Tuesday, September 16, 2014

BALOZI MDOGO WA NCHI YA TANGANYIKA ALIYEPO NCHINI ZANZIBAR BALOZI IDDI ASEMA KAZI YA VIONGOZI WADINI NI KUOMBEA WATU NA VIONGOZI ((WATAWAOMBEA VIPI NA NYINYI MNAWAFUNGA JELA NA KUWALAWITI NA KUWAITA MAGAIDI...?? ))


Makamo wa Pili wa Rais wa Maskani ya Kisonge, Balozi Iddi,              
Makamo wa Pili wa Rais wa Maskani ya Kisonge, Balozi Iddi, amesema viongozi wa kidini wanapaswa kuwa macho kuzikataa choko choko na ushawishi unaotolewa na wanasiasa.Alisema kazi inayotakiwa kufanywa na viongozi hao ni kuwaombea watu wakiwemo viongozi wa nchi ili baraka ziongezeke ndani ya taifa pamoja na umma jambo ambalo litasaidia kupunguza misuguano.
Alisema hayo wakati akilifungua tamasha la kuliombea taifa na kuhamasisha amani, linalofanyika ukumbi wa Masai Laugwa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.Alisema amani na utulivu wanaojivunia Watanzania miaka mingi sasa ni miongoni mwa neema zinazopaswa kutumiwa vizuri.Alisisitiza njia nzuri ya kuzitumia neema hizo ni kwa wananchi kuzidisha juhudi katika uzalishaji mali wiwandani na mashambani, kuzidisha upendo na mshikamano bila ya kujali rangi, kabila au asili ya mtu.
Aliitahadharisha jamii kutotoa nafasi kwa watu wenye nia mbaya ya kutaka kuliangamiza taifa na kulitumbukiza kwenye vurugu na mapigano. “Mimi kamak wa serikali kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na wananchi wenye nia njema na taifa letu tutaendelea kufanya kazi wakati wote na tutahakikisha amani na utulivu inadumu ndani ya nchi yetu ambayo ndio maisha yetu,” alisema. Alitoa wito kwa akina mama kuendelea kuwa walinzi na wasimamizi wa amani na utulivu.
Alisema mara nyingi wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa wa vurugu, hivyo amani ndio suluhisho pekee la
kuwalinda. “Mara nyingi tunashuhudia kwenye vyombo vya habari jinsi wanawake na watoto wanavyokufa au kujeruhiwa kutokana na vita vinavyozuka katika maeneo yao,” alisema. Akizungumzia dawa za kulevya ambazo ni tishio a vijana, alisema serikali inachukua juhudi kupambana na janga hilo.
Alisema serikali zote mbili zinachukua hatua za makusudi katika viwanja vya ndege na bandari kwa kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu na kupunguza kasi ya uingizaji.Aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi ili kuwabaini wahusika wakuu wa mtandao wa biashara hiyo. Alilipongeza kanisa la Restoration kwa jitihada linazochukua kuokoa maisha ya vijana walioathirika na dawa za kulevya.
Mapema Askofu Sedrick Ndonde wa kanisa hilo, alisema taifa limekuwa na cheche hatarishi inayoonekana kuchochea choko choko za kidini, kisiasa pamoja na vitendo vya kigaidi. Alisema hali hiyo inayokwenda sambamba na matumizi ya dawa za kulevya inasababisha mfumko wa uhalifu unaowafanya wananchi waendelee kuishi katika maisha ya hofu.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment