Thursday, May 21, 2015

DIKTETA NKURUNZIZA WANANCHI WA NCHI YAKO YA BURUNDI WASHAKUPA TALAKA HATA UKIJITIA PODA HUPENDEZI TENA


DIKTETA NKURUNZIZA BADO HAJAKUBALI KUSIKILIZA WANANCHI WAKE

MOJA WA MAJENERALI NCHINI BURUNDI AKIFIKISHWA MAHAKAMANI JE DIKTETA NKURUNZIZA ATAFIKISHWA LINI MAHAKAMANI KWA KUVUNJA KATIBA NA KUTAKA KUBAKI MADARAKANI KWA MUHULA WA TATU AMBAYO NI KINYUME NA KATIBA YA NCHI YA BURUNDI NA KUSABABISHA KULIWA KWA WANDAMANAJI 20 WASI NA HATIA.

BAADHI YA WANA MAPINDUZI NCHINI BURUNDI WAKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA MAPINDUZI KUFELI

WAKIMBIZI KUTOKA NCHI YA BURUNDI WAKIWA NCHINI TANGANYIKA

Bujumbura, Nchini Burundi. Maofisa 17 wa Jeshi la Burundi wametiwa mbaroni wakiwamo majenerali watano na kufikishwa mahakamani kwa atii kwa kosa la kuipindua Serikali ya Dikteta Pierre Nkurunziza. Wanajeshi watatu wametajwa kuwa vinara wa kupanga njama za kuipindua Serikali ya Burundi ya Dikteta Nkurunziza wakiwamo maofisa wawili wa ngazi za juu wa polisi. Msemaji wa Ikulu wa nchi ya Burundi,Muhafidhina wa Dikteta Nkurunziza Gervais Abayeho alisema jana kwamba washtakiwa wengine wanne ni maofisa wenye vyeo vya chini na wanane ni wanajeshi wa kawaida. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kukamatwa kwa Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye aliongoza mapinduzi hayo.
Askari hao wanatuhumiwa atii kwa kufanya jaribio la kumpindua Dikteta Nkurunziza wakipinga  uamuzi wake wa kugombea urais kwa muhula wa tatu ambayo ni haki yao maana katiba imesema hivyo mihula miwili lakini Dikteta Nkurunziza utamu wa madaraka umemkolea anataka kuongeza wa Tatu ni kuvunja katiba ya nchi ya Burundi na makubaliano ya amani yaliyo fanyika nchini Tanganyika jijini Arusha. Abayeho alisema wakati maandamano yakiendelea Bujumbura kupinga uamuzi wa Chama cha CNDD-FDD kumteua Dikteta Nkurunziza kugombea nafasi hiyo kwa mara nyingine,  Meja Jenerali Niyombare alitangaza kutomtambua Dikteta Nkurunziza kama rais wa nchi hiyo ya Burundi. Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walisema kwamba baada ya wateja wao kukamatwa waliteswa na kuumizwa.
 “Wamepigwa na ukiwatazama wamechoka na hawana mashati wala viatu,” alisema mmoja wa mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao kutoka Kampuni ya Mawakili ya Bar, Miburo Anatole. Anatole alisema anamwakilisha Meja Jenerali Cyrille Ndayirukiye ambaye alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo na maofisa wawili wa polisi. Wakili mwingine, Cyriaque Nibitegeka alisema mteja wake ambaye ni ofisa wa jeshi la nchi hiyo alilazimishwa kwa mtutu wa bunduki kukiri kwamba alihusika kuipindua nchi hiyo. Alisema mteja huyo amegoma kula tangu walipokamatwa wiki iliyopita. Taarifa zilieleza kwamba endapo watuhumiwa hao watapatikana na hatia watahukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani swali je Dikteta Nkurunziza akipatikana na hatia ya kuvunja katiba na kutaka kuwa raisi kwa muhula wa tatu na jeshi lake la polisi kuuwa rai wasio na hatia kwa jili tu ya kuandamana je yeye Nkurunziza atafungwa kifungo cha miaka mingapi....?
