Tuesday, June 2, 2015

SEREKALI YA TANGANYIKA IMETUMIA DOLA 29 MILLIONI KUNUNUA MAGARI YA ASKARI YAKIWEMO YA MAGARI YA MAJI YA WASHAWASHA

4chadema (1)

Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi wa Mji wa Vwawa, mkoani Mbeya nchini Tanganyika.
Lissu asema Dk Slaa ni Rais ajaye
Mbozi. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, huenda usiwe huru na haki kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo uamuzi wa Serikali kununua magari ya polisi zaidi ya 700 kwa lengo la kukabiliana na wapinzani. Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi wa Mji wa Vwawa, mkoani Mbeya. Alisema badala ya kutengeneza na kuboresha mazingira mazuri ya uchaguzi, Serikali inaonekana kujiandaa kupambana na wapinzani. “Serikali imetumia dola 29 milioni kununua magari 700 ya polisi, yakiwamo yale maarufu kwa jina la ‘washawasha’. Haya yote wanataka yatumike wakati wa uchaguzi,” alisema Dk Slaa.
Kuhusu vituo vya kuandikisha wapigakura wilayani hapa, Dk Slaa aliwataka mawakala kuwapa ushirikiano wananchi ili waweze kujiandikisha kwa wingi. “Mawakala na viongozi wa Serikali, acheni kuwabagua wananchi kwa misingi ya ushabiki wa vyama vya siasa,” alisema. Alisema ubaguzi wa aina yoyote kwa misingi ya vyama haukubaliki na kwamba kila mmoja ana haki ya kujiandikisha. Aliongeza: “Ubaguzi katika uandikishaji kwa kuwataja wananchi kwa majina ya vyama CCM, Chadema au CUF hautavumilika.”
Akizungumzia wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari kupata haki ya kupiga kura, Dk Slaa alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kuwaruhusu vijana hao kupiga kura mahali popote kutokana na ukweli kwamba siku hiyo watakuwa maeneo tofauti na walikojiandikisha. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mchungaji Stephen Kimondo alisema hivi sasa kuna mpasuko kati ya Serikali na wananchi wake ndiyo maana kila kukicha migomo na maandamano inazidi kutikisa.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment