Sunday, August 3, 2014

MARUHANI YA JESHI LA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA YAMVA MANSOR YUSSUF HIMID SASA

mansour
Nchini Zanzibar jeshi la mkoloni mweusi Tanganyika na maruhani yake sasa yamuandama Mansour Yusuf Himid. Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar Mansour Yusuf Himid amekamatwa na Jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika kwa tuhuma atii za kumiliki silaha kinyume na sheria imefahamika nchini humo jana nchini Zanzibar.
Mansour ambaye alivuliwa na kupoteza nafasi ya mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Kiembesamaki kwa kuwa anatetea haki za Wazanzibari, alikamatwa nyumbani kwake huko Chukwani na kufanyiwa upekuzi mkali na askari wa Mkoloni Mweusi Tanganyika  kikosi cha upelelezi wakiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na kutilia watu fitina, Salum Msangi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi hilo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai fitina, Salum Msangi alisema Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kiintelejensia kuwa waziri huyo wa zamani anamiliki silaha kinyume na sheria.(swali tunakuliza wewe Msangi mbona alipokuwa waziri wa CCM hizo silaha alikuwa nazo mbona hamumpekuwa....? je balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika iddi seif je yeye hana hizo silaha mbona hamumpekuwi....? vuai je...? nahonda munataka kutuambia hawa hawana silaha mbona hamuwepekuwi.....?)
Msangi alisema mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Jeshi hilo la Mkoloni Mweusi Tanganyika lilianza kuifanyia kazi na jana ilikuwa siku rasmi ya kwenda kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kufanikiwa kupata silaha aina ya Shortgun yenye namba za usajili 1904136413 aina ya Bore Browning pamoja na risasi 112.
Msangi alisema kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha, hairuhusiwi kumiliki zaidi ya risasi 55 kwa silaha aina ya Shortgun na kueleza kuwa Jeshi hilo linaendelea kumhoji waziri huyo wa zamani.
Vilevile, Msangi aliongeza kuwa silaha nyingine aliyokamatwa nayo ni bastola yenye namba F76172W pamoja na risasi 295 jambo ambalo ni kinyume na sheria ya umiliki wa silaha za moto, ambapo mmiliki anatakiwa kuwa na risasi zisizozidi 25.(tnakuliza tena Msangi ni nani aliye muzia hizo risasi kama sio nyinyi jeshi la polisi...?)
“Tunafanya uchunguzi ili kujua ilikuwaje amiliki kiwango kikubwa cha risasi, pamoja na kumiliki silaha aina ya bastola kinyume na sheria ya Mkoloni Mweusi Tanganyika inayokataza watu binafsi kumiliki silaha za moto.
Upekuzi huo ambao ulifanyika chini ya ulinzi mkali wa polis wa jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika saa saba za mchana ulichukua saa zipatazo mbili na baadaye waziri huyo wa zamani alifikishwa katika Makao Makuu ya Polisi kabla ya kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Madema kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.
Mansour alipakiwa katika gari aina ya Toyota Landcruiser, iliyokuwa ikisindikizwa na gari nyingine za Polisi wa Mkoloni Mwesi Tanganyika iliyokuwa na askari wa FFU, wakiwa na silaha.
Mara baada ya kufikishwa Makao Makuu ya Polisi, baadhi ya ndugu wakiwamo watoto wa Rais mstaafu wa nchi ya Zanzibar, akiwamo Fatma Karume ambaye ni mwanasheria pamoja na mdogo wake Abeid Amani Karume ambao walikuwa wakifuatilia hatua zote zilizokuwa zikichukuliwa na Jeshi hilo la MKOLONI MWESI TANGANYIKA.
“Mimi ni mwanasheria naomba kuwepo hatua zote za mazungumzo” alisema Fatma Karume muda mfupi baada ya waziri huyo wa zamani kuchukuliwa kwa ajili ya kufikishwa katika kituo cha Polisi Madema.
Vitu vingine vilivyokamatwa na Jeshi hilo ni pamoja na kompyuta mpakato (laptop) na vifaa vingine vya mawasiliano ambavyo vyote vinaendelea kufanyiwa uchunguzi atii tusistajab ikiwa hiyo laptop hata pewa tena.

No comments:

Post a Comment