Tuesday, June 23, 2015

NCHINI ZANZIBAR WAWAKILISHI WA CHAMA CHA CUF WATOKA BARAZA LA WAWAKILISHI NA WAWAKILISHI WA CCM WATAKA GNU IVUNJWE


Nchini Zanzibar Wajumbe wa baraza la wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi CUF leo wametoka nje ya ukumbi wa baraza hilo kwa kile wanachodai ukiukwaji wa sheria, ikiwemo kujaza askari Polisi na wengine wakivaa ninja katika uwandikishaji wa Daftari la wapiga kura linaloendelea nchini Zanzibar. Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Makao makuu ya chama hicho Vuga mjini Unguja nchini Zanzibar walisema kwamba wameamua kutoka kwa lengo la kupinga matokeo ambayo yanendelea kutokea katika uandikishaji wa daftari kwa wilaya za magharbi ambayo yanakwenda kinyume na sheria za Nchi ya Zanzibar. 

Akizungumza kwa niaba ya wawakilishi na mawaziri wa SMZ kutoka upande wa CUF Juma Duni Haji makamo mwenyekiti wa chama hicho alisema ni jambo la kushangaza katika nchi iliokubali demokrasia kuona askari wanavaa ninja bila ya sera zao wakiwatisha watu wanaokwenda kujiandikisha. “Huu jamani ni uhuni unaingiza majambazi katika vituo vya kujiandikisha halafu unasema ni askari wa kulinda Amani, hemu niambieni mumeona wapi mambo hayaa ispokua hapa kwetu” alisema Haji. Alisema tokea uwandikishaji huo kuaza katika kisiwa cha Unguja umekuwa na vurugu kutokana na chama cha Mapinduzi CCM kuingiza wageni na watoto wadogo kutoka nje ya jimbo husika.


Lakini pia Juma duni Maarufu kama Babu alisema wao wametoka barazani lakini wataendelea kuwa mawaziri na wawakilishi mpaka mwisho wa Serikali ya awamu hii. “Sisi ni mawaziri na tutakuwa mawaziri mapaka Rais atakapo sema basi au muda wetu kumalizika, sambamba na wawakilishi hadi litakapo vunjwa baraza la Wawakilishi hapo june 26 mwaka huu” alisema Haji. Alieleza kuwa wataendelea kuitumikia serikali lakini hawatojishuhulisha na shuhuli za baraza hilo kwa kipindi hiki, na hawatohudhuria katika ufungaji wake ambapo Rais wa zanzibar atalihutubia baraza hilo hapo tarehe 26 mwezi huu sambamba na kulivunja rasmi. Kabla ya kutoka barazani humo shuhuli za bara hilo waziri wa Mawasiliano na Miundombinu ndie aliyesimama na kutoa malalamiko hayo kwa spika wa baraza hilo Pandu Ameir kificho, na baadae wote kutoka nje huku wakiacha bajeti ya wizara ya fedha ikiendelea kujadiliwa. Mapema Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazurui alisema ameziona kambi za Jeshi tatu zanzibar zinatumika katika kuwapatia watu vitambulisho vya mzanzibar mkaazi kinyume na utaratibu. “Nimekwenda mpaka kwenye kambi ya Chukwani, nikakaaa kwenye geti, nikaziona gari tatu namba ninazo wanaingia na vijana ambao ni watoto wadogo na watu kutoka Tanganyika kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya Zan id” alisema Mazurui.

Alisema tayari walishamueleza Rais wa Tanganyika Jakaya Kikwete juu ya Jeshi la wananchi(JWTZ) linavyotumika katika siasa wazi wazi lakini bado hali haijabadilika kutokana na jeshi hilo kuendelea na mchakato huo kama kawaida. Alisema kwa ushahidi walionao kambi ya jeshi Chukwani, mwalimu nyerere, Bububu na Dunga iliyooko wilaya ya kati ndizo ambazo zinahifadhi vijana wa aina tofauti kwa ajili ya kuendikishwa katika daftari la wapiga kura. Akijibu suali juu kushiriki uchaguzi mkuu alisema licha ya uharibifu wote unaotokea hawatosusia uchaguzi na kujigamba kwamba gharama yoyote watashiriki. “Hapa hapana dezo kuwa tuwaachiee CCM wachukua Serikali hivi hivi tuu tutashirikia uchaguzi kwa vyovyote vile itakavyokua”alisema Mazrui. Alisema chama chake kimejipanga kushiriki uchaguzi hata kwa mazingira gani ili kiweze kuwakomboa wananchi na dhulma ilyodumu muda mrefu. Kufuatia wajumbe wa CUF kutoka nje ya baraza hilo mwakilishi wa kwamtipura Hamza Hassan Juma akichangia bajeti wizara ya fedha aliliomba baraza hilo kuongeza siku tatu, ili aweze kupeleka hoja binafisi ya kuwataka wananchi kupiga kura ya maoni kuamua kuwepo au kutowepo serikali ya Umoja wa Kitaifa.

“Waziri ndie anasusia shuhuli za Serikali ndani ya baraza hili kwa kweli ni gumu na si vyema kuendelea na Serikali ya umoja wa kitaifa kwani wezetu hawaitaki” alisema Juma. Alisema kwa sababu mawaziri wote wametoka basi ni vyema na vyombo vya Serikali kuvirejesha.Tendo hilo la kususia kikao cha baraza kinachoendelea kilionekanakana kwamba kimekasirisha wawakilishi wa CCM waliokuwemo wakati huo na kuwafanya wote kutaka GNU ivunjwe. Miezi miwili iliopita akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)Salum kassim Ali alieleza kuwa tume hio haina mafungamano na taasisi yoyote ile katika ufanyaji kazi zake na wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ustadi mkubwa licha ya chama cha CUF kupinga vikali kauli hio kwa mujibu wa taarifa waliotoa kwa waandishi wa habari.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment