Tuesday, May 12, 2015

MKURUGENZI WA ZEC SALUM KASSIM ALI NA VUAI ALI VUAI WAJARIBU KUMJIBU MAALIM SEIF NA KUTUNZA TONGE ZAO ZISIWATOKE


HUYU NDIO MKURUGENZI WA ZEC , SALUM KASSIM ALI AKIJARIBU KUMJIBU MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD

Nchini Zanzibar. Siku moja baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kutoa tuhuma nzito dhidi ya Tume ya Uchaguzi ya nchi ya Zanzibar (ZEC), kuandikisha wapigakura wasio na sifa, tume hiyo imeibuka na kukanusha vikali je wanakanusha ni kweli au wanalida mafupa yao na tonge zao kwenda katika matumbo yao ziendele.....??
Mkurugenzi wa ZEC, Salum Kassim Ali alisema jana kuwa hakuna majina ya marehemu yanayoendelea kutumika katika Daftari la Kudumu la Wapigakura hivyo CUF iache kuipotosha jamii. Alikuwa anajibu madai ya Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa ZEC iliandikisha na kuruhusu wapigakura wenye umri wa chini ya miaka 18, walioandikishwa mara mbili, wasiokuwa wakazi na waliotumia ama majina au picha za watu wengine. Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha CUF, alisema madai hayo yamebainika katika utafiti uliofanywa na chama hicho ili kubaini hujuma zilizofanywa na SMZ na taasisi zake ambazo zinaweza kufanyika pia katika uchaguzi ujao.
Katika majibu yake, Salum Kassim Ali alisema sheria na taratibu za uchaguzi kabla ya kupiga kura, yaani daftari huhakikiwa na majina kubandikwa hadharani katika vituo vya kupigia kura zilifanyika, hivyo kama kungekuwa na dosari, zilipaswa kuwekewa pingamizi. Akiendelea kusema sekretarieti ya ZEC inafanya kazi zake kwa maelekezo ya makamishna wake wakiwamo wawili kutoka CUF ambao wanafanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa na hayakuwahi kujitokeza malalamiko hayo. (( realy ))
Alisema kabla ya kuanza uandikishaji mwezi huu, ZEC ilikutana na wadau vyama vya siasa na kuwaeleza mambo manne yatakayofanyika ambayo ni uandikishwaji wa mwisho kwa wapiga kura, kuhakiki daftari la wapigakura, ikiwamo kuondoa waliokufa, kubadilisha taarifa na kuhamisha taarifa za wapigakura. Alisema endapo kungekuwa na kasoro, makamishna hao wa CUF ndiyo wangekuwa wa mwanzo kulalamika kwa vile wapo jikoni na siyo viongozi wa chama wanaolalamika kwenye vyombo vya habari.
“Kama kweli ana ushahidi wa kile anachokizungumza, kwa nini haleti malalamiko yake ZEC badala yake analalamika kwenye vyombo vya habari?” alihoji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, Mohamed Juma Ame alisema viongozi wenye dhamana wanapaswa kufanya utafiti na kupata ukweli kabla ya kutoa shutuma nzito ili wananchi wapate taarifa sahihi. Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari Mkaazi, mtu yeyote kabla ya kusajiliwa, anatakiwa awe na cheti cha kuzaliwa, barua ya sheha na haiwezekani mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 kupewa kitambulisho hicho. (mnawapa ili wawapigie kura CCM na nyinyi mbaki hapo mlipo mkila bure)
Alisema kabla ya kuandikishwa kuwa mpiga kura, lazima mtu awe na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na masharti ya kukipata lazima awe na cheti cha kuzaliwa na sheha amtambue. ((ndio maana masheha wanawatambuwa wamasai na warundi lakini hawawatambui wazanzibari halisi....?))  Mkurugenzi huyo alikanusha madai ya kuwepo kwa kambi ya jeshi inayotumika kuandikisha na kuwapatia watu vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi bila sifa, akisema idara yake haina uhusiano wowote na kikosi wala jeshi lolote hapa nchini.
Alisema Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais, hivyo ana uwezo wa kumwita ofisini kwake wakati wowote kumwelezea madai yake, lakini hajawahi kufanya hivyo isipokuwa mara moja baada ya mtoto wake wa kumlea kukwama kupata barua ya sheha ya kumwezesha kupata kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi. ((ama kweli hili jitu hasa jinga, pumbavu, zebwe,juha sasa wewe mtoto wa mkamo wa raisi kakwamishwa na sheha itakuwa watoto wa rai wa kawaida itakuwa vipi hii mijutu sijuwi inatolewa pori gani na kupewa hizi kazi.))
Alisema utafiti wa CUF una kasoro kubwa kwa vile mamlaka inazozishutumu hazikupewa nafasi ya kujieleza dhidi ya malalamiko hayo, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za utafiti.
Kuhusu madai kuwa baadhi ya wafuasi wa CUF hawapatiwi vitambulisho vya ukaazi, alisema kuna zaidi ya vitambulisho 20,000 ambavyo havijachukuliwa na wahusika, wengi wao kutoka Pemba.(( si mumevizui watakuja kuchukuwa vipi na hata wakija hamuwapi muwazungusha tu kwani hatujuwi mbinu zenu nyinyi))
Kuhusu Shein
Akizungumzia madai kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anatakiwa kuanza kujitayarisha kisaikolojia kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema Maalim Seif hana ubavu wa kuiangusha CCM visiwani hapa.
Alisema kama alishindwa akiwa kijana hawezi kufikia malengo hayo akiwa mzee.
Vuai alisema Dk Shein ana kila sababu za kushinda kutokana na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi, kulinda misingi ya amani na umoja wa kitaifa na ndiyo maana Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeendelea kuwapo na kuhudumia wananchi wake.
Vuai alisema endapo Maalim Seif haridhishwi na utendaji wa ZEC alitakiwa kuzungumza ndani ya Baraza la Mapinduzi na si kwenye vyombo vya habari, jambo ambalo linazorotesha malengo ya maridhiano yaliyozaa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment