Thursday, May 28, 2015

PANDU AMIR KIFICHO NI KUBWA LAO KUMBE NDIO JENGA LAO VUAI ALI VUAI AKILI ZAKO UMEZIWEKA KWENYE TUMBO LAKO NDILO LINALO KUPA SHIDA


WAKUU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawachoki kumshambulia Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, licha ya kuwa pia ndiye Makamo wa Kwanza wa Rais wa nchi ya Zanzibar.
Wala hawajali mashambulizi yao yanayofikia kumtusi na kumdhalilisha, kama binaadamu na kama kiongozi katika nchi, yameshindwa kumdhoofisha kisiasa. Kinyume chake, wamezidi kumjenga na matokeo yake, ni hali inayojionesha ya kuimarika kwa CUF, chama alichokiasisi tangu 1992.
CUF imekua isivyo kawaida. Mafanikio yake yanaelezeka kirahisi hata kwa anayeichukia.
  • Kimefanikiwa kueneza itikadi yake ya utajirisho nchi nzima na ughaibuni.
  • Ni sehemu ya Serikali ikiwa na Makamo wa Rais na mawaziri saba.
  • Kimefuta kile wapinzani wake walichokiaminisha kuwa kina nguvu tu Pemba; kina wawakilishi na wabunge Unguja.
  • Kina taarifa nyingi za mipango ya kukihujumu.
  • Kimekuwa kimbilio kuu la wana-CCM.
  • Kimepokea mawaziri watatu wa zamani kutoka CCM.
  • Kimefanikiwa kukusanya raslimali nyingi kwa maandalizi ya uchaguzi ujao.
  • Ndio tumaini la maendeleo na maisha kwa Wazanzibari wakubwa na vijana.
Chama kimekuwa na nguvu kubwa kiasi cha kulazimisha wakuu wa CCM kukosa utulivu,usingiza,mitetemeko ya moyo na kukosa raha katika nafsi zao kwa kuona kinapokwa madaraka. Ile hali iliyokuwepo miaka ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi 1992, ya baadhi ya wana-CUF kuhofia kuvaa hadharani sare za chama, sasa imehamia CCM. Hali ni mbaya kwa CCM kwa sababu baada ya kushuhudia umma wa vijana kwa wazee wake kwa waume wakikitenga CCM na kuchagua CUF, tena kwa fakhari wakikabidhiwa kadi na Maalim Seif, sasa mikutano ya CCM inadharauliwa na wananchi wa nchi ya Zanzibar kwa hali ya juu maana washajuwa wanacho kwenda kukisikia sio kutatuliwa matatizo yao ya kimaisha bali ni matusi kwenda.
Kwa kuwa CCM haiaminiki tena hapa nchini Zanzibar, wengi hawajali kukosa hotuba za viongozi wake au wao. Kule kuamini kuwa watakachosikia ni matusi zaidi, kumechangia kuwatenga na kutoona haja ya kuhudhuria mikutano ya chama hicho. Wiki iliyopita, wakazi wa Magogoni na maeneo jirani, walisogelea mkutano wa hadhara uliotangazwa kwa siku mbili na kuahidiwa mhutubiaji mkuu angekuwa Balozi mdogo wa nchi ya Tanganyika iliyepo hapa nchini Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi. Masikini wee, hakufika mkutanoni, na hakuna sababu iliyotajwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, ya kutofika kwa kiongozi huyo.
“Mnamo saa 11.15 (saa 11 na robo) nilipita nikashuhudia watu wachache wanamsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi kubwa lao kumbe ndio jinga lao,” amesema msomaji wa safu hii aliyenipigia simu Ijumaa wiki iliyopita. Msomaji anasema baadaye alimpigia simu ndugu yake anayeishi karibu na uwanja wa Kwa Mabata, jimbo la Magogoni, ngome ya CUF, na kumuuliza mkutano ulivyomalizika. “Ameniambia Balozi Seif hakufika mkutanoni. Anadhani maofisa wa usalama walimzuia kutoka kwa sababu mkutano ulikuwa na watu wachache sana,” anasema. Nimethibitishiwa na vyanzo ndani ya CCM tukio kama hilo la Balozi kutofika kwenye mkutano wa CCM aliotarajiwa kuhutubia, inakuwa mazoea.
“Usishangae, mara nyingi dakika za mwisho Balozi anazuiwa kwenda mkutanoni kwani kumekosekana watu wa kumsikiliza. Ndiyo hali halisi, chama kina hali ngumu kwa kweli,” anasema. Wananchi waliokuwa wamesimama kwa mbali uwanjani wakisikiliza, wengi wakionekana kama si wapenzi wa CCM, walianza kuondoka, walipomsikia Vuai akiporomosha kauli za Uchochezi na Matusi.
Vuai ambaye Machi mwaka huu alinukuliwa akitamba CCM itahakikisha Maalim Seif anabakia Makamo wa Rais na siyo Rais wa nchi ya Zanzibar, alirudia kauli hiyo, safari hii akija na mapya yanayoonesha namna CCM walivyopanga kung’ang’ania madaraka, wakipuuza msingi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Amenukuliwa akisema, “… tunasema hata siku moja hawezi kuwa rais, haiwezekani na haiwezekani, kama anasema iko siku atakuwa rais, labda Mtambwe kwa sababu ana nia chafu na hawapendi Wazanzibari. Mtambwe ndio kijiji cha nyumbani kwao Maalim Seif, ndani ya Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba. “CCM imejidhatiti na kuhakikisha katika uchaguzi tunaendelea kushinda na kuchukua majimbo yote ya Unguja, baada ya kufanyika mabadiliko makubwa ya mipaka ya majimbo ya uchaguzi.” “Hakuna jimbo la Magogoni wala Mtoni litakalotoka CCM na kuchukuliwa na CUF mwaka huu, tumejidhatiti.” Vuai anasema serikali haitamvumilia mtu yeyote anayeazimia kufanya fujo. Akadai wao wanazijua mbinu za Maalim Seif za kutaka kuleta vurugu.KIFICHO KUBWA LAO NDIO JINGA LAO LIMEJIFICHA WEEEE MPAKA SASA LIMESHINDWA KUJIFICHA LIMEFICHUKA LISIKILIZE LINAVYO BWABWAJI KISHA NDIO SPIKA HUYU NDIO MAANA NCHI YA ZANZIBAR HAENDELEI MAANA TUNA MIJUTI IPO IPO TU KWA MATUMBO YAO.
Wakati huo, Spika Pandu Ameir Kificho na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi, Yussuf Mohamed Yussuf, mbunge mstaafu Mwembemakumbi, walishampakazia Maalim Seif wakimtaja kama kiongozi mchochezi. Yussuf alinukuliwa akimtaja Maalim Seif kama adui mkubwa wa nchi ya Zanzibar na Wazanzibari, ndo maana “amekuwa akizorotesha misingi ya Mapinduzi na Muungano.” Kificho aliye nadra kuhutubia mikutano ya hadhara, alisema Maalim Seif anatoa kauli zinazohatarisha amani wakati ni mmoja wa viongozi wakuu serikalini. Aliipigia chapuo Katiba Inayopendekezwa ambayo aliisimamia ipitishwe licha ya kukosa maslahi yaliyotarajiwa na Wazanzibari na kwa nchi ya Zanzibar kificho anataka ipitishwe tu hili jitu sijuwi namna gani.
Lakini akigusia Mapinduzi ya nchi ya Zanzibar na Muungano feki wa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar, alisema misingi yake ikitetereka, itavuruga mshikamano wakati “Wazanzibari wanaoishi katika nchi ya Tanganyika wanafikia laki tano (500,000) ambao muungano feki ukivunjika Zanzibar itashindwa pa kuwaweka hao Wazanzibari wafikao laki tano.”(nambiya tena hili kificho ni kubwa lao lakini ndio jinga lao) Hakugusia chochote kuhusu mbinu za CCM kuwakusanya kama dagaa Watanganyika na kuwapeleka Zanzibar unapokaribia uchaguzi ili waibebe CCM kwa kura za hila. Bali hajasema lini waliogoma kuondoka nchini Zanzibar baada ya uchaguzi, watarudi Tanganyika. Na ajue Zanzibar kama nchi ya visiwa ina haki, kulingana na sheria za kimataifa, ya kulindwa isivurugwe silka zake.
CCM inaumia sasa kwa mbinu zake kufichuliwa. Isipotengeneza hofu mitaani, CCM haina maringo na haichaguliki. Uonapo viongozi wake wanazidisha mashambulizi kwa Maalim Seif, ni kwa vile tu anazianika njama zao. Analaumu kuitumia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Idara inayotoa Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, kutafuta ushindi wa nguvu. Ni kujiandaa na anguko la kihistoria. Nguvu wanazoongeza za propaganda zinasema dhahiri kuwa arobaini ya CCM imefika. Hakuna Donge, hakuna Makunduchi, hakuna Kiembesamaki wala Kikwajuni. Anguko tu. Tena anguko mbele ya matumizi ya vikosi vya ulinzi na usalama wa taifa. Wakati haukubali tena hila, vitisho, ulaghai na uongo.
CCM inatumia yote hayo, huku CUF imempokea Juma Hamad Omar, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii wakati wa uongozi wa Ali Hassan Mwinyi, na Mohamed Hashim Ismail, naibu waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar. Hamad amejisogeza kwenye uteuzi wa kugombea ubunge jimboni Wawi, ambako Hamad Rashid Mohamed ametema kiti akitangaza kugombea urais kupitia Alliance for Democratic Change (ADC) alichokiasisi baada ya kufukuzwa 2013. Hashim ambaye pia aliongoza Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB), mfano wa TRA, amejisogeza kwenye uteuzi wa kugombea uwakilishi kwao Dimani. CUF tayari inaye Mansour Yussuf Himid, shujaa aliyeapa kuipigania Zanzibar yenye mamlaka kamili tangu akiwa waziri wakati wa Amani Karume na Shein. Wameichagua haki CCM imebakiwa na kipovu cha mwisho.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment