Wednesday, May 27, 2015

SEREKALI YA KIFALME YA OMAN IMEIPATIA NCHI YA ZANZIBAR BILLIONI 12.3 SHILLINGI ZA KITANGANYIKA NA NYARAKA ZA MAGARI 10


Rais wa Maskani ya Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la 

Mapinduzi Shein akipokea Hundi ya Tanganyika Shilingi 

pesa za Mkoloni Mweusi Tanganyika Billioni 12.3 

kutoka Balozi wa Oman  Nchini Tanganyika  Mhe,Saoud Al 

Ruqaishi  ikiwa ni msaada  kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa kwa  

kiwanda cha upikaji Chapa (kushoto  Balozi Mdogo  wa 

Oman 

aliyepo nchini Zanzibar Mhe,Ali Abdulla Al-Rashdi  hafla ya 

makabidhiani ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.


SERIKALI ya Kifalme ya Oman imeikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hundi ya Tanganyika.Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Kiwanda cha Upigaji chapa zikiwemo mashine za kuchapishia magazeti na vitabu. Wakati huo huo, Serikali ya Kifalme ya Oman imeikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nyaraka za gari 10 zilizotolewa msaada na nchi hiyo zikiwemo za viongozi wakuu. Balozi wa Oman katika Jamhuri ya nchi ya Tanganyika Mhe. Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi alimkabidhi Rais wa Maskani ya Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein hundi hiyo pamoja na nyaraka hizo za gari, makabidhiano yaliofanyika leo Ikulu Mjini Mnazi moja nchini Zanzibar.
Mara baada ya kupokea hundi kwa ajili ya vifaa vya kiwanda hicho cha Upigaji chapa pamoja na nyaraka za gari hizo, Rais wa Maskani ya Kisonge na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shein alitoa pongezi kwa Serikali ya Kifalme ya Oman chini ya uongozi wa Mfalme Sultan Qabous Bin Said Al Said kwa msaada wake huo kwa nchi ya Zanzibar. Shein alisema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukamilisha nia na malengo yake ya kuhakikisha inakuwa na kiwanda chake cha kisasa cha Upigaji Chapa ambacho kitachapisha magazeti na vitabu. Katika mazungumzo hayo, Balozi Seif Ali Idd alihudhuria, Shein alisema kuwa msaada huo unaonesha wazi mahusiano na mashirikiano mazuri na ya muda mrefu pamoja na mapenzi yaliopo kati ya Serikali ya Kifalme ya Oman na ndugu zao wa Zanzibar.((duuuh ndugu zao wa Oman sio tena Masultani walio wafanya watumwa....? hahaha kuishi kwingi kuona mengi kweli))
Alisema kuwa msaada huo ni muendelezo wa misaada kadhaa iliyotolewa na Serikali ya Kifalme ya Oman kwa nchi ya Zanzibar ikiwemo ujenzi wa Chuo cha Afya kilichopo Mbweni nje kidogo ya mji mkuu wa nchi ya Zanzibar pamoja na misaada mengineyo ambayo tayari nchi hiyo imeshaitoa. Aidha, Dk. Shein alimuhakikishia Balozi huyo kuwa misaada hiyo itatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa na kusisitiza kuwa nchi ya Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na wa nchi ya Kifalme ya Oman. Dk. Shein, alisema kuwa kwa niaba ya wananchi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ametoa shukurani kwa Serikali ya Kifalme ya Oman kwa misaada hiyo ukiwemo msaada huo wa ukubwa wa fedha. Pamoja na hayo, Shein, kwa mara nyengine tena alimtumia salamu kiongozi wa nchi hiyo na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwa na afya njema yeye pamoja na wananchi wa nchi hiyo ya Kifalme ya Oman.
Mapema Balozi wa Oman Katika Jamhuri ya nchi ya Tanganyika, Mhe. Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi ambaye alifuatana na Balozi Mdogo wa nchi ya Kifalme ya Oman anayefanyia kazi zake hapa nchini Zanzibar Mhe.Ali Abdulla Al Rashdi alieleza kuwa Oman itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake kati yake na nchi ya Zanzibar. Balozi huyo wa nchi ya Kifalme ya Oman nchini Tanganyika alisema kuwa ni matumaini makubwa Serekali yake ya Kifalme ya Oman kuwa msaada huo wa fedha taslim kwa ajili ya ununuzi wa vifaa zikiwemo mashine kwa ajili ya Kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali utasaidia kwa kiasi kikubwa katika utengenezaji wa magazeti na vitabu hapa nchini Zanzibar. Alisema kuwa kiwanda hicho kitawawezesha wananchi wa nchi ya Zanzibar kuweza kuwa na kiwanda maalum cha kuchapisha magazeti pamoja na vitabu.
Pamoja na hayo, Balozi huyo alieleza kuwa gari hizo kumi zikiwemo za viongozi nazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza shughuli za maendeleo hapa nchini. Balozi huyo vile vile, alieleza kuwa Mfalme wa nchi ya Kifalme ya Oman Sultan Qaboos Bin Said Al Said anathamini uhusiano na mashirikiano yaliopo kati ya Oman na Zanzibar na kuahidi kuwa hatua hizo zitaendelezwa kwa upande wa wananchi pamoja na Serikali za pande zote mbili. Upatikanaji wa vifaa hivyo kwa ajili ya Kiwanda hicho cha Upigaji chapa kutakiwezesha kiwanda hicho kuchapisha magazeti pamoja na vitabu mbali mbali hapa nchini Zanzibar.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment