Friday, August 22, 2014

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA AWATHALILISHA KIJINSIA NA KUWAPIGA WAKIWA UCHII WA MNYAMA WAZANZIBARI WALIO WATEKA NYARA NA KUWAFUNGA KATIKA JELA ZAO KINYUME CHA SHERIA

uamsho+clip
Wanachama na Wananchi wa nchi ya Zanzibar wa kundi la uamsho atii wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi wakitoka wakiwa chini ya ulinzi wa Magereza ya Mkoloni Mweusi Tanganyika walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika jana.
Asema: “Waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”(( nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi Makaburu Weusi wajifanya Wamarekani nambari 2 sasa))
Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu kutoka nchini Zanzibar (Jumiki), akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) wameilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi “walitumia ushenzi na ukatili” wakati wa kuwahoji.
Sheikh Farid na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne waliyobambikiwa na nchi ya Tanganyika Makaburu Weusi atii likiwamo la kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.
Washtakiwa hao walitoa malalamiko hayo jana kwa Hakimu Mkazi, Hellen Liwa muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kuiomba Mahakama iwaruhusu washtakiwa saba kwenda polisi kuhojiwa kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Baada ya wakili huyo kuwasilisha ombi hilo, Sheikh Farid aliuliza: “Wametuomba tena kwenda kuhojiwa...???? Kwanza waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”.
Sheikh Farid alidai kuwa kiongozi Mkuu wa Jumuiya za Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem alimweleza watu hao walichomfanyia.
Hata hivyo, Hakimu Liwa alimkata kauli Sheikh Farid na alimwambia alimtaka kuzungumzia kile ambacho amekiona siyo cha kusimuliwa.
Sheikh Farid Aliendelea kueleza: “Walipigwa na wala hawakupewa matibabu na watu wameumizwa, utakuta wanakojoa damu wiki moja hadi mbili, tunaomba wafanyiwe uchunguzi wa afya zao.”
Mshtakiwa Salum Ali aliiomba Mahakama kupeleka daktari mahabusu kwa madai kuwa wanafanyiwa vitendo vya ‘kuingiliwa kinguvu kinyume cha maumbile’ na kuhoji kwa nini wamekamatwa nchini kwao Zanzibar na kusafirishwa mpaka nchini Tanganyika na kushtakiwa katika nchi ya Tanganyika wakati waliokamatwa Arusha walishtakiwa huko huko na hawakupelekwa hata Dar es Salaam au nchini Zanzibar kwa nini sisi tufanyiwe hivi.......????
Akiendelea kutoa malalamiko yake, Sheikh Farid alidai kuwa wao wamekamatwa kwa sababu hawautaki Muungano na kwamba huo ndiyo msingi wa kesi hiyo.
Baada ya kauli hiyo, Hakimu Liwa kutaka kuziba ziba na kuwavunja moyo alisema: “Tupo kwenye mchakato wa Katiba Mpya na masuala ya muungano yanatajwa mbona watu wanasema na hawakamatwi......????”
Mara baada ya Hakimu Liwa kusema hayo, Sheikh Farid alisema ni kwa sababu wao wanahubiri ukweli na watu wanaukubali.
Hakimu Liwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au laaa.
((kwa mara nyengine tena wanapelekwa mahakamani wakati upelelezi haujakamilika ni kwa nini basi munawapeleka mahakamani au ndio munataka musikie mulichowafanyia huko jela na sisi wandishi tuandike kisha watu wengine wakisoma waogope kutetea nchi yetu ya Zanzibar ndio nia yenu sio....???))
Katika kesi hiyo, Sheikh Farid na Jamal Nooridin Swalehe (38) waliunganishwa na wenzao 18 mahakamani hapo.
Mbali na Sheikh Farid na Jamal, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni, mwaka huu walipanga njama ya kutenda makosa hayo na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi lakini ukweli wa mambo ni kuwa wanapigania nchi ya Zanzibar kuwa huru na hawautaki MUUNGANO FEKI WA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NDIO MAANA WANAWASINGIZIA KESI HIZO WANAZO ZIJUWE WENYEWE MAKABURU HAWA WEUSI TANGANYIKA.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO HAITAKUFA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment