Tuesday, August 5, 2014

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA AMFIKISHA MANSOUR YUSSUF HIMID KATIKA MAHAKAMA YAO FEKI VUGA


Aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la kiembe samaki Mh.Mansour Yussuf Himid akishuka gari maalumu ya Polisi kuelekea Mahakama kuu Vuga,Picha na Mazrui media.Mkoloni Mwesi Tanganyika na (SMZ) Wauwaji leo Mansour Yussuf Himid amepandisha katika mahakama yao feki ya Mkoa Vuga iliopo ndani ya manispaa ya magharib nchini Zanzibar kama walivyowafanya viongozi wengine wanaogombea nchi ya Zanzibar kuwa HURU atii akikabiliwa na tuhuma za makosa matatu ikiwemo kukutwa na silaha, risasi na marisau.
Wakati akisomewa mashitaka hayo mwendesha mashitaka kutoka ofisis ya Mkurugenzi wa mashitaka( DPP MASHUZI) Maulid Ali amesema mtuhumiwa huyo mnamo Agosti 2, mwaka huu majira ya saa 7.18 huko nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa mjini magharib  alikutwa na silaha aina ya pistol (Director) yenye namba F76172 W.
Kitendo hicho cha kumiliki silaha kimedaiwa mahakamani feki hapo kuwa ni kwenda kinyume na kifungu cha sheria no 6(3) na 34 (1) (2) cha sheria ya silaha na risasi No 2 ya mwaka 1991 sura ya 223 sheria ya Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Na atii Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kupatikana na risasi za moto 295 za pistol jambo ambalo pia ni ni kosa kisheria za Mkoloni Mweusi Tanganyika.
Aidha Kosa la tatu ni kupatikana na marisau 112 ya bunduki aina ya short gurn( gobore) baada ya marisau 50 aliyotakiwa kuwa nayo kisheria.
Kwa upande wake mtuhumiwa Mansour Yussuf Himid mtoto wa Jenerel wa kwanza nchini Zanzibar aliyakana makosa yote hayo matatu aliyosomewa Mahakamani feki hapo.
Naye Mwendesha mashitaka na kibaraka wa serikali ya Mkoloni Mweusi Tanganyika Maulid Ali aliomba mahakama ipange siku nyengine ya kutajwa kesi hiyo kwani ushahidi bado haujakamilika.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo Khamis Ramadhani ameiambia mahakama hiyo kuwa makosa mawili ya mtuhumiwa yana dhamana lakini kosa moja la kukutwa na silaha halina dhamana.
Wakili wa mtuhumiwa,Mansour Yussuf Himid Gasper Nyika amedai mahakamani hapo kuwa wanakusudia kupeleka ombi la dhamna katika Mahakama kuu nchi hapa Zanzibar.
Hata hivyo Hakimu Khamis ameiakhairisha kesi hiyo hadi Agosti 18 mwaka huu kwa kutajwa na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi tarehe hio wakati kesi yake itakapotajwa tena Mkono wa Mkoloni Mweusi Tanganyika sasa wataka kmtia adabu mansour hawajwi kuwa ndio kwanza wanamuongezea umarufu na kupendwa na watu.

No comments:

Post a Comment