Thursday, July 9, 2015

KATIKA HAWA CCM MAFISADI NI YUPI MSAFI AMBAE HAJAWAHI KUPOKEA AU KUTOWA AU YEYE MWENYEWE KULA RUSHWA.....?????

pic+vichwa
Vikao vya maamuzi ya CCM mafisadi vimeanza Giningi Dodoma. Huku wanachama na wapenzi wa CCM mafisadi Macho na masikio yao yakiwa yametegeshwa giningi dodoma kusubiri ni nani fisadi mpy atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya ofisadi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kwa miaka yote ambayo CCM mafisadi imeshirki chaguzi kama hizi huko nyuma, Ni mwaka huu pekee ambapo CCM imekuwa katika wakati mgumu. Ugumu huu unatokana na mambo mengi, Lakini jambo kubwa ni MAKUNDI ya Mafisadi hawa na mgombe wa nafasi ya urais, ambayo kwa kiwango kikubwa kinaitishia uhai wa CCM mafisadi kama vikao hivi havitatumia busara katika hitimisho ya mchato huu. Siyo mara ya kwanza CCM mafisadi kuwa na makundi ya ufisadi wakati kama huu wa uchaguzi, Bali makundi haya yalikuwepo lakini walikuwa wakifanya kampeni zao kwa kufuata kanuni na taratibu za chama bila ya vitisho au kuchafuana. Lakini taratibu makundi haya ya ufisadi yalianza kushinikiza vikao vya maamuzi kuteuwa wagombea mafisadi wanaowataka na hata wakati mwingine kutoa vitisho kwa viongozi na wajumbe wa vikao hivi ili mgombea wao ateuliwe kwa lazima ndio ulaji atiii kila moja ana mawazo akishinda huyu mimi nitakula nae hakuna anae fikiri wananchi ni wao na matumbo yao basiiiiiiiiii.
Kwa mfano kundi la WANAMTANDAO: Kundi hili lilianzishwa mwaka 1995 likiwa na wagombea EDWARD LOWASA na JAKAYA MRISHO KIKWETE. Baada ya lowasa kuenguliwa katika hatua za awali, kundi hili lilihamishia nguvu zake kwa kikwete,ambapo katika hatua za mwisho, Mkapa aliibuka mshindi na hivyo, akateuliwa kupeperusha bandera ya CCM. Kwa kumbukumbu zaidi, Mkapa baada ya kuteuliwa na CCM, Aliwaomba wanaCCM wenzake wavunje makundi ili waingie katika kampeni wakiwa wamoja, Na kuonya kwamba kundi hili la wanamtandao ni hatari kwa uhai wa chama.
WANAMTANDAO WALIKUBALI MDOMONI LAKINI MOYONI HAWAKUVUNJA KUNDI LAO.
Taratibu,kundi la wanamtandao likaanza kujiimarisha kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa kuongeza watu katika kundi hili pamoja na kuandaa mpango mkakati utakaowawezesha kushinda uchaguzi wa mwaka huo. Kwa upande wa mikakati, WANAMTANDAO walianza kuwaweka watu wao katika chaguzi za chama ili wapate idadi itakayowezesha mgombea wao kuteuliwa, KIKWETE. Kwa kuanzia,wanamtando waliwaweka watu wao katika uchaguzi wa ndani ya chama wa mwaka 1997 na uchaguzi wa mwaka 2002. Kwa kumbukumbu zaidi, uchaguzi wa nadani ya chama ya mwaka 2002, Kikwete alilalamikia kura za itifaki zilizopigwa katika uchaguzi huo. Katika kuhakikisha kuwa idadi ya wanamtandao unaongezwa,kundi hili liliwaingiza kundini, wafanyabiasha ,wanachama na viongozi wa CCM mafisadi ,watumishi wa umma pamoja na watendaji katika vyombo vya dola. Baadhi ya wanamtandao waliokuwa wanakundi ni: Kikwete, Lowassa, Rostam, Membe, Sitta, Apson Nwang’onda, Kingunge, Sofia Simba, Makala, Karamagi, Chenge, Noni, Diallo, Meghji nk. Kwa wale wenye kumbukumbu watakubaliana na mimi kuwa, Uchaguzi wa mwaka 2005, Ulitawaliwa na rushwa,kuchafuana miongoni mwa wagombea pamoja na uzushi, vitisho, shinikizo za kila aina,maada mgombea wao ateuliwe. Ni uchaguzi huu ambapo Watanganyika na Wazanzibari walishuhudia Dr Salim akizushiwa kuwa alimuua Karume,mara Hizbul mara mwarabu kumbe hawna lolote CCM mafisadi wanangalia matumbo yao ni kiongozi gani akipita mimi na huyu na yule tutakula manono na sio vipi tutawatatulia wananchi matatizo yao.
