Thursday, July 2, 2015

POLISI AU WAHUNI...? IKIWA SIO POLISI BASI WAZANZIBARI TWASUBIRI NINI WAPITAPO TUWANADIYE KUWA NI WEZI NA TUKIWAPATA KICHAPO CHA GUVU HATA WAKIWA KATIKA GARI MAWE TU

Gari linalotumika na watu wenye kufunika uso
GARI NA WAHUNI WALIOLETWA KUJA KUWATISHA WAZANZIBARI WAENDELE KUTAWALIWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NDIO HAWA KAMA UNAVYO WAONA.MWAKA HUU 2015

HAWA NA WAKATA MAKONGE KUTOKA TANGA NDIO WALIO WAUWA WAZANZIBARI 1964 WATU WALICHUKULIA KAMA MZAHA AU UTANI LAKINI ATHARI YAKE MPAKA LEO BADO INAONEKANA NCHI HAPA ZANZIBAR SASA 2015 MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ANAONA WAZNZIBARI WASHAMKA ANATULETEA TENA WAHUNI KUJA KUUWA TENA JE YATAJIRUDIA YA 1964 AU MARA HII NA SISI TUWATIE ADABU MPAKA WAKOME....??

MAITI ZA WAZANZIBARI WALIO ULIWA NA MANAMBA KUTOKA NCHI YA TANGANYIKA  MWAKA 1964 NA KUITWA MAPINDUZI MATUKUFU
Mpiga Picha Omar Ali Juma
Kundi la watu wasiopungua 20 wakiwa wamefunika nyuso zao na kukamata silaha za moto, mapanga, na marungu jana wamevamia kituo cha Radio (Coconut FM) hapa nchini Zanzibar na kumtisha Mwandishi wa kituo hicho Ali Mohammed aliyekuwa akiendesha mjadala kuhusiana na uandikishaji unaoendelea katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura Zanzibar na kumpiga vibaya Mpiga picha kwa kumcharanga mapanga. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili asubuhi na kuzusha khofu kubwa wa wafanyakazi wa kituo hicho ambapo watu hao waliojifunika nyuso zao wakirusha mapanga juu na kumtishia kumpiga Mwandishi huyo ambaye alikuwa ndani pamoja na wafanyakazi wenzake. “Walikuja kunitafuta mimi lakini wakawa wanatoa vitisho huku wamefunika nyuso zao kwa kweli sisi kila mmoja alikuwa anaogopa na mwenzangu mmoja tuliyekuwa tunaandaa kipindi pamoja yeye alizimia kutokana na vitisho na ule mshituko” alisema Ali Mohammed.IMG-20150630-WA0008WAKISUKUMA GARI LAO BAADA YA KUZIMA GARI NA WAHUNI WALIOLETWA KUJA KUWATISHA WAZANZIBARI WAENDELE KUTAWALIWA NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA NDIO HAWA KAMA UNAVYO WAONA.
Alisema watu hao walikuwa wamebeba silaha hizo na kuchukua msumeno wa moto wa kukatia miti na kuuwasha kwa lengo la kuwatisha huku wakitoa vitisho vikali dhidi ya mwandishi huyo na kituo hicho kinachorusha mijadala ya moja kwa moja na kutoafursa kwa wananchi kupiga simu kutoa maoni yao. Askari hao wametoa kila aina ya vitisho dhidi ya Mwandishi huyo kwa kukaribisha mjadala kuhusu vitendo vya kundi hilo kuingilia utaratibu wa uandikishaji uchaguzi na kumkosoa Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa idara maalumu, Haji Omar Kheri anaesimamia Vikosi vya Zanzibar kwa kusimamia hujuma hizo zinazofanywa wazi wazi bila ya kificho. Mjadala huo ambao uliwashirikisha waandishi wa habari akiwemo Deogratuse Balile, Ali Saleh, Salim Said Salim, wakati kwa upande wa wawakilishi walioshiriki ni Mwakilishi wa CCM Hamza Hassan Juma na Mwakilishi wa CUF Hijja Hassan Hijja. Katika kipindi hicho ambacho kimerushwa moja kwa moja huku wananchi wakishiriki mjadala huo kwa kupiga simu na kusikitishwa kwa yale walioyashuhudia katika mitaa mbali mbali kwa vikosi hivyo kutembea wakiwa wamefunika nyuso huku wabebeba silaha, huku watu kadhaa wakijeruhiwa na watu wasio na sifa kupelekwa kuandikishwa katika vituo ambavyo hawana haki kuandikwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Wakati hayo yanatendekea katika tukio jengine Mpiga Picha, Omar Ali Juma ni mpiga amevamiwa  na kupigwa vibaya jana asubuhi wakati akitoka nyumbani kwake akielekea Mjini kufanya kazi zake na kuumizwa vibaya ambaye amelazwa katika hospitali akipatiwa matibabu. “Nilikamatwa na kuingiza katika gari na watu walovaa Ninja wakanikamata na kunivisha kitambaa usoni wakanipiga sana mpaka nikapoteza fahamu na hapo nilipokuja kupata fahamu zangu najikuta sina chochote wameninyanganya kamera yangu na vitu vyangu vyote kisha wakanitupa ndipo nikapapatua na kufunua uso nikajikuta nipo maeneo ya maisara kituo cha KMKM” alisema. Tukio jengine Ali Makame Khamis amepigwa vibaya na kukatwa kidole na watu waliojifunika uso na baadae kumtupa sehemu ambayo wasamaria wema walimuokota na kumkimbiza hospitali. Hivi juzi Kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari alisema jeshi la polisi halivai vitambaa vya kujifunika nyuso na linafanya kazi zake kwa uwazi halina sababu ya kujifunika nyuso katika utekelezaji wa shughuli zake. “Mimi nimetembea katika vituo sijawaona hao watu mnaosema wamevaa vitambaa vyeusi lakini kama wapo vichochoroni hao mimi sijui” alisema Mkadam.
Hata hivyo katika kikao cha Baraza la wawakilishi Mohammed Aboud aliwahi kuwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba wale ni polisi na wanavaa vile kwa ajili ya usalama wao. hivi karibuni Chama Cha Wananchi (CUF) waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kulalamikia zoezi linaloendelea la uandikishaji ambapo walisema watu wananyimwa kuandikishwa huku ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu ukifanyika mbele ya macho ya watu wa tume na jeshi la polisi bila ya kuchukuliwa hatua zozote. CUF walisema vijana wao zaidi ya 20 wamekamatwa na jeshi la polisi huku watu kadhaa wakiwa wakitekwa nyara na kupigwa kisha kutupwa wakiwa taaban ambapo baadhi yao wanapokamatwa hunyanganywa kila kitu ikiwemo simu fedha na vitambulisho vyao. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Jumuiya ya Waaandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) imelaani kitendo hicho cha kuvamia vituo vya radio na kutishwa kwa waandishi wa habari.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar WAHAMAZA kinalaani kwa nguvu zote kitendo cha makundi ya kihuni yanayojiziba uso kuvamia mara kadhaa kituo cha radio binasfsi cha Cocconut FM kwa kisingizio cha kumtafuta mwandishi Ali Muhammed. Makundi hayo yakiwa katika magari ya Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yamefika kituo cha radio hiyo kiliopo Migombani, Zanzibar kwa zaidi ya mara 8 kudai kumpata mwandishi huyo ambaye leo asubuhi aliendesha kipindi ambacho kilikuwa kikijadili makundi hayo yakiwa yanajifunika nyuso na kubeba silaha kuingilia zoezi la uandikishaji au uboreshaji wa Daftari la Kudumua la Wapiga Kura (DKWK). Taarifa ya WAHAMAZA imesema kitendo hicho hakina afya kwa demokrasia ya Zanzibar na ni hatari sana kwa uhuru wa waandishi wa habari lakini zaidi ni tishio kwa kada hiyo kuelekea Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu. Vitendo kama hivi haviwezi na havipaswi kupewa nafasi katika Zanzibar na Tanganyika.
Imekuwa ikidaiwa kuwa makundi hayo yamekuwa yakifanya vitisho mitaani na kwenye vituo vya kupiga kura na hata kupelekea watu wasiokuwa na sifa ya ukaazi kuandikishwa katika majimbo ambayo hawana sifa nayo, kinyume cha sheria. Mwandishi Ali Muhammed alifanya mahojiano na Waziri wa Vikosi vya Zanzibar Haji Omar Khamis na kisha kuchezesha jawabu zake kabla ya kufungua majadiliano kutoka kwa wasikilizaji ambapo wazi wazi walimshushia lawama Waziri huyo kuhusika na kunyamazia makundi hayo. Ndipo kipindi kikiwa hewani gari tatu za difenda zikiwa na zaidi ya watu 20 wote wakiwa wamejiziba nyuso walifika kituoni hapo na kudai kumpata mwandishi huyo ambaye alikuwemo ndani. Mwandishi huyo amesema watu hao wote wakiwa ni wanaume walikuwa na bundiki aina ya SMG, marungu, mapanga na msumeno wa kukatia miti walitoa maneno kadhaa ya vitisho na kurudi mara nyengine kadhaa kuendelea na madai yao hayo.
WAHAMAZA imesema hali hiyo inadumaza demokrasia na uhuru wa waandishi wa habari na wametaka Serikali ichukue hatua za haraka kuzuia vitendo hivyo. Juzi mwandishi wa kujitegemea aitwae Ali Omar alikamatwa na watu wasio julikana na kuchukuliwa na kupelekwa sehemu ambako alipigwa kisha akatupwa eneo la Maisara mjini Unguja kwa madai kuwa alikwenda kituo cha kujiandikisha kutafuta habari huku yeye eti akiwa ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF. Matukio yote mawili yameripotiwa Polisi ili kupata uingiliaji wao dhidi ya vitisho hivyo na taarifa hizo zipo kwa Kamanda wa Mkoa Mjini Magharibi na Afisa wa Upelekezi wa Mkoa huo pia na wote wameu UFYATAA.
WAHAMAZA imeomba vyombo vya habari na  vyama vya waandishi wa habari waliopo Tanganyika ((Tanzania)) na nje ya Tanganyika waliopo Zanzibar na nje ya Zanzibar kulaani vitendo hivyo na kuitolea wito Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuheshimu uhuru wa waandishi wa habari kufanya kazi na kutimiza wajibu wao bila ya vitisho. Kwa sasa mwandishi Ali Muhammed yuko mafichoni. Tokea kuanza kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura huko Unguja Kaskazini wiki mbili zilizopita, kufika Wilaya ya Magharibi na sasa Wilaya ya Mjini watu kadhaa wamejeruhiwa na makundi hayo na wengine kadhaa kukamatwa kwa sababu ya kuyazuia kufanya uovu wa kidemokrasia wanaotaka kuufanya katika vituo vya kujiandikisha.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Wananchi (CUF) kinalaani vikali kitendo kilichofanywa na kikundi cha watu wapatao 20 wanaosadikiwa kuwa ni askari wa vikosi vya SMZ cha kuvamia kituo cha redio cha COCONUT FM kilichopo Kilimani, mjini Zanzibar jana tarehe 29 Juni, 2015 na kumtisha mwandishi Ali Mohamed wa kituo hicho kwa sababu ya kuandaa kipindi maalum kilichokuwa kikijadili hali ya vitisho inayoendelea katika uandikishaji wa wapiga kura. Tukio hili ambao limefanywa na askari hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa staili ya NINJA huku wakiwa na silaha za bunduki za SMG, mapanga, marungu, na msumeno wa Chain Saw na wakitumia gari zenye namba za vikosi vya SMZ ni muendelezo wa vitendo vya kukamata, kuwateka nyara, kuwapiga na baadaye kuwatupa kwenye vichaka watu kadhaa vilianza pale uandikishaji wa wapiga kura ulipoanza katika kisiwa cha Unguja.
Kitendo cha kuvamia COCONUT FM na kumtisha mwandishi Ali Mohamed na wafanyakazi wengine ni kitendo kinacholenga kuvinyamazisha vyombo vya habari na waandishi wa habari ili waogope kuanika uovu unaofanywa na vikundi hivyo katika jamii. Kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote, watetezi wa haki za binadamu na kila anayeamini katika Utawala bora. Inasikitisha zaidi kuona Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao linaiona hali hii ikifanyika mbele ya macho yake na halichukui hatua zozote kuzuia. Badala yake tunawasikia Wakuu wa Jeshi la Polisi wakisema wao hawahusiki na vikundi hivyo. Ni dhahiri kwa hatua hizo na matamshi hayo, Jeshi la Polisi limeamua kukimbia dhamana zake.
Hali hii imeleta taharuki kwa wananchi wa Zanzibar ambao wengi wao wakiwa ni Waislamu wanaendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku wakiwa wanakosa amani na utulivu hata wa kufanya ibada zao. Hatukutegemea katika zama hizi baada ya Maridhiano yaliyofikiwa mwaka 2009 ambayo yalileta siasa mpya za maelewano kwamba Zanzibar ingerudishwa tena katika siasa za hujuma, vipigo, vitisho na uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya Utawala bora. Kutokana na hali hii: sisi katika chama cha CUF tunasisitiza haja ya kuchukuliwa hatua zifuatazo:
  1. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, kuchukua hatua za kukomesha matukio haya na kuirudisha Zanzibar katika hali ya amani, utulivu, umoja na maelewano kama ilivyokuwepo wakati anakabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi hii na mtangulizi wake, Dk. Amani Abeid Karume, mwaka 2010.
  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANGANYIKA ((Tanzania,)) Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, achukue hatua za  kuhakikisha kuwa vyombo vyenye dhamana ya kusimamia ulinzi wa raia na mali zao vinatekeleza ipasavyo majukumu yake.
  1. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amwajibishe kisiasa Waziri mwenye dhamana ya Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheri, ambaye vikosi vilivyo chini yake ndivyo vinavyofanya uovu huu.
  2. Iundwe tume huru ya uchunguzi itakayoshirikisha mashirika ya kimataifa yanayosimamia haki za binadamu ili kuchunguza na kubainisha ni nani wanaohusika na kutoa maagizo haya na utekelezaji wake na watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.
  1. Jumuiya ya kimataifa ifuatilie kwa karibu matukio yanayoendelea Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na mwenendo wa mambo kwa ujumla na kuweka kumbukumbu sahihi ili kuona kama matukio haya hayavunji wajibu wa Jamhuri ya Muungano wa ((Tanzania)) katika utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa inayohusu haki za binadamu na Utawala bora ukiwemo ule unaohusu wajibu wa ((Tanzania)) katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
HAKI SAWA KWA WOTE
Ismail Jussa
Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA TUNASEMA HIVI....IKIWA NI POLISI KWELI BASI KAMISHNA,MKUU WA UPELELEZI MKUU WA VIKOSI SMZ WOTE WAJIUZULU NA KUPELEKWA MAHAKAMANI KWA KUTAKA KUMWAGA DAMU NDANI YA NCHI KWA KUTUMIA VIJANA WAFICHA NYUSO NINJA KWA KUHUJUMU RAI WEMA WASIO NA HATIA.
KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment