Thursday, July 30, 2015

JESHI LA POLISI LAFUNDISHWA NINI HAKI ZA BINADAMU KABLA YA UCHAGUZI JE WALE POLISI WAFICHA NYUSO NAO WATAFUNDISHWA NA KUFUATA SHERIA....???


Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Semina ya Siku mbili kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ili kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika kulinda haki za binadamu kipindi cha uchaguzi. Semina hiyo imefanyika  huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.


Jeshi la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza. Kufanya hivyo kutalipelekea Jeshi hilo kuepuka lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani. Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar. Amesema Jeshi hilo linawajibu wa kuhakikisha Sheria za nchi zinafuatwa lakini jambo la msingi ni kuzielewa Sheria hizo kabla ya kuzitekeleza.


Jaji Mihayo amesema inashangaza kuona kuwa nchi ya Tanganyika na ya Zanaibar inaelekea katika kipindi cha uchaguzi Mkuu wakati Maafisa na Makamanda hawazielewi vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi unaokuja.
1964 NCHINI ZANZIBAR HAWA WAHUNI WALIUWA WATU BURE BURE WAKATHANI WAO HAWATA KUFA WAKO WAPI LEO HII 2015 MBONA HATA HATUWASIKI.............???
MAITI ZA WAZANZIBARI WALIO ULIWA 1964 NA HAO WAHUNI PICHA HAPO JUU LEO YAITWA MAPINDUZI MATUKUFU ASTAHAFIRUH ALLAH.
HAWA NAO WANAITWA POLISI LAKINI HEBU WANGALIYE HIVYO WALIVYO VYAA NA WASHA PIGA WATU RISASI NA KUJERUHI BADHI NA KUPORA VITU VYA WATU KAMA KAMER.COMPUTA INA YA LAPTOP,PESA N.K. NA HAWA NDIO ATI NI POLISI WATAKAO SIMAMIA UCHAGUZI HAPA NCHINI ZANZIBAR

Hivyo amewaomba Maafisa Wawaelimishe Makamanda wenzao juu ya Sheria na kanuni za uchaguzi ili wakati utakapofika watende haki na Wajibu wao bila ya upendeleo. “Polisi kazi yenu nikuhakikisha Sheria zinafuatwa lakini zitafutwa vipi wakati wenyewe hamzijui.....?? alihoji Jambo la msingu ni kuzisoma na kuzielewa kwanza ndio mufanye juhudi za kutekelezwa” alisema Mihayo. Amefahamisha kuwa Jeshi hilo linapaswa kufuata Sheria za nchi bila kufuata matakwa ya Watawala na kwamba Watawala hao watabadilika kulingana na uchaguzi lakini Wananchi wataendelea kuwepo.

“Jeshi la Pilisi linawajibika kwa Wananchi na si Viongozi wa Serikali hivyo nakuombeni mzijue Sheria na muwe wakwanza kuzitekeleza” Alishauri Jaji Mihayo. Kwa upande wake Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Zanzibar Hamdan Makame ameshukuru Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu kwa kuendesha Semina hiyo katika kipindi muafaka cha harakati za uchaguzi mkuu.

Amesema kila mtu ni mlinzi wa haki za binadamu katika kila sehemu anayofanyia kazi nakwamba jambo muhimu ni kuhakikisha Haki zinalindwa hasa ikizingatiwa kuwa suala la haki za binadamu ni lakimataifa. Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Harusi Mpatani ameliomba Jeshi hilo kuhakikisha linawalinda Wananchi wote ikiwemo Watetezi wa haki za binadamu.


Semina hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ni mwendelezo wa kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika kulinda haki za binadamu ili kuufanya uchaguzi unaokuja uwe huru,haki na Salama.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment