Monday, May 25, 2015

MSANGI SIO MKUU WA UPELELEZI BALI NI MKUU WA UKANDAMIZAJI WA WAZANZIBARI WASIDAI NCHI YAO YA ZANZIBAR


HUU NI USHAHIDI TOSHA KUWA MSANGI KUMEMSHINDA MKOANI SIMIYU KWAO KWA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA WAKAONA WAMLETE NCHINI ZANZIBAR AJE ATIMIZE KAZI YA BABU YAO NYERERE YA KUIFISIDI NCHI YA ZANZIBAR NA KUWATESA WAZANZIBARI NDANI YA NCHI YAO HAKUNA LA AJABU

Tuugeukie sasa upuuzi wa Naibu Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai kutoka nchini Tanganyika aliyeletwa hapa nchini Zanzibar katika Jeshi la Polisi Zanzibar ili aje wawshughulikiye Wazanzibari wote wanao taka Zanzibar Huru yanye Mamlaka Kamili, Kamishna Msaidizi Msangi, ambaye siku moja baada ya Waziri Mkuu Pinda Mr Zanzibar sio Nchi kuyasema hayo bungeni, yeye aliwaita waandishi wa habari kwenye chumba cha mikutano Makao Makuu ya Polisi kuwatangazia wananchi kukamatwa kwa vijana wawili, Said Ali Abdullah mwenye umri wa miaka 26 mkaazi wa Kiwani, Pemba nchini Zanzibar, na Hussein Mageni Hussein mwene umri wa miaka 27 mkaazi wa Pangawe, Unguja nchini Zanzibar, kwa makosa ya kuwatukana Raisi wa maskani ya Kisonge  Shein na rafiki yake Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika aliepo hapa nchini Zanzibar, Balozi Seif Iddi, wakitumia mitandao ya simu.
MSANGI LABDA HUKUJUWA YALIO TOKE MIMI NAKUSAIDI KUKUPATIA PIC ZA WATU WALIO PINGWA MAWE WAKATI WAKIRUDI MKUTANONI WA CUF JANJAWEED WENU WAKAWAPIGA MAWE SASA UPELELEZI WAKO UMEISHIA WAPI
Upuuzi wa Kamishna Msaidizi Msangi upo kwenye ngazi nyingi, na hapa nitazitaja tatu: kwanza, kwenye kutupambaza sote, akitaka tuamini kuwa kilichofanywa na jeshi lake kilikuwa kitu sahihi kwa kuwa tu kinachoshukiwa kufanywa na vijana hao hakikuwa si sahihi. Kwa mfano, kijana Said ambaye anatajwa kwengineko kuwa ni kiongozi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Mkoani, Pemba, amekamatwa kwa kosa la kumtukana Balozi Seif kwa kumtaka asiende kisiwani Pemba kufanya mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini kwenye vidio ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ambayo ndiyo ushahidi pekee wa Kamishna Msaidizi Msangi, Said anasema pia kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM, Balozi Seif, asijaribu kuwazuia wanachama wa CUF kufanya mikutano kwenye jimbo la Kitope lililo Kaskazini B kisiwani Unguja, kwa kuwa wao CUF hawamzuii yeye kufanya mikutano Pemba, ambako CCM haina jimbo hata moja. Kwa hivyo, Msangi anatupumbaza kwa kutuambia nusu ukweli na nusu uongo. Hasemi kuwa kauli hiyo ni majibizano ya kisiasa kati ya vyama vya siasa.MSANGI UPELELEZI WAKO UMEISHIA WAPI KATIKA ILE KESI YA WAFUWASI WA CUF KUPINGWA MAWE NA JANJAWEED WA CCM CHAMA CHANU CHA WAKOLONI WEUSI TANGANYIKA....???
Pili, upuuzi unakuja pale jeshi la polisi linapotangaza kuwachukulia hatua vijana hawa wa CUF, lakini likiwaacha vijana na viongozi wa CCM ambao wanaowatukana viongozi wakuu wa CUF kwa matusi makubwa kuliko hayo yaliyoripotiwa kusemwa na Said. Hapa upuuzi unamaanisha kutenda jambo lisilo maana, kwa sababu hatua hii inayochukuliwa na taasisi yenye jukumu la kusimamia usalama wa raia na mali zao imekosa maana yoyote ya kiusalama kwa kuchukuliwa kwake inachukuliwa kibaguzi. Inakuwaje kumtukana Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa mfano, kuwe si jambo la kuchukuliwa hatua za kiusalama na polisi, lakini lichukuliwe hatua inapotokezea aliyetukanwa na mjumbe wa kamati kuu ya CCM, Balozi Iddi....???MOJA KATIKA WAFUWASI WA CUF WALIO PINGWA MAWE NA JANJAWEED WA CCM WAKITOKEA MKUTANONI MAKUNDUCHI NA KUFARIKI MSANGI UPELELEZI WAKO UMEISHIA WAPI....???
ALIPOULIZWA KUHUSIANA NA HILO, MSANGI ALISEMA POLISI HAWAJAWAHI KUWAKAMATA WALE WANAOWATUKANA VIONGOZI WA CUF KWA KUWA WENYEWE VIONGOZI WA CUF HAWAJAWAHI KUWASHTAKIA MAKOSA HAYO, AKITAKA TUAMINI KUWA SHEIN NA BALOZI SEIF WALIKWENDA KUFUNGUA JALADA LA MALALAMIKO MAKO MAKUU YA POLISI, MADEMA. HUU NI UPUUZI ULIOPITILIZA.
Tatu ni upuuzi kwa kuwa umesemwa kipuuzi. Kwa mfano, kwenye maelezo yake Kamishna Msaidizi Msangi anawataja vijana hao kuwa ni wahalifu na anaelezea kushangazwa kwake kuwa kuna mawakili walikwenda kutaka kusimamia mahojiano yao, akiwemo mwakilishi wa jimbo la Kiwani kwa tiketi ya CUF, jimbo ambalo ndilo analotokea kijana Said. Ikiwa maadili ya kipolisi na sheria za mwenendo wa mashitaka anazijuwa na si mpuuzi, basi Kamishna Msaidizi huyu anajuwa tafauti baina ya neno “mtuhumiwa” na “mhalifu” kama anavyojuwa pia haki ya kila mtuhumiwa kuwa na wakili. Mtuhumiwa anabakia kuwa na haki zote za utuhumiwa na si mhalifu hadi hapo mahakama iamuwe hivyo.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment