Friday, September 5, 2014

MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA A.K.A (TANZANIA,TANZANIA BARA,TZ,BONGO LAND) AENDELEA KUWATESA WAKOMBOZI WA NCHI YA ZANZIBAR NA KUWAPAKA MAVI ATII NI MAGAIDI


Nchini Tanganyika Dar es Salaam. Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu nchini Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed amemuomba Rais kuunda tume itakayowahusisha watu kutoka Tanganyika, nchi ya Zanzibar, wanasheria na madaktari ili waweze kuchunguza afya zao.
Sheikh Farid aliyaeleza hayo jana muda mfupi baada ya mawakili wa Serikali Peter Njike na George Barasa kuiomba mahakama kubadilisha hati ya mashtaka atii ya ugaidi iliyokuwa ikiwakabili na kumuunganisha Sheikh Mselem Ali Mselem na mwenzake Abdallah Said Ali na kufanya idadi ya washtakiwa hao wa ugaidi kufikia 22.
Farid alimueleza hakimu kuwa anacho cha kusema na akapewa nafasi, kisha akasema kuwa Agosti 6 na 21, 2014 walifika mahakamani hapo na kueleza matatizo, madhila na unyama waliofanyiwa na polisi na siyo magereza.
Alisema kuwa gerezani wanaishi vizuri kwa kufuata sheria isipokuwa suala la matibabu ambapo aliongeza kuwa uwezo wa bajeti yake ni mdogo hivyo wanashindwa kuwatibia jambo ambalo linasababisha waagize dawa nje wakati ugonjwa huwa hausubiri.
“Watu wameingia gerezani wanaumwa wanavuja hadi usaha kutokana na kipigo walichopewa na polisi hivyo tunamuomba Rais aunde tume kutufanyia uchunguzi wa afya zetu,”alisema na kuongeza;
“Sisi tunachodai siyo uchochezi ninayoeleza polisi wapo wameyasikia tumekamatwa na kushtakiwa Tanganyika kwani Zanzibar siyo nchi.....????????????” aliuliza Sheikh Farid.
Hakimu Hellen Liwa na akamjibu Sheikh Farid  kuwa yeye anachojua wote ni Watanzania na suala la Muungano wengine wanauamini na wengine wanataka ukazikwe Butiama.
Hakimu alimtaka aandike kwa maandishi malalamiko yake ili waweze kuyapeleka sehemu husika na kuiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 17, 2014.
Baada ya kutolewa kwa ombi hilo, Hakimu Hellen Liwa alikubaliana na ombi hilo na mawakili hao waliwaunganisha washtakiwa hao na kuwasomea mashtaka manne mapya.
Mawakili wa Serikali, Njike na Barasa jana walidai mbele ya Hakimu Liwa kuwa washtakiwa hao walijihusisha na mashtaka yakiwamo ya kula njama na kuwaingiza watu kushiriki vitendo vya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Njike alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja waliwaingiza nchini Sadick Absaloum na Farah Omary ili kutenda makosa ya ugaidi.
Sheikh Farid na Mselem kwa makusudi wanadaiwa kutoa msaada kwa Absaloum na Omary ili waweze kushiriki katika vitendo vya kigaidi.
Mbali na shtaka hilo, Sheikh Farid anadaiwa kuwa kwa makusudi aliwahifadhi Absaloum na Omary wakati akijua fika walikuwa wakishiri katika kutenda vitendo vya ugaidi.
Baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo ya ugaidi, Sheikh Faridi na wenzake walitakiwa wasiongee kitu chochote kwa sababu mahakama ya hakimu mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hadi mahakama Kuu.
CHAJABU NI KUWA MAHAKAMA HII HAINA UWEZO WA KUSIKILIZA KESI HII KWA NINI BASI MUNAWAPELEKA KILA WAKATI KATIKA MAHAMA HIYO HIYO AMBAYO HAINA UWEZO WA KUSIKILIZA KESI HIYO.....? WAKOLONI WEUSI NYIEEE ANGALIENI SANA MUNAJIONA MUNA DOLA BASI MUNAONA MTAONEA WATU MUTAKAVYO MUTATESA WATU MUTAKAVYO SAWA NYERERE BABU YENU YUKO WAPI,HITLER N.K.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment