Utaondoka wewe Fisadi wa Mafisadii hayo ndio yaliomkuta fisadi Mussa Ali Hassan, na kuhemewa kama vile kuku mgeni mwenye kuhemewa.
Hali hii imewakumba badhi ya Wabunge ,Wawakilishi na Wajumbe wa Tasisi mbali mbali kutoka nchi Zanzibar.
Wananchi wa nchi ya Zanzibar wamechukua msimamo huo wa kuwazomea na kuwatupia maneno ya kua ni wasaliti wa nchi yetu ya Zanzibar wenye kuiuza nchi yetu Zanzibar kwa kusaka Tonge za Matumbo yao wake zao na watoto wao.na kuwawacha rai wengine wa nchi ya Zanzibar wakihaha na maisha.
Mambo hayo yamekua yakitokea sehemu tafauti za Miji ya nchi yetu ya Zanzibar pale wapitapo na huzomewa na kurushiwa maneno hayo, Jana ndio yalimkumba Muwakilishi wa Koan Mussa Ali Hassan Zidi ya wananchi wa nchi yetu ya  Zanzibar wenye hasira na viongozi watapia mlooooooo.

No comments:

Post a Comment