Sumaye alizushiwa kuwa ameficha fedha nyingi nje ya nchi, Mwandosya akizushiwa kuwa aliiuza TTCL na mtoto wake anasomeshwa na wanunuzi wa TTCL afrika kusini. Haya yote yalifanyika kwa lengo moja tu!: KIKWETE aingie madarakani kwa namna yoyote ile na sio kiongozi yupi anae faa kuja kuwaokuwa wananchi katika hali duni sio kabisa, iwe kwa uzushi, kwa shinikizo,kwa vitisho au kwa fedha haramu za EPA nk na walifanikiwa, Huku wakiacha maumivu makali kwa washindani wao. Ni hapo ambapo kundi hili la wanamtandao walijiaminisha kuwa Kile watakacho amua kukitenda kitafanyika kwa matakwa yao. Ndiyo maana Lowassa alipoongea na wanahabari siku chache kabla ya kutangaza nia, alisema kuwa walikubaliana na Kikwete kuwa kipindi hiki ni kipindi cha Lowassa kuwa rais wa awamu ya tano ((swali tunawauliza hawa mafisadi je wao ni Masultani....? maana wanarithishana kama Masultani. Vivile Mzee Kingunge wakati Lowassa anatangaza nia Arusha alisea”Ni vyema Lowassa wakakaa na Kikwete ili wamalize tofauti zao. Kwa kuwa kundi hili lilijiapisha kufanya wanayoyataka iwe kwa uhalali au haramu na kujiona kuwa ni wamoja, Walisahau jambo moja muhimu sana, DHAMBI YA UBAGUZI. Madhara yatokanayo na dhambi hii imefafanuliwa vizuri katika hotuba ya baba wa taifa wa nchi hii ya Tanganyika mwalimu nyerere ya mwaka 1995 kilimanjaro hotel,ambpo mwalimu alisema”Dhambi ya ubaguzi ni dhambi mbaya sana, Na ukishaitenda huwezi kuiacha na ni sawa na kula nyama ya mtu”….”Huwezi kutenda dhambi hii halafu ukabaki hivihivi salama”.na ukisha kula nyama ya mtu hutaweza kuwa utaendelea tu kuila ndio haya yanayo toke leo CCM mafisadi wanalana wenyewe kwa wenyewe.
Watu wa nchi ile ile mnapoamua kubaguana ukisema sisi ni na wao ni…Na kwamba mkawaacha wenzeni wa wamebung’aa,wao watabaki salama lakini ninyi ….hamtabaki salama”.DHAMBI HII NDIYO INAWATAFUNA WANAMTANDAO MPAKA LEO. Kwa nini nasema hivyo......??.Unapokuwa ukiwachambua watia nia wa CCM mafisadi, Utagundua kwamba,Ni wanamtandao walewale ambao sasa wamemeguka au wamangatuka na kuwa vimtandao, Na kwamba,Ndio wanaokashifiana ,kuzushiana na kuchafuana maadam mtu wao ateuliwe na CCM mafisadi. Hii inaonyesha kuwa wanamtandao waliomzushia na kumchafua salim hawapo pamoja kama walivyokuwa mwaka 2005,Lakini dr salim aliyeathirika kutokana na kampeni hizo..YUPO SALAMA. Wanamtandao walishindwa kuelewa na kuchambua hotuba ya mwalimu nyerere Baba wa taifa hili Tanganyika ya 1995 kilimanjo hotel/ Kama vikao hivyo vitakapokuwa vimeshindwa kusimamia hili,MAKUNDI NDANI YA CCM MAFISADI HAYATAISHA KABISA,BADALA YAKE CCM MAFISADI ITAKUFA KIFO CHA KUJITAKIA. Baadhi ya majjina ya wanamtandao waliotia nia ni: Lowassa, Membe, Sitta, Nyalandu, Wasira, Migiro, Mwigulu, January, Ngeleja, Kamani, Kitine, Mbega, Mahiga, Bilal, Kingwangala, Muhongo, Amina Salum, Ally Karume na kadhalika.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment