Wednesday, July 15, 2015

HASARA NA FAIDA IKIWA POMBE MAGUFULI ATAKUWA RAISI WA NCHI YA TANGANYIKA


KAZI KWENU SISI TUKO PALE PALE ZANZIBAR YENYE MAMLAKA KAMILI TUACHIWEE TUPUMUWEEE

1)Moja ya taswira mbaya zinazoweza kujitokeza na kuikumba serikali ya Pombe Magufuli (ikiwa atashinda uchaguzi huko nchini Tanganyika) ni maamuzi ya haraka na yasiyo na tija ya uhakika. Katika utendaji mzuri wa Pombe Magufuli serikalini, madoa makubwa aliyopata ni kwa nyakati kadhaa kusimamia mambo ambayo baadaye yalilalamikiwa sana. Niliwahi kutoa mfano namna ambavyo amewahi kulalamikiwa juu ya maamuzi yake ya kubomoa nyumba za wananchi bila kuwapa muda wa kutosha kuhama. Kibinadamu hayo ni matendo ya ukatili na yanatokana na ufanyaji maamuzi wa haraka katika jambo linalohitaji muda. Sijui kama Pombe Magufuli ataachana na tabia hiyo ya “haraka haraka” ili pia kuifanya serikali yake ijiendeshe kistratejia na kimipango kuliko haraka na nguvu. Ikiwa atasonga mbele na tabia hiyo na serikali yake ikaenda kwa kasi hiyo ya “pupa” kuna uwezekano kuwa kila mambo kumi atakayoyasimamia basi mawili hadi matatu yakawa yanafanywa bila kuwa na tija kwa taifa.
2)Mtihani wa pili ambao unaweza kujenga taswira mbovu ya utawala au serikali itakayoundwa na Pombe Magufuli (ikiwa atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Tanganyika) ni usimamizi wa masuala ya kiuchumi. Eneo hili naliona kama muhimu sana kwa sababu kama nilivyoeleza hapo juu, Pombe Magufuli amekuwa waziri bora katika serikali inayomaliza muda wake na amekuwa akitumwa na kufanya kila jambo haraka kwa wakati na kwa maamuzi yenye misimamo. Sielewi uwanda wake katika masuala ya kiuchumi na misimamo yake kwenye eneo hilo, hapa sina maana kuwa Rais huyu mtarajiwa wa nchi ya Tanganyika lazima awe mchumi, la hasha! Benjamin Mkapa Muuwaji wa Wazanzibari hakuwa mchumi lakini alikuwa na uwezo mpana wa kusimamia uchumi, Jakaya Kikwete aliye waita Waznaibari walima vitungu ni mchumi lakini amefanya vibaya kwenye eneo hilo kuliko Mkapa Muuwaji wa Wazanzibari. Pombe Magufuli amejionyesha mara zote kama mtendaji kuliko “mfikiriaji na mpanga mambo”. Uchumi wa nchi uliopo kama Tanganyika unahitaji akili ya ziada kuweza kuufufua tena, nchi haina viwanda, inanunua kila kitu kutoka nje. JK anaiacha nchi ya Tanganyika ikiwa hoi sana kwenye eneo hilo. Ikiwa Pombe Magufuli ataingia na mtindo wa kusimamia utendaji zaidi kuliko kufikiri na kubuni vyanzo vipya vya uchumi, serikali yake itabeba taswira ya kushindwa kusimamia uchumi.
3)Taswira nyingine ya tatu ambayo si salama na ambayo inaweza kujitokeza kwenye serikali itakayoundwa na Pombe Magufuli ni serikali ya “One Man Show” (serikali ya mtu mmoja). Watu waliozoea kuwa watendaji wa juu kama Pombe Magufuli huwa na kasumba ya kutaka kila jambo liende kama wanavyotaka kila wakati na wakiona haliendi huingilia haraka na kutaka walifanye wao wenyewe, hili ni jambo la kisaikolojia zaidi. Kilema cha serikali za namna hii huwa ni kumjenga mtu mmoja zaidi kuliko wengine si kwa makusudi, bali kwa sababu watendaji wake wanashindwa kwenda na uwezo wa rais wao. Madhara ya hali hii ni kujenga serikali inayokosa vionjo pale ambapo rais anapokuwa hayupo, kunakuwa na hofu ya dhahiri kuwa ni nani anaweza kusimamia masuala mbalimbali kama awezavyo rais na huyo mtu hayupo. Taswira hii itavunjwa tu iwapo mkuu wa nchi ataamua kuwaachia watendaji wafanye maamuzi magumu wao wenyewe, wajifunze kukosea na kukosolewa.
4)Jambo la nne ambalo linaweza kuwa “taswira dhaifu ya serikali ya Pombe Magufuli” (ikiwa atashinda na kuwa raisi wa nchi ya Tanganyika) ni uwezo wa kusimamia masuala ya haki za binadamu na haki za msingi za raia. Hili linaweza kuunganishwa na ile kanuni yake ya ‘kufanya maamuzi kwa mbio na haraka sana kila mara’. Maamuzi ya haraka na yasiyotoa mwanya wa kutosha wa kuzingatia masuala mengine muhimu ya haki za kiraia huwa hayana tija na huumiza dhana ya usimamizi wa haki hizo na yasipokomeshwa huwaumiza raia. Mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ambaye nimeongea naye na hakumpigia kura Pombe Magufuli katika mkutano mkuu huo amenieleza kuwa hakufanya hivyo kwa sababu nyumba yake ya urithi iliwahi kubomolewa bila kupewa muda wa kutosha kwa sababu ilikuwa karibu na barabara. Dhana ya usimamizi wa sheria lazima iendane na dhana ya kusimamia haki za raia, watu wa namna hii wanaweza kuwa wengi na ni kielelezo cha wazi kwamba Pombe Magufuli atawajibika kurekebisha sana taratibu za ufanyaji maamuzi katika serikali yake ili aweze kulinda haki za raia. Serikali yake inaweza kuepukana na taswira hii mbovu kwa kuchukua muda na kutafakari kwa kina juu ya mustakabali wa wananchi kila jambo fulani linapotokea
5)Taswira ya tano mbaya inayoweza kujitokeza katika uongozi “serikali” ya Magufuli ikiwa atachaguliwa kuwa Rais wa nchi ya Tanganyika ni uwezo wa kukiongoza Chama Cha Mapinduzi cha mafisadi. Mtu yeyote hawezi kuwa na shaka na uwezo wa Pombe Magufuli katika utendaji wake muda wote serikalini, lakini kunaweza kuwa na shaka kubwa katika uwezo wa kukiongoza chama chake cha mafisadi. Mahasimu wake kisiasa tayari wameanza kuwa na hofu na uwezo wa CCM mafisadi miaka ya mbele chini ya Pombe Magufuli, namna ambavyo anaweza kupambana na changamoto za kuongoza chama chenye watu wengi wenye maslahi tofauti tofauti sana haswa ufisadi. Ukweli uliopo ni kwamba muda wote ambao Pombe Magufuli amekuwa serikalini hakuwahi kuwa kiongozi mkubwa wa moja kwa moja ndani ya CCM. Jambo hili linatafsiriwa kama linaweza kumsababishia makosa ya kiutendaji kwa sababu ya “kutaka kujinasibisha kama yuko karibu na wanachama wa CCM mafisadi” kumbe akawa anaingizwa kwenye makosa.
6)Mfano mzuri ni wakati anashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM mafisadi na kabla hajataja jina la mgombea mwenza, mara kadhaa alisikika akisema “CCM kwanza, chama chetu kwanza….” Na kisha baadaye ndiyo anasema Tanganyika  ((“Tanzania kwanza”)). Wafuatiliaji wa mambo wanaweza kuanza kuhoji, gia hii ya Pombe Magufuli ndiyo kutaka kuwaonyesha wanachama kuwa yeye anaifahamu CCM vizuri sana...?? Kwa chama kikongwe kama CCM mafisadi unatarajia kiongozi akitanguliza maslahi, kwanza aseme Tanganyika ((“Tanzania kwanza”)) chama baadaye. Kusimama hadharani na kusema “Chama Kwanza, Chama Chetu kwanza…” inaleta mtazamo kwamba anaweza kujikuta anafanya makosa ya kiutendaji katika serikali yake kwa lengo tu la kutaka “kuwaridhisha wana CCM mafisadi”.  Ni bora Pombe Magufuli akajiamini, akajiona ni mwana CCM mafisadi imara na asijione kama vile “kapewa hisani” kuwa mgombea wa chama hicho. Kujiamini kutamfanya akitazame na kukihukumu chama chake bila woga kila mara na pia aitazame nchi yake kama kipaumbele cha kwanza kabla ya chama, kama Rais wa nchi ya Tanganyika.
7)Pombe Magufuli ni mtu mahiri ndani ya chungu kibovu. Ule ule mkakati wa kuiokoa CCM mafisadi mwaka 2005 kwa “kumleta Jakaya” ndiyo unatumika mwaka 2015 tena sijuwi kama Watanganyika wako macho kwa hili au wamelala bado, kwamba CCM mafisadi inajitahidi na inajaribu kutaka kuendelea kuishi kwa kutumia mgongo wa kukubalika kwa mgombea wake, kwamba Watanganyika wakaipigie kura kwa kumuamini zaidi Pombe Magufuli kuliko kutazama makosa ya kihistoria ya chama hicho tangu miaka 50 iliyopita. Kwa Watanganyika waliokata tamaa na uongozi unaomaliza muda wake, aina ya watu kama Pombe Magufuli wanaweza kuwa kimbilio kubwa sana kwa maana ya upigaji kura, lakini hatujui baada ya kura hizo nini kitatokea, maana Pombe Magufuli anakwenda kuzungukwa na wana CCM mafisadi kama alivyo zungukwa Jakaya Kikwete na CCM mafisadi nini kilikuja kwa masikini hakuna zaidi ya mafisadi kuchota mamillioni kwa mamillioni kisha wakibadilishwa wizari bila ya kushtakiwa bali wanalindwa mafisadi katika CCM mafisadi, pia Pombe Magufuli atazungukwa na watendaji lukuki serikalini ambao kwao “kuiba fedha za umma na kufanya utendaji mbovu ni amri ya kila siku na ndio CCM mafisadi walivyo”. Mambo haya yanaweza kuanza kuwa kikwazo kikubwa kwake hadi pale atakapoamua kuchukua hatua thabiti sana.Mimi binafsi napenda kumtakia kila la kheri kiongozi huyu, katika safari aliyoianza.
8)Taswira ya kwanza ambayo pombe Magufuli anaweza kuirejesha bila wasiwasi ni usimamizi thabiti wa serikali na nidhamu ya utendaji ndani ya serikali. Naamini kuwa serikali ya Pombe Magufuli itakuwa ya kiusimamizi na yeye mwenyewe anaweza kulifanya jambo hilo bila kusita. Katika nyadhifa nyingi alizopitia hadi sasa ameijenga taswira hii kila alikopita na bado inambeba hata ikitokea anachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano wa nchi ya Tanganyika.  Tukumbuke kuwa moja ya mambo ambayo yameanguka kabisa nchini hivi ni utendaji ndani ya serikali. Tunafahamu kuwa wafanyakazi ndani ya serikali ukiachilia mbali matatizo waliyonayo kwa maana ya vipato, hata mambo madogo ambayo wangeweza kuyasimamia ndani ya dakika au saa chache huchukua wiki kadhaa na hata miezi kadhaa. Utaratibu wa utoaji huduma umekwama sana na nadhani kama akiwa na uwezo huo atafanikiwa kutatua changamoto kubwa na ya siku nyingi. Ikiwa utendaji wa serikali unaimarika na huduma zinatolewa kwa wakati, Watanganyika mutaweza kujenga taifa linalokwenda mbele bila kujali chama gani kiko madarakani.
9)Taswira bora ya pili ya serikali ya Pombe Magufuli inaweza kuwa ni misimamo katika masuala ya msingi na kutoyumba sana. Pombe Magufuli muda wote ambao amekuwa kiongozi ameonyesha jambo hilo. Kila mara amekuwa na misimamo hata kama siyo sahihi. Kwa tafsiri nyingine hii huwa ni njia bora ya uongozi wa nchi japo kuwa misimamo ya serikali au kiongozi mkuu wa serikali huwa haipaswi kuwa juu ya haki na matakwa ya wananchi. Moja ya mambo ambayo serikali iliyopita ilikosa, ni pamoja na kukosa misimamo na kuwa na “double standard”. Mfano mdogo tu ni kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo Rais anayeondoka alisimamia uanzishwaji bora wa mchakato huo, akaunga mkono katika hatua zote na rasimu zote, lakini akaja kuwageuka wajumbe wa tume hiyo na rasimu yao ya pili alipolihutubia Bunge Maalumu la Katiba. Naamini Pombe Magufuli si mtu wa kugeuka na kuna masuala mengi anaweza kuyasimamia kwa dhati na kila mmoja katika nchi ya Tanganyika akakubali kuwa, naam! Hapa kuna kiongozi anasimamia masuala haya.
10)Taswira ya tatu ya serikali inayoweza kuundwa na Pombe Magufuli ikiwa atachaguliwa kuwa rais ni uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo. Pombe Magufuli ni mtu wa namna hiyo na ametuonyesha katika sekta ya ujenzi na hasa katika eneo la barabara. Moja ya masuala ambayo nayaona kama mafanikio makubwa ya serikali ya Kikwete ni ujenzi wa barabara, ukiniuliza, nitakwambia jambo hili ndilo Kikwete anapaswa kujivunia atakaporudi nyumbani kwake pale ‘Msoga’. Lakini aliyeleta mapinduzi hayo kiusimamizi ni Pombe Magufuli.
11)Mwalimu Nyerere baba wa Taifa hili la Tanganyika aliwahi kusema kuwa “ikitolewa tenda ya ujenzi wa barabara nchini Tanganyika na India halafu nchi zote zikakabidhi tenda hizo kwa watoto wa marais wa nchi, kule India walau barabara ya ‘kudanganyishia’ itajengwa lakini hapa Tanganyika unaweza usione hata kokoto” (tafsiri yangu). Dhana hiyo ina maana kwamba huku kwetu wizi na kujijazia manoti ndivyo vitu vinavyoshamiri kama tulivyo ona kesi za EPA na ESCROW na kwa tafsiri ya Mzee Nyerere “ilipasa Pombe Magufuli awe anaongoza kwa kuchukua noti za barabara na kuzijaza tumboni kwake”,  jambo ambalo limekuwa nadra kutokea na kama liliwahi kuwepo ndiyo tutajua sasa wakati watu wataanza kutoa taarifa zake kwa sababu anataka kwenda Ikulu. Kwa uwezo huu wa kiusimamizi namuona Pombe Magufuli akisimamia miradi ya serikali kwa ustadi mkubwa hata kama siyo “waziri wa miradi” katika serikali atakayoiunda.
12)Taswira ya nne nayoiona katika serikali ya Pombe Magufuli ikitokea anashinda urais wa Tanganyika ni uundaji wa Baraza la Mawaziri na nyadhifa za kiutendaji zilizojaa watu wenye uwezo kuliko marafiki. Serikali za Tanganyika kadhaa zilizopita ikiwamo hii inayoondoka zimekuwa na sifa ya kubeba marafiki kufa au kupona. Siyo siri kwa JK amelalamikiwa mno na mara kadhaa serikali yake ilionekana kama “imejaa washkaji” watu wanaolindana na kuoneana haya kwa heshima za urafiki kuliko kuangalia maslahi ya nchi.
13)Pombe Magufuli anaweza kuwa dawa ya serikali za ushkaji kwani tangu kwenye mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCMmafisadi hakuonekana kama “kitisho” na hakuwa na makundi nyuma yake, penyeza yake ya kimya kimya hadi anakuwa mgombea urais wa CCM mafisadi imemsaidia kuanza kujenga marafiki wasio na masharti ya kutaka kubebwa naye. Marais wengi huunda mitandao na mitandao hiyo huwapa fedha mapema na huwasaidia kila jambo, wanapofika madarakani huwa na deni la kuilipa mitandao hiyo, malipo yenyewe ni miradi ya serikali, tenda mbalimbali na vyeo lukuki. Naamini Pombe Magufuli hatakuwa na tatizo hilo na itamsaidia kutengeneza serikali isiyo na “washkaji kibao.”hapa nchini Tanganyika
14)Taswira ya tano inayoweza kujitokeza ni uwezekano wa kurejesha nguvu ya CCM mafisadi ambayo inasambaratika, na naamini hili linaweza kujitokeza sana hasa kwenye kipindi cha kwanza cha uongozi wake. Siamini kama ataweza kurekebisha taswira ya CCM mafisadi kwa miaka mitano mingine (ikiwa atapata vipindi vyote viwili) kwa sababu hatujaona utendaji halisi wa serikali ijayo, ikiwa CCM mafisadi ndiyo itashinda. Wananchi wengi hawaiamini tena CCM mafisadi na jambo hilo linaweza kuipeleka ikaangushwa katika uchaguzi wa mwaka huu, lakini ikitokea CCM mafisadi inavuka kizingiti na inapona kuangushwa halafu Pombe Magufuli anakuwa rais, anaweza kujizatiti na akatumia miaka mitano kufanya mambo makubwa yatakayowafanya wananchi wa Tanganyika warudishe imani kwa chama hicho. Ila akifanya vibaya sana atazidi kuididimiza. Kwa mtazamo wangu wa msisitizo ni kwamba naona akifanikiwa kwenye eneo hili, japokuwa naweka msisitizo wa pili kuwa ni lazima tusubiri kujua ikiwa atashinda kipindi chake cha kwanza kitakuwaje kiuongozi huyu.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment