Saturday, June 13, 2015

KAZI YA KUCHIMBA NA KUKATA MAWE INAUWA NDUGU ZETU KWA UKOSEFU WA ZANA BORA



“Tunauza roho zetu  kwa kusaka riziki…. mikono iende kinywani na 

midomo iweze kucheza cheza ‘’.

Hayo ni maneno ya wachimbaji wa mawe eneo la Kwareni  Vitongoji ndani ya 

wilaya ya Chakechake Pemba nchini Zanzibar.“Hatuna hila wala uwezo  

wakutafuta  kazinyengine ya kutuwezesha maisha yetu  ambayo hatuna ajira’’ 

walikua wanalalamika nilipofika machimboni. Pamoja na yote hayo kazi hii  ya 

uchimbaji wamawe  ni hatari wakati mwengine  kupoteza viungo na  kupoteza 

maisha pia. “Najitahidi tu lakini mawazo telee  kichwani na machozi kunilegalega  

nikikumbuka mwenzangu Hamadi Zahor  Faki, alivyo weza kukatikiwa na 

mwamba wa jiwe na kufariki hapo hapo” alinieleza kwa uchungu Abdalla ‘bati 

ambae nikiongozi wa chimbo hilo.

 
Hao ni  baadhi tu ya mamia ya watu, wakati wanapokuwa wakiendelea na kazi 

yao ya  uchimbaji wa  mawe katika eneo hilo kisiwani Pemba , wanapo pambana  

na kazi ngumu na yenye kuhitaji ujasiri. Wengine huchimba mawe hayo hata kwa 

kutumia mapango, na kujikata vidole, huku nyundo nazo zikitawala eneo hilo kwa 

Kware, ambao palichangamka ni sawa na soko la Mwanakwerekwe 

Unguja. Kubwa ambalo unaweza kulishangaa na kudondokwa na machozi hasa 

kwa alie na huruma, ni kuona wapo wanachimba na kuvunja mawe wakikosa 

zanabora za kufanyia kazi  sambamba na mbinu bora za  kuchimbia mawe .

Kalamu ya makala hii, haikutosheka na jicho la mbali, ndipo ilipojongea karibu na 

kumsaka alau mmoja,  na kumkatisha kazi ili aweze kuzungumza name.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment