Saturday, June 14, 2014

JESHI LA POLISI NCHINI ZANZIBAR NI LA KUFUNGA MASHEIKH NA WATETEA MAMLA KAMILI SIO KUSHIKA WAHALIFU WANAO WASHAMBULIA WANANCHI KWA NJIA TAFAUTI


kijana moja afa baada ya kurushwa bomu na watu wasio julikana nchini Zanzibar

VYEO KIBAO KATIKA BEGA VYA KULA PESA ZA BURE TU HUKU WANANCHI WANAISHI KWA WASI WASI NDANI YA NCHI YAO BORA HIVI VYEO UKAUZEYE MBATATA ZA OROJO NA ZANZIBAR PIZZA
RPC Mkoa wa Mjini Maghar Mkadam Khamis wakakati akizungumza akizungumza na vyombo vya habari


Jeshi feki la walala hoi na kujuwa peke kushika masheikh lakini wahalifu wa kweli hawawashiki la nchini Zanzibar limesema bado halijabaini mtu yoyote au kundi lolote kuhusika na uripuaji wa Bomu katika eneo la jana mjini magharibi nchini Zanzibar.
Kauli imetolewa na RPC Mkoa wa Mjini Maghar Mkadam Khamis wakati akizungumza na kupitia simu yake ya mkononi na baadhi ya vyombo vya habari.
Amesema katika tukio hilo mtu mmoja amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko huo wa bomu.
Taharuki hio imetokea wakati waumini wa Dini ya kiislamu walipokuwa wanatoka msikitini wa Darajani ambapo kulikuwa na mawaidha baada ya kumalizika kwa sala ya Ishaa.
Akibainisha kutokea kwa tukio hilo RPC huyo ,amesema kwamba watu waliokuwa ndani ya gari ndogo aina ya Vits walirusha bomu hilo na kukimbia kusiko julikana wakati waumini wa Dini ya kiislamu walipokuwa wanatoka msikitini.  ((nchi hii ya Zanzibar ina ukumbwa gani ambao gari ikikimbia huwa haijulikani ilikotokomeya Maghar Mkadam Khamis...???))
Hadi sasa Jeshi la Polisi bado halijabaini iwapo bomu hilo ni lakutengeneza kwa kutumia baruti au ni bomu wenyewe ambalo limetengezwa kwa njia ya kitaalamu. ((ni lini jeshi hili la polisi hapa nchini Zanzibar lilibaini jambo lolote la kishenzi wanalofanyiwa Wazanzibari....???))
Alieleza kuwa aliefariki katika tukio hilo ni Khatibu Mkumbiladuha (26) mkaazi wa Mkoa wa Tanga ambae alikuwa miongoni mwa wahadhir waliofika msikitini hapo.
Aidha RPC Mkadam amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu katika kipindi hichi huku wakiliacha Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo na hatimae kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
RPC Mkada je mume wabaini walio mpiga risasi yule padri..? je mume mbaini aliyempiga risasi yule padri mwengine na kuumuwa...? je mume mbaini yule aliye mpiga mapaga sheikh kule kitope..? je mume mbaini yule aliye mrushia sheikh tindi kali...? je mume mbaini yule aliye mrushia padri tindi kali....? je mume mbaini yule aliye warushi tindi kali wale wasichana wakizungu kutoka uengereza n.k. hamna leno moja kazi kula pesa za bure basi nakujuwa kufunga masheikh jela.
Katika kipindi cha hivi karibuni nchi ya Zanzibar imekuwa akikubwa na matukio mbali mbali ya uchafuzi wa amani ikiwa pamoja na kuwawa kwa sheikh kwa mapanga kitope na baadhi ya matukio mengine kadhaa ya uchafuzi wa amani.
Lakini nashauri uchunguzi huo uanzie kwa akina salmini awadh,asha bakari,lukuvi,jon komba na mussa ali hassan,kwani katika wao na wenzao ni baadhi ya watu ambao wameanza kuonyesha na kutoa kila dalili mbaya na ukilinganisha na matokeo kama haya.mfano
mussa ali hassan alisema katika bunge la katiba kua ukawa watoke zanzibar si hivyo wao watawatoa maana wao ni wapiganaji mahiri sasa kauli kama hizi wazanzibari zinatutia mashaka.

No comments:

Post a Comment