Ijumaa iliyopita, Dikteta Nkurunziza alirejea mjini Bujumbura akitokea nchini Tanganyika, huku maandamano ya kumpinga yakiendelea kama kawaida. Licha ya Serikali yake kuzuia kufanyika kwa maandamano, waandamanaji vikiwamo vyama vya upinzani na wananchi wameapa kuendelea hadi Dikteta Nkurunziza atakapotangaza kuacha mpango wake wa kugombea tena urais. “Tutaendelea kufanya maandamano kwa kuwa malengo yetu ni kumtaka Nkurunziza aache kugombea urais muhula wa tatu. Tunaona wanajaribu kuzuia maandamano yetu, lakini sisi hatutasitisha maandamano. Tutaendelea kuipigania katiba ili iheshimike,” alisema Jean Paul Ndayiragije.
Uchaguzi mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika Juni 26, mwaka huu.
Jaribio la kumpindua Dikteta Nkurunziza lilitekelezwa na Meja Jenerali Niyombare na maofisa wenzake wa jeshi wakati Nkurunziza akiwa nchini Tanganyika kuhudhuria mkutano wa dharura kuhusu mgogoro unaendelea nchini humo, lakini mapinduzi hayo yalizimwa na Maofisa Wahafidhina wa jeshi wanaomtii Dikteta Nkurunziza ili aendelea kubaki madarakani na wao waendele kuula bure na kuwawacha wananchi wakiwa katika hali mbaya ya maisha.
Wakimbizi wa Burundi walio kimbia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa nchi ya Tanganyika, Isaac Nantanga alisema Serikali imetoa ushirikiano mzuri katika shughuli ya  kuwapokea wakimbizi wanaotoka nchi ya Burundi. Zaidi ya watu 105,000 wameikimbia Burundi, 70,000 wameingia nchini Tanganyika na 26, 300 wamekimbilia nchini Rwanda tangu kuanza kwa vurugu nchini Burundi. Wakimbizi wengi wanaishi katika Kambi ya Mahama. “Taarifa zinaeleza kwamba watu 10,000 wako mpakani mwa nchi ya Tanganyika na Burundi wakisubri kuingia katika kambi ya wakimbizi mkoani Kigoma,” lilisema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).
Dikteta Nkurunziza Faida Gani Umeipata Kwa Kulazimisha Kuka Madarakani...??
Kwa mara ya kwanza, Dikteta Nkurunziza alionekana hadharani jana, huku akiwa amevaa kaunda suti ya bluu. Alionekana akijikaza kisabuni na kujitia kutabasamu, huku akiwasalimia waandishi wa habari na kuzungumza masuala ya ugaidi..!!!!!!! bila kugusia jaribio la kuipindua serikali yake. Dikteta Nkurunziza alizungumzia tishio la ugaidi ambalo limetolewa na kundi la   Al-Qaeda ambalo lina uhusiano na wanamgambo wa Al- Shabaab.((huyu jamaa anachanganyikiwa nini...?)) “Tumechukua tahadhari dhidi kundi la Al-Shabaab, tishio hili tumelichukua kwa umakini mkubwa kwa ajili ya usalama wa raia wetu,” alisema Dikteta Nkurunziza.
Burundi na nchi nyingine za Afrika zimepeleka majeshi ya kulinda amani nchini Somalia.  Katika tukio jingine, Raia wa Burundi wanaoishi Uingereza wamemuomba Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron kusimamisha misaada ya kifedha kutokana na msimamo wa Dikteta Nkurunziza.  Raia hao walisema  uamuzi wa Dikteta Nkurunziza ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo ya Burundi.
Watu hao waliandamana juzi jijini London wakipinga Dikteta Nkurunziza kukiuka katiba na watu 22 waliouawa kwenye maadamano mjini Bujumbura nchini Burundi. Waandamanaji hao walikuwa wamebeba bendera ya nchi hiyo, huku wakitaka Serikali kulinda amani na kumtaka Dikteta Nkurunziza aache kugombea urais muhula wa tatu. Kwa mujibu wa Muungano wa Ulaya (EU), Burundi imekuwa ikipewa msaada wa Dola 6 milioni mpaka 9 za Marekani kwa ajili ya kusaidia shughuli za uchaguzi mkuu kila unapowadia.